Kiki ya derby ya Kariakoo ndio imebamba ila tunaua soka letu

Ni kweli mpira wetu unaenda kufa ni suala la mda tu
Baada ya baadhi ya viongozi wa Simba SC walioshiriki kikao na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali timu hiyo icheze Dabi ya Kariakoo tarehe 25 Juni, hali ndani ya klabu hiyo si ya utulivu.

Taarifa kutoka ndani ya Simba SC zinaeleza kuwa viongozi wengine wa juu wa klabu hiyo hawajakubaliana na maamuzi hayo, wakieleza kuwa hawakushirikishwa kwenye maamuzi hayo muhimu kwa mustakabali wa timu. Mvutano huo wa ndani ndiyo sababu kuu ya klabu hiyo kuendelea na ukimya wake hadi sasa, licha ya kuwepo kwa ratiba rasmi ya mchezo huo kutoka Bodi ya Ligi.

Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Simba kilichofanyika leo asubuhi kinatarajiwa kutoa mwelekeo sahihi wa msimamo wa klabu hiyo kuhusu kushiriki au kutoshiriki Dabi hiyo. Mashabiki na wadau wa soka wanalisubiri tamko hilo kwa hamu kubwa.

Taarifa hii inakuja katika kipindi ambacho upande wa wapinzani wao, Yanga SC, tayari umeonesha utayari wa kushiriki mchezo huo baada ya baadhi ya masharti yao kutekelezwa na TFF, ikiwemo kupokea barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na hatua ya kumsimamisha Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo.

FOLLOW The Street Media
 
Ee Mungu baba ikikupendeza juu ya soka la tz , fifa ikafanye lolote..
WADAU WAMTUMIA TAARIFA MICKY FIFA IIFUNGIE TANZANIA

Kuna watu wanamiminika kutuma meseji kwa huyu mtangazaji Micky Jnr wakitaka FIFA ilifungie Tanzania kutokana na serikali kusuluhisha mgogoro wa kimpira kati ya Young Africans SC, bodi ya ligi kuu, TFF na Simba SC.

Hii imekaaje, Ina Afya kwenye Soka Letu ?

#mrreporter
 
Shabiki Nguli na Mwanachama wa Simbasc Aggy Simba ameandika Haya kwenye Instagram yake Baada ya Derby kupangiwa Tarehe Mpy

“Siwezi kuwa mnafki aisee tumevuliwa nguo, tumedhalilika, niseme tu nyuma mwiko wanapendelewa sana.

Aliyetuzuia Simba tarehe 8 ni nani?? Na wamechukuliwa hatua gani?? Kiongozi aliyepiga simu geti la Benjamin Mkapa lisifungulie nani???

#HiiniyakilaMmoja
 
#pumzika salama Mdude

 
Mechi ili ahirishwa siku ambayo lisu alikuwa mlimani City kutangaza no reforms no election siku ya wanawake.
Bibi samia alikuwa mwanza kwenye siku ya wanawake.
Ili lisu asisisikike ilibidi mechi iahitishwe.
Kesho wanakwambia ccm inakubalika. Hivi huwa hawaangalii hata trends za watu kufuatilia bunge na mambo mengine.
Wakamwambie kwanza mzee wasirq akatoe MJINI YAKE PALE MBUYUNI karibu na St. Peters ili barabara ya mwendo kasi ipite
 
Mbunge mstaafu mh Mangungu ambaye ndiye boss wa Simba amesema Derby ya kariakoo ni kesho 🐼
Hamna kitu mule!! Ukitaka kujua mule hamna kitu muhoji mamb ya msingi hawez kujibu kwa weledi 🤣🤣🤣🤣atapiga blah blah then anaingia mitini!!!
 
Ndugu yangu kazi tuliyonayo kwa sasa na huko mbele ni NO REFORMS NO ELECTION baaasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…