Ukiwa kama mzazi, vitendo kama hivi vinaweza visikuathiri wewe moja kwa moja lakini vinawaweka kwenye wakati mgumu sana mke wako na watoto. Just imagine mkeo yupo saluni au sehemu ya mkusanyiko halafu mmoja wapo wa wateja anatoa simu yake na kuanza kuangalia hiyo video.. wanaanza kucheka na kusema "huyu si mume wa fulani?" Au watoto wako shuleni wanaanza kuchekwa na wenzao na kutaniwa kisa baba yao unafanya vituko kama hivi. Mtoto anajikuta anakua mnyonge hata kujibu swali darasani hathubutu!
Jifunze kutafuta ugali kwa njia ambazo hazikudhalilishi bila sababu na kuwaletea matatizo wale uwapendao ambao kimsingi ndio unaowatafutia maisha.