Timothy Peter Thomas
Senior Member
- Jan 23, 2013
- 114
- 48
Sina imani kama majibu yangu yatamridhisha mleta mada hapa kwa kuwa tayari ameonesha kupingana na uhalisia..
HATA HIVO NITAJARIBU.
Katika hali ya kawaida, Baba ni kiongozi na mwanzilishi wa familia. Hii inaapply hata kama baba huyu si mzazi wa kibiolojia wa mtoto.
Tukubali kitu kimoja cha msingi sana. Baada ya kupata uhuru wa Tanganyika, Tanganyika ilifanyika kuwa familia.. Raia wake walianza kushiriki kikamilifu kufanya maamuzi juu ya Taifa lao. Wote kwa pamoja tuliipata heshima iliyokosekana kwa zaidi ya miaka 120!! Tukaanza kujituma wenyewe kwa maslahi yetu na ya nchi yetu badala ya kutumikishwa na wazungu kwa maslahi yao na mataifa yao. HII ILIKUWA NA KILA ELEMENT YA FAMILIA. Baba wa Taifa, mwalimu J.K. Nyerere alilisimamia hili akishirikiana na mlolongo mrefu wa wapigania uhuru, wengine tunaowataja katika historia na hata wale ambao historia haiwataji, walio hai leo na wale waliotangulia. Mwalimu aliikamilisha kazi njema ambayo baba na babu zetu akina Kinjekitile, Mkwawa, Mirambo, Isike na wengine wengi waliifanya miaka mingi kabla. Historia na masimulizi yanazielezea juhudi za Baba wa Taifa katika kufanikisha mapinduzi ya Zanzibar na hata uhuru wa mataifa mengine ya Afrika. Baada ya mapinduzi ya Zanzibar, mwalimu pamoja na wapigania uhuru wa Zanzibar, hawakuona sababu ya kuwa na nchi mbili ilhali umoja ndiyo iliyokuwa falsafa yao. Zanzibar ikaungana na Tanganyika kuunda Tanzania. Muungano huu ulileta mtoto mpya, taifa la Tanzania. Hapa mchango wa Mwalimu ulikua mkubwa,wa kipekee na uliotukuka. Nyingi ya hotuba zake zinaonesha namna alivyopendezwa na umoja wa waafrika.
Wapigania uhuru wenzake, wengine bado tuko nao leo (Mwenyez Mungu awape heri ya maisha marefu zaidi) waliridhia Nyerere aitwe BABA, na walimwita hivyo tangu siku za awali za uhuru..
HUYU NI BABA!
HUYU NI MSINGI WA UANZISHWAJI WA TAIFA LA TANZANIA!
HUYU NI CHIMBUKO LA MAFANIKIO YA JUHUDI ZA KUJIKOMBOA!
R.I.P BABA WA TAIFA..