Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
- Thread starter
- #41
Baada ya baadhi ya viongozi wa Simba SC walioshiriki kikao na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali timu hiyo icheze Dabi ya Kariakoo tarehe 25 Juni, hali ndani ya klabu hiyo si ya utulivu.Ni kweli mpira wetu unaenda kufa ni suala la mda tu
Taarifa kutoka ndani ya Simba SC zinaeleza kuwa viongozi wengine wa juu wa klabu hiyo hawajakubaliana na maamuzi hayo, wakieleza kuwa hawakushirikishwa kwenye maamuzi hayo muhimu kwa mustakabali wa timu. Mvutano huo wa ndani ndiyo sababu kuu ya klabu hiyo kuendelea na ukimya wake hadi sasa, licha ya kuwepo kwa ratiba rasmi ya mchezo huo kutoka Bodi ya Ligi.
Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Simba kilichofanyika leo asubuhi kinatarajiwa kutoa mwelekeo sahihi wa msimamo wa klabu hiyo kuhusu kushiriki au kutoshiriki Dabi hiyo. Mashabiki na wadau wa soka wanalisubiri tamko hilo kwa hamu kubwa.
Taarifa hii inakuja katika kipindi ambacho upande wa wapinzani wao, Yanga SC, tayari umeonesha utayari wa kushiriki mchezo huo baada ya baadhi ya masharti yao kutekelezwa na TFF, ikiwemo kupokea barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na hatua ya kumsimamisha Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo.
FOLLOW The Street Media