Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Mkuu umeongea saana lakini bado unabaki kule kule katika ushabiki na hisia kuliko uhalisia! hayo unayosema yoote ni katika kutafuta huruma kwa wanananchi bila ya kuleta suluhu! Suluhu ni wapinzani kuacha maneno kufanya kazi kwa vitendo ionekane dhahiri kwa wananchi sijui kama kuna tawala itaweza kuzuia nguvu ya umma inayokubalika kwa wananchi wote bila kujali tofauti zao mfano kwa utendaji wa mbunge joseph haule jimboni kwake sioni kama kuna mtu anaewaza kuwa atatoka leo au kesho jamaa anakubalika kwa asilimia nyingi hata na hao wanaccm japo bado wenye uchu wa madaraka wanampinga kimtindo kwa kuwa jamaa yupo karibu na wananchi wake na anafanya kazi zao kwa kadri ya uwezo wake kama alivyokuwa yule late filikunjombe na ludewa hii ni miongoni mwa suluhu kwa upinzani kushika dola ila kama wapinzani wataendelea na siasa za kiharakati za kina lijualikali,lema kelele yingi majungu na kutia hamasa za fujo na chuki hakika vipigo kwa wafuasi wa upinzani havitawaacha salama sababu tz ukiwa mbwatukaji watu watajaa kukusikiliza kwa kuwa ni nchi yenye raia wanaopenda kusikia umbea, majungu, fulani kamsema fulani, but hawako tayari kukussuport katika mambo ya hovyo japo kuna watakaonaswa kutokana na sababu mbalimbali mfano kutokuwa na umri wa busara na mob psychology! Ukiangalia nchi za kiafrika ambazo upinzani umeweza kuwaondoa watawala mostly watu hao walijenga imani kwa wananchi kupitia kazi zilizonekana na sio maneno ya kelele mfano mfuatilie late michael satta wa zambia mfuatilie macky sally wa senegal ambae ni mkristo anaetawala taifa lenye 90% ya waislamu,adama barrow gambia kupitia Majum Real Estate aliweza kutoa ajira nyingi kwa vijana wa kigambia mwisho wa siku kaja kumng"oa kigogo yahya jameh. Wapinzani wa nchi hii kama wana dhamira ya kushika dola na si kula ruzuku kwa vyama vya familia zao, lazima waache usanii kwa kuwapumbaza watu na kutafuta huruma kwa wananchi wafanye kazi kweli kwani na wawe karibu na wananchi sidhani kama kuna mtu atakubali kupewa t shirt na kanga sijui na chumvi aunge mkono watu wasio karibu nao wala kuwajali. Nina hakika kupitia tume hiyo hiyo ndio iliyowaptia hao wabunge na madiwani sasa iweje sehemu upinzani ukishindwa tume hiyo iwe mbaya?? Mzee lowasa alitoa wosia mzuri sana kwa mameya walipoenda kumtembelea ofisini kwake pale mikocheni KUWA NENDENI MKAFANYE KAZI WATU WAONE TOFAUTI YA SISI NA WAO nadhani hii ndio silaha pekee ya upinzani kuwin the situation pia akongeza kule arusha katika mkutano wa madiwani wa Ukawa TUACHE SIASA ZA KIHANAHARAKATI TUJENGE CHAMA TOKEA KATIKA MASHINA YA CHINI KABISA nadhani wewe pia unaweza kuwa shahidi wanazi na mashabiki wa Ukawa walivyomponda mzee huyu. Mdau hamna shortcut katika maisha upinzani lazima ufanye kazi kubwa na si kubwata bwata, kuzungusha mikono,kumsema rais vibaya,kushadadia nyufa za hostel, kupaka watu rangi na kusema wamepigwa mapanga,(ushawahi kujiuliza hali zao zinaendeleaje baada ya uchaguzi) kuandaa vijana kuzuia kina mama kwenda kupiga kura,kuzungumzia sana mambo ya chama tawala kuliko ya chama chao,Kuhamisha magoli kuwa mtu akihama kanunuliwa basi kama ni hivyo hamna mtu mwenye akili timamu atakepigia kura mtu ambae baadae atanunuliwa.Upinzani Lazima ufanye kazi na uache usanii wa kihanaharakati
Naona unapanga nadharia nyingi bila uhalisia, kama utendaji ndio kigezo cha kuchaguliwa hivi leo ccm isingekuwa madarakani. Ni kweli kuna walioshinda uchaguzi kwa utendaji ila hao ni wachache sana. Wengi wao wameingia kwa sababu zilizo nje ya utendaji. Kwa taarifa yako 50% wameshinda nafasi zao kwa rushwa, wizi wa kura, hofu kwa wapiga kura na udhaifu wa tume ya uchaguzi. Kwenye washindi wa hivi kuna wengi wazuri wameachwa.
Kwa mujibu ya maelezo yako waliochaguliwa ni wale kazi zao zilizoonekana kwa jamii inayowazunguka. Nakuambia watu wameumizwa kisa madaraka, ww unaniambia eti wamepakawa rangi ili kupotosha ionekane ule ulikuwa uzushi kwakuwa hutujui wahanga wanaendeleje sasa. Hivi unadhani unaongea na mtoto hapa? Watu wangapi wamepata matatizo tena yaliyotambuliwa kitaifa umewahi kuona baada ya matukio hayo taifa likifuatilia kujua hali zao? Wahanga wa tetemeko la Kagera umewahi kusikia wanaendeleaje? Wanaopata ajali za barabarani na kutangazwa baada ya hapo huwa unajua hali zao zinaendekeaje? Huenda una hoja lakini unaziwakilisha kwa utetezi dhaifu.
Kuchaguliwa kwa nafasi za kisiasa sababu kubwa kabisa huwa ni hoja za ushawishi. Utendaji huwa ni sababu nyingine, mvuto pia huchangia mtu kuchaguliwa. Ila ushawishi wa kisiasa huwa ni sababu kubwa. Sasa ww kuja hapa na kuniambie eti cdm ili ichaguliwe ni lazima ifanye sana kazi ndio ikubalike ni kama unanifanya sijui sababu zinazochangia mgombea kuchaguliwa. Sababu ziko nyingi na sasa zimeingia za ukabila na ukanda bila kujali hilo la utendaji unalolazimisha kuwa ndio sababu pekee.