Kikokotoo cha Mafao bado ni kilio kwa Askari Polisi

Na kwa kuongezea tu, hiyo 33% hawatapewa kwa mkupuo mmoja kama wanavyoota!

Wastaafu wenzao wa toka 2019 hadi leo wanasotea mafao baada ya kulipwa pungufu kisa michango yao haikupelekwa PSSSF na mwajiri.
 
Nakumbuka waziri Jenista Mhagama ndo alituingiza kwenye hili janga la kikokotoo wakati akihudumu kwenye secta hiyo, toka wakati huo sijawahi kumuelewa kabisa huyu mama.
 
Si rahisi kustaafu hiyo kazi bila kuwa na laana.

Wachache huwa na uzee mwema na watoto wao hufanikiwa.
 
Mafao mengi yana masharti magumu kuzikwapua pesa zako, kodi pia ni vyema sasa mifuko kulegeza kamba wafanyakazi wachukue pesa zao walikatwa kwa lazima kuchukua nayo ni tatizo, tucta vyama vya wafanyakazi wana kazi gani kama hawawezi kutetea maslahi ya wafanyakazi.
 
Selekale ina matumiz ya hovyo hela wanazichukua za mifuko na kuzifuja. Hakuna awamu imezifuja kama ya mpwani jk.
Kwa upande wa polis wapambane na hal yao wao si hujiona sehem ya utawala wacha wakomeshwe na hao wanaowatuma
 
Mifuko yenu haina hela...serikali ilizichukua ikajengea miradi mikubwa...nyingine wanasafiria.
Kwahiyo, vumilieni tu sababu wakitoa hicho kikokotoo, mtakosa kabisa.
 
Sasa hiyo 17 milioni si unaweza kumalizia beach kidimbwi kwa miezi miwili kisha ufe kwa stress!
 
Ndiyo maana wakati mwingine hasira ya Mapolisi inaishia kwa raia!
Sasa hapo Askari wataacha kupokea rushwa, kushiriki vitendo vya unyanganyi,nk?
 
hakuna wa kumtetea polisi ila ni polisi mwenyewe,au polisi mwenzake.

kikokotoo ni mwiba kwa baadhi ya watumishi,ila kwa polisi ni mkuki kabisa.
kabla ya kikokotoo tayari polisi walikuwa na kiinua mgongo duni kuliko mtumishi yoyote,mfano huyu cpl anayemtaja mletamada,kabla ya kikokotoo alikuwa hafikii malipo ya shilingi milioni 30,kwa utumishi wa miaka 30 sawa na mwaalimu wa muda huo ambay kabla ya kikokotoo alikuwa anapata zaidi ya milioni 70.
leo hii cpl huyu anapewa milioni 17,wakati mwalimu yule anapewa milioni 50 na zaidi.

haifahamiki ni kigezo kipi kimetumika kuamua hilo,ni kama mwenye nacho kapunguziwa kidogo,na asiye nacho kaporwa zaidi.
kama kigezo ni kada zenye watumishi wengi,bado ingekuwa na maana kama wangepeleka hicho na kwa jeshi la ulinzi ingawa bado haihalalishi,lakini bado haieleweki ni nani yuko nyuma ya hili.

kwa hali inavyoendelea si ajabu mabadiliko ya nchi hii yatakuja kuletwa na polisi wenyewe,iwe wao kuanzisha vurugu,ama kuruhusu haki itendeke kwenye box la kura,vinginvyo wataendelea kutumika na ccm kama condom tu kwa jeuri isiyo na mfano
 
...wamehoji busara iliyotumika kuwaondoa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa nini haikutumika kwa askari wa Jeshi la Polisi na Magereza.
Mwenye kisu KiKALi ndiye hula nyama
 
Your browser is not able to display this video.
 
Huyo askari Polisi aliyetoa maoni ninamsikitikia kutokuwa muelewa wa mambo mengi.

Kwanza aelewe kwamba, sheria zilizounda jeshi la Polisi, Zimamoto ama Magereza na sheria zilizounda Jwtz ni sheria mbili tofauti kabisa.

Jwtz hawaajiriwi, wao wanaandikishwa, halafu Pensheni zao huchukulia hazina, hawajaunganishwa na mifuko ya hifadhi za jamii.

Cha kutetea yeye ilitakiwa ashauri kurekebishwa kwa sheria kandamizi zinazowanyima wao maslahi.

Haya mambo ya kulinganisha na taasisi tofauti na uliyopo bila kujua kwa ufasaha yaliyomo katika mfumo wa kule ni sawa na kusema: ...mbona mimi nafungwa kwa kosa la wizi, wakati mwizi mwenzangu aliiba kama mimi lakini yeye aliachiwa huru?...

Pigania kurekebishwa kwa sheria na siyo kulinganisha na taasisi zingine usizozielewa kiundani wake.
 
Kuna polisi hapa mtaani alustaafu mwaka Jana, anatia huruma. Ameuza mikweche yote na mke kamukimbia. Kwa cheo alichostafia ndo anakamua 200k Kwa Sasa.


Polisi wengi hawavuki ukaguzi...... So watanyoooka
 
Polisi hata wawakate kias chote sawa ,nyie ndo mnatumika kisiasa sana ,kuiba kura ,kuua ,na kipigo kikubwa wakat tunapiga kura kuwaondoa wetesi wenu madarakan!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…