Rugas
JF-Expert Member
- Jan 8, 2009
- 1,048
- 197
Kikaptula Alichovaa Michelle Obama Chazua Mjadala Mrefu
Je mke wa rais haifai kuvaa kaptula?
Wakati Michelle Obama alipovaa nguo ambayo ilionyesha mabega na mikono yake wazi mjadala ulizuka kuhusiana na nguo zipi ni sahihi kwa mke wa rais kuvaa, hivi sasa umezuka mjadala mwingine kama huo baada ya Michelle Obama kutinga na kikaptula kifupi. Picha za kikaptula hicho cha Michelle Obama mwisho wa habari hii.
Mke wa rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama amezidi kuonyesha tofauti yake na wake wa marais waliopita wa Marekani. Michelle amekuwa mke wa kwanza wa rais kuvaa kaptula na kupanda dage la rais Air Force One.
Obama, mkewe na binti zake walikuwa Arizona katika vakesheni yao binafsi ya kutembelea sehemu mbali mbali za kitalii katika jimbo hilo lakini vyombo vya habari badala ya kushughulika na ziara ya mkuu huyo wa taifa kubwa duniani, walikuwa bize kupata taswira za kikaptula cha mke wa rais.
Vyombo vingi vya habari vya Marekani vimekuwa vikijadili nguo anazovaa Michelle Obama kama zinafaa kuvaliwa na mke wa rais au la huku watu wengine wakitoa maoni kwamba Michelle ni mwanamke kama wanawake wengine hivyo ana haki ya kuvaa atakavyo.
>
nini maoni yako