Kikokotoo kilivyomtenda mstaafu Jeshi la Magereza

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Aliyekuwa mtumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania, Salum Shamte (56), amesimulia namna kanuni za kukokotoa mafao (kikokotoo) ilivyosababisha apigwe butwaa baada ya kupokea ujumbe (sms) wa kiasi cha fedha za pensheni ya kustaafu alicholipwa.

Anasema alipokea sms ikionyesha malipo ya Sh21 milioni badala ya Sh55 milioni aliyotarajia baada ya kuitumikia Serikali kwa miaka 33.

Alipotafutwa na Mwananchi, Kamishna Jenerali wa Magereza, Mzee Nyamka amesema utaratibu wa malipo ya pensheni haupo kwa Mkuu wa Magereza, Waziri wa Mambo ya Ndani au Katibu Mkuu.

"Mfuko wa pensheni ya kustaafu unalipwa kulingana na michango aliyotoa na kikokotoo kinazingatia utaratibu huo,” amesema.

"Pensheni halipi CGP, Waziri wa Mambo ya Ndani au Katibu Mkuu, ila inategemeana na michango yake aliyoitoa," amesema.

Salum aliyestaafu akiwa na cheo cha Staff Sajenti Kikosi Maalumu cha Kutuliza Ghasi Magerezani (KMKG), Dar es Salaam, anasema aliposoma ujumbe huo alihisi macho yake yana ukungu kiasi cha kutokusoma vizuri tarakimu.

"Niliomba msaada wa mke wangu anisomee, akanitajia vilevile. Miaka 33 napata Sh21 m

ilioni na kiasi hicho nimekatwa Sh10 milioni, nilikuwa nimekopa Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS Saccos)," anasema Salum.

Screenshot 2024-05-20 110641.png
Mstaafu huyo aliyetembelea ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tabata Relini anasema licha ya kufanya kazi kwa uadilifu, kikokotoo kimeathiri ndoto zake.

Salum anasema alitarajia baada ya kustaafu akanunue maeneo aanzishe shughuli za kilimo.

"Najiona mfungwa mtarajiwa, kwa sababu Sh10 milioni zilizobakia kuna baadhi ya watu niliwakopa muda wote wanazengeazengea nyumbani kwangu wakihitaji niwape chao,” anasema.

"Hata nikitoa hakitatosha, nitaishi katika mazingira magumu. Nashindwa kusimulia, tunafanya kazi katika mazingira magumu ni kama vile Serikali haitambui umuhimu wetu. Kikokotoo sikujua makali yake, sasa najionea," anasema.

Salum anasema mwanzoni wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo alikuwa anaona kawaida lakini ameona ukali wake, hivyo kutoa wito kwa watumishi wengine wasijione wako salama.

"Familia yangu hainielewi inahisi nimekula fedha, lakini hata wale niliowakopa nao hawanielewi, wanasema nina fedha niwalipe chao wakafanye shughuli zao. Ninaishi kama digidigi, muda wote nalala ndani," anasimulia.

Anasema hali ilikuwa ngumu, mke wake na baadhi ya majirani wakamtuliza kwa kumtaka awe na subira.

“Nilipofuatilia kwenye uongozi wa Magereza waliniambia Serikali imeshaamua na sisi hatuna namna nyingine ya kukusaidia, kikubwa ridhika.Kuna wengine walikuwa wananishauri nisubiri tamko la Serikali kusitisha kikokotoo,” anasema.

Anaeleza aliposikia kauli ya Serikali siku ya Mei mosi kupitia kwa Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango haoni mwanga.

Katika Sherehe za Mei mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Arusha, Dk Mpango alisema uamuzi wa kukibadilisha kikokotoo utatokana na tathmini ya kina ya kisayansi ya watakwimu bima.

Salum anasema,“nimeona nipaze sauti yangu kupitia vyombo vya habari ili familia na wale wanaonidai wajue maana kila nikiwaeleza hawanielewi kabisa. Na Serikali ijue shida tunazozipitia, na sisi tuna mahitaji na mipango mingi.”

“Rais inawezekana halifahamu hili kama sisi wastaafu tunapitia shida hizi, atusaidie vinginevyo tutakufa tuna majukumu mazito ikiwamo kusimamia familia,” anasema.

Salum anasema hata wakati wanaanza kutoa elimu ya kikokotoo hicho walielezwa watakatwa kidogo sehemu ya mshahara wao baada ya kustaafu na utakaribiana na waliokuwa wanapokea walipokuwa wakifanya kazi.

Anasema baada ya kustaafu kwa mwezi anapokea Sh290,000 wakati kipindi anafanya kazi mshahara kwa mwezi ulikuwa Sh745,000.

Historia yake
Salum mzaliwa wa Rufiji mkoani Pwani anasena alianza kazi Jeshi la Magereza mwaka 1990 Kiwira mkoani Mbeya akiwa Kuruta.

Anasema alijiunga rasmi na Jeshi hilo mwaka 1991 katika Gereza la Maweni mkoani Tanga.

“Mwaka 1992 nilihamishiwa Gereza la Chumbageni, lakini mwaka 1993 nilirudi tena Maweni, baadaye mwaka 1994 nilihamishiwa Kikosi Maalumu cha Kutuliza Ghasi Magerezani (KMKG), Dar es Salaam,” anasema.

Mwaka 1996 hadi 2006 alihamishiwa Kisongo katika Gereza la Umoja wa Mataifa Arusha walikokuwa waanzilishi kabla ya kuhamishiwa Dar es Salaam kuendelea na kazi KMKG hadi alipostaafu mwaka 2023.

Msimamo wa Serikali
Hoja ya kikokotoo iliibuliwa katika risala ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), iliyosomwa Mei mosi 2024.

Dk Mpango aliyemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan alisema uamuzi wa mabadiliko ya kanuni hiyo, utatokana na tathmini ya kina ya kisayansi ya watakwimu-bima na Serikali inaamini Tucta itawasilisha maoni yake.

“Tunawategemea wataalamu wetu watushauri kuhusu suala hili la uhimilivu na uendelevu wa mifuko ya hifadhi ya jamii, tunawahakikishia wafanyakazi hakuna mtu angependa kuona watu waliotumikia nchi hii wanaathirika kwa kukosa kiinua mgongo stahiki au pensheni zao,” alisema.

Kwa mara kadhaa suala la kikokotoo limekuwa likiibuliwa bungeni na wabunge wakitaka Serikali kufanya marekebisho.

Suala la kikokotoo lilianza kufukuta mwaka 2018 baada ya iliyokuwa Mamlaka ya Kudhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuandaa kanuni mpya zilizolenga kukipunguza kwa watumishi wa umma kutoka asilimia 50 hadi asilimia 33 na kupandisha kutoka asilimia 25 hadi 33 kwa watumishi wa sekta binafsi.

Hatua hiyo ilipigiwa kelele na watumishi wa umma, ndipo hayati Rais John Magufuli alipoivunja SSRA na kuahirisha matumizi ya kanuni hizo, akitaka zianze kujadiliwa mwaka 2023.

Julai 1, 2022, Serikali ilipeleka suala hilo bungeni, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako alisema kikokotoo kipya kinafanya wafanyakazi wote wa Tanzania wa sekta ya binafsi na umma, kutumia viwango sawa vya ukokotozi wa mafao.

Kanuni hizo zimeendelea kulalamikiwa na wafanyakazi, huku baadhi ya wabunge wakikishikia bango katika mijadala yao.

Chanzo: Mwananchi

Pia Soma:
- Rais Samia, Watumishi Wastaafu wa Jeshi tunaomba utusaidie kupata stahiki zetu, tunateseka
- Kikokotoo kipya cha mafao ni mwiba kwa wastaafu
 
Vijana msitegemee au kungoja hizo hela za pension na kuzipangia bajeti
Ona sasa hawa ndio huwa wanajitia kitanzi
Miaka 33 kazini anawaza pension imtoe
Vijana akiba ya miaka 33 ni hela nyingi unaweza kujiwekea kama una mipango na kuwaza kuwa je nikistaafu nitakuwa na nini?

Mimi msaafu mtarajiwa ila nina savings ziko sehemu 3 na pension 2 shauri zenu mtanikumbuka
 
Mimi msaafu mtarajiwa ila nina savings zako sehemu 3 na pension 2 shauri zenu mtanikumbuka
Ujumbe mzuri huu. Tuzingatie kuwekeza kabla ya kustaafu
 
Vijana msitegemee au kungoja hizo hela za pension na kuzipangia bajeti
Ona sasa hawa ndio huwa wanajitia kitanzi
Miaka 33 kazini anawaza pension imtoe
Vijana akiba ya miaka 33 ni hela nyingi unaweza kujiwekea kama una mipango na kuwaza kuwa je nikistaafu nitakuwa na nini?

Mimi msaafu mtarajiwa ila nina savings zako sehemu 3 na pension 2 shauri zenu mtanikumbuka
Ni rahisi sana kulisemea jambo hasa kama hujui uhalisia wake.
Mkuu,hivi unadhani huyu hakuwa anawekeza??au hana kabisa savings kama wewe??
Unafikiri kama wakiruhusiwa waandamane,waliowekeza na kuweka akiba hawataingia barabarani kwa sababu wana akiba zao???

Embu tafuta mwalimu,mwanajeshi,au afisa mwingine wa serkali aliyefanya kazi miaka 30 tujue mshahara wake wa mwisho,na alicholipwa kama kiinua mgongo,utamuelewa huyu jamaa.

Kujiwekea akiba,kuwa na miradi,sio tiketi ya mtumishi kutapeliwa na serikali aliyoitumikia kwa moyo wote.mbaya zaidi CGP naye anajibu kama kiazi.
Wizara ya MN imejaza mabumunda sana.
 
Mkuu nisamehe bure, sikuwa na maana ya kuwabeza hao watumishi wa serikali, ila system ya serikali kuhusu pension ni mbovu sana na ni laana tu
Unakuta hela zinachukuliwa na kufanyiwa miradi isiyokuwa na tija na je kwanini hela za watumishi zitumike badala ya kuweka na mtu apewe stahiki zake pindi anapohitaji?

Wizi mwingi sana kila sekta na watu ni wapole mno
Naelewa madhila ya wastaafu mkuu ila nilikuwa nashauri tu vijana wajiwekee akiba pia

Sio kwa ubaya wala nia mbaya bali ni ushauri tu
Kama serikali inawafanyia watu kwa hela zao halali je ni ngapi zinapigwa huko
 
Aliyekuwa mtumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania, Salum Shamte (56), amesimulia namna kanuni za kukokotoa mafao (kikokotoo) ilivyosababisha apigwe butwaa baada ya kupokea ujumbe (sms) wa kiasi cha fedha za pensheni ya kustaafu alicholipwa.

Anasema alipokea sms ikionyesha malipo ya Sh21 milioni badala ya Sh55 milioni aliyotarajia baada ya kuitumikia Serikali kwa miaka 33.

Alipotafutwa na Mwananchi, Kamishna Jenerali wa Magereza, Mzee Nyamka amesema utaratibu wa malipo ya pensheni haupo kwa Mkuu wa Magereza, Waziri wa Mambo ya Ndani au Katibu Mkuu.

"Mfuko wa pensheni ya kustaafu unalipwa kulingana na michango aliyotoa na kikokotoo kinazingatia utaratibu huo,” amesema.

"Pensheni halipi CGP, Waziri wa Mambo ya Ndani au Katibu Mkuu, ila inategemeana na michango yake aliyoitoa," amesema.

Salum aliyestaafu akiwa na cheo cha Staff Sajenti Kikosi Maalumu cha Kutuliza Ghasi Magerezani (KMKG), Dar es Salaam, anasema aliposoma ujumbe huo alihisi macho yake yana ukungu kiasi cha kutokusoma vizuri tarakimu.

"Niliomba msaada wa mke wangu anisomee, akanitajia vilevile. Miaka 33 napata Sh21 m

ilioni na kiasi hicho nimekatwa Sh10 milioni, nilikuwa nimekopa Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS Saccos)," anasema Salum.

Mstaafu huyo aliyetembelea ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tabata Relini anasema licha ya kufanya kazi kwa uadilifu, kikokotoo kimeathiri ndoto zake.

Salum anasema alitarajia baada ya kustaafu akanunue maeneo aanzishe shughuli za kilimo.

"Najiona mfungwa mtarajiwa, kwa sababu Sh10 milioni zilizobakia kuna baadhi ya watu niliwakopa muda wote wanazengeazengea nyumbani kwangu wakihitaji niwape chao,” anasema.

"Hata nikitoa hakitatosha, nitaishi katika mazingira magumu. Nashindwa kusimulia, tunafanya kazi katika mazingira magumu ni kama vile Serikali haitambui umuhimu wetu. Kikokotoo sikujua makali yake, sasa najionea," anasema.

Salum anasema mwanzoni wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo alikuwa anaona kawaida lakini ameona ukali wake, hivyo kutoa wito kwa watumishi wengine wasijione wako salama.

"Familia yangu hainielewi inahisi nimekula fedha, lakini hata wale niliowakopa nao hawanielewi, wanasema nina fedha niwalipe chao wakafanye shughuli zao. Ninaishi kama digidigi, muda wote nalala ndani," anasimulia.

Anasema hali ilikuwa ngumu, mke wake na baadhi ya majirani wakamtuliza kwa kumtaka awe na subira.

“Nilipofuatilia kwenye uongozi wa Magereza waliniambia Serikali imeshaamua na sisi hatuna namna nyingine ya kukusaidia, kikubwa ridhika.Kuna wengine walikuwa wananishauri nisubiri tamko la Serikali kusitisha kikokotoo,” anasema.

Anaeleza aliposikia kauli ya Serikali siku ya Mei mosi kupitia kwa Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango haoni mwanga.

Katika Sherehe za Mei mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Arusha, Dk Mpango alisema uamuzi wa kukibadilisha kikokotoo utatokana na tathmini ya kina ya kisayansi ya watakwimu bima.

Salum anasema,“nimeona nipaze sauti yangu kupitia vyombo vya habari ili familia na wale wanaonidai wajue maana kila nikiwaeleza hawanielewi kabisa. Na Serikali ijue shida tunazozipitia, na sisi tuna mahitaji na mipango mingi.”

“Rais inawezekana halifahamu hili kama sisi wastaafu tunapitia shida hizi, atusaidie vinginevyo tutakufa tuna majukumu mazito ikiwamo kusimamia familia,” anasema.

Salum anasema hata wakati wanaanza kutoa elimu ya kikokotoo hicho walielezwa watakatwa kidogo sehemu ya mshahara wao baada ya kustaafu na utakaribiana na waliokuwa wanapokea walipokuwa wakifanya kazi.

Anasema baada ya kustaafu kwa mwezi anapokea Sh290,000 wakati kipindi anafanya kazi mshahara kwa mwezi ulikuwa Sh745,000.

Historia yake
Salum mzaliwa wa Rufiji mkoani Pwani anasena alianza kazi Jeshi la Magereza mwaka 1990 Kiwira mkoani Mbeya akiwa Kuruta.

Anasema alijiunga rasmi na Jeshi hilo mwaka 1991 katika Gereza la Maweni mkoani Tanga.

“Mwaka 1992 nilihamishiwa Gereza la Chumbageni, lakini mwaka 1993 nilirudi tena Maweni, baadaye mwaka 1994 nilihamishiwa Kikosi Maalumu cha Kutuliza Ghasi Magerezani (KMKG), Dar es Salaam,” anasema.

Mwaka 1996 hadi 2006 alihamishiwa Kisongo katika Gereza la Umoja wa Mataifa Arusha walikokuwa waanzilishi kabla ya kuhamishiwa Dar es Salaam kuendelea na kazi KMKG hadi alipostaafu mwaka 2023.

Msimamo wa Serikali
Hoja ya kikokotoo iliibuliwa katika risala ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), iliyosomwa Mei mosi 2024.

Dk Mpango aliyemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan alisema uamuzi wa mabadiliko ya kanuni hiyo, utatokana na tathmini ya kina ya kisayansi ya watakwimu-bima na Serikali inaamini Tucta itawasilisha maoni yake.

“Tunawategemea wataalamu wetu watushauri kuhusu suala hili la uhimilivu na uendelevu wa mifuko ya hifadhi ya jamii, tunawahakikishia wafanyakazi hakuna mtu angependa kuona watu waliotumikia nchi hii wanaathirika kwa kukosa kiinua mgongo stahiki au pensheni zao,” alisema.

Kwa mara kadhaa suala la kikokotoo limekuwa likiibuliwa bungeni na wabunge wakitaka Serikali kufanya marekebisho.

Suala la kikokotoo lilianza kufukuta mwaka 2018 baada ya iliyokuwa Mamlaka ya Kudhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuandaa kanuni mpya zilizolenga kukipunguza kwa watumishi wa umma kutoka asilimia 50 hadi asilimia 33 na kupandisha kutoka asilimia 25 hadi 33 kwa watumishi wa sekta binafsi.

Hatua hiyo ilipigiwa kelele na watumishi wa umma, ndipo hayati Rais John Magufuli alipoivunja SSRA na kuahirisha matumizi ya kanuni hizo, akitaka zianze kujadiliwa mwaka 2023.

Julai 1, 2022, Serikali ilipeleka suala hilo bungeni, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako alisema kikokotoo kipya kinafanya wafanyakazi wote wa Tanzania wa sekta ya binafsi na umma, kutumia viwango sawa vya ukokotozi wa mafao.

Kanuni hizo zimeendelea kulalamikiwa na wafanyakazi, huku baadhi ya wabunge wakikishikia bango katika mijadala yao.

Chanzo: Mwananchi

Pia Soma:
- Rais Samia, Watumishi Wastaafu wa Jeshi tunaomba utusaidie kupata stahiki zetu, tunateseka
- Kikokotoo kipya cha mafao ni mwiba kwa wastaafu
Serikali inabidi kuliangalia hili kwa kina sana

Ililie CCM ,badala ya kumlaumu CGP. Mchawi wetu ni CCM
 
Polisi wastaafu nao wametendwa na kikokotoo lkn wakikumbuka waluvyokua mstari wa mbele kuitetea CCM imebidi wawe wapole.
 
Hii mifuko ya pension ilitakiwa iwe inatumika kuwekeza kama mitaji itengeneze faida ili pesa za hawa pensioners ziongezeke thamani.

Umekatwa labda milioni 100 kwa miaka 33 ikiwekezwa kwa faida inaweza kuwa million 400 au 500.

Sasa milioni 500 wakikupa hata million 400 unakuwa vibaya mzee.

Shida hii inchi inaendeshwa na majitu yenye tamaa na manyakuzi kama mapaka ndio maana pesa haziendi mahala kwenye tija.
 
Vijana msitegemee au kungoja hizo hela za pension na kuzipangia bajeti
Ona sasa hawa ndio huwa wanajitia kitanzi
Miaka 33 kazini anawaza pension imtoe
Vijana akiba ya miaka 33 ni hela nyingi unaweza kujiwekea kama una mipango na kuwaza kuwa je nikistaafu nitakuwa na nini?

Mimi msaafu mtarajiwa ila nina savings ziko sehemu 3 na pension 2 shauri zenu mtanikumbuka
Mm sio mtumishi wa serikali, ila kama una familia inakutegemea, na labda ndugh, kwa mshahara wa 700k utasave nn hapo? Hebu kuwa realistic mzee, haya ni maisha ya watu na viumbe wanaomtegemea
 
Back
Top Bottom