Kikokotoo kilivyomtenda mstaafu Jeshi la Magereza

Huyo jamaa ana madeni , ukweli usemwe huko majeshini hakuna mishahara ya kiivyo wana stress na hasira kinoma ..Wengi wanastaafu na vimeo vya mikopo .

Miaka yote pesa alikuwa anahudumia familia , familia sio mchezo kama una watato zaidi ya watatu jiandae.
 
Mm sio mtumishi wa serikali, ila kama una familia inakutegemea, na labda ndugh, kwa mshahara wa 700k utasave nn hapo? Hebu kuwa realistic mzee, haya ni maisha ya watu na viumbe wanaomtegemea
Familia ndio inaumiza unajikuta pesa yote pata potea , wanaokopa kukimbilia kujenga ni shinikizo la familia.. Ukweli ambao hausemwi usikimbilie familia na kuwa na watoto weng.
 
Familia sio ya kwako iliyotoka kiunoni kwako pekee,kuna watoto wa marehem kaka,dada,mdogo wako,na ndugu wengine,tunajitahidi kuhakikisha nao wanakuwa watu mwisho wa siku,wakati mwingine changamoto ya maradhi kwa mhusika,mwenzi au hata mwanafamilia inamfanya mtumishi huyu kuishi maisha yenye msoto sana na kushindwa kujitetea ktk chnagamoto za kipato hafifu.

Hawa wengine wanaojibu hivi ndio unakuta ni ndugu wa nape,mpwa wa samia,shemeji wa januari,mdogo wa tulia.
Hawajui kabisa aina ya maisha watu wanayolalamikia,wao kwa mwezi kuwekewa milion 2 za matumizi tu ktk acc.
 
😀 😀Wnaume tunaleta familia mazima hatujali kuvaa kwa miaka hata 30 na zaidi ukiwa na nguvu ila huwezi kupata wa kukuthamini , ukute sasa watoto nao hawana kazi mpaka unastaafu uliwekeza pesa kibao.
 
hao umbwa waonege hivyohivyo wanakomaa kula rushwa wakiwa kwenye uniforms zao wakitolewa huko kwenye vikazi vya laki nne nne kwa mwezi wanakuwa wapoleee sasa huyu angekua baunsa wa ukumbi flani wa starehe si angekuwa na afadhali ya maisha kuliko huko kwenye majeshi uchwara, sasa mimi najiuliza vihela kiduchu wanavyopata wanaona ugumu gani kutumia silaha wanazobeba kufanya kweli? daaadekii wanakuja kulalama tu kuomba public sympathy wapigwe tu maana wamejitakia.
 
😀 😀Wnaume tunaleta familia mazima hatujali kuvaa kwa miaka hata 30 na zaidi ukiwa na nguvu ila huwezi kupata wa kukuthamini , ukute sasa watoto nao hawana kazi mpaka unastaafu uliwekeza pesa kibao.
Ukimsilikiza nape au madelu anavyoongea bungeni,unajiskia kuzimia.

Uviccm hawajui hili hustle wao wamekuwa na maisha ya broiler toka wameweza kwenda wenyewe chooni.
 
"Najiona mfungwa mtarajiwa, kwa sababu Sh10 milioni zilizobakia kuna baadhi ya watu niliwakopa muda wote wanazengeazengea nyumbani kwangu wakihitaji niwape chao,” anasema.
Maneno mazito sana hayaaa komandoo mstaafu.....
 

Kusema ni rahisi kuliko matendo, imagine basic salary amesema TZS 745,000 kama sijakosea, hapo take home yaweza kuwa laki 5 na ushee. Hebu tufanye ana familia ya watoto watatu tuu na mkewe tusaidie kuweka matumizi yake kuanzia kodi ya nyumba, chakula, matibabu, elimu, bili mbaliimbali nk ...nina uhakika hiyo pesa hata nusu mwezi haikatizi anaanza madeni dukani, gengeni nk. Si umemsikia hapo kachukua mkopo wa 10M ili akamilishe nyumba yake??
 

Unachosema ni sahihi, hata majuzi bungeni Mhe Easter Bulaya amelizungumza sana hili suala la serikali kwanza inadaiwa fedha nyingi na hii mifuko, lakini pili ni uwekezaji mbaya wa hizi fedha. Ametoa mfano uwekezaji uliofanywa kiwanda cha sukari Mbigiri ambao umeleta hasara tuu.

Tatizo kubwa mimi naona ni wafanyakazi wenyewe kutolivalia njuga suala hili kwa kuliishikia bango mwanzo mwisho, badala yake wamewaachia wanasiasa wawasemee wakati tunajua wanasiasa hawaguswi na hii kitu. Ndiyo maana juzi RC mmoja amesikika akiwakejeli wafanyakazi kwamba eti wanalalamikia kikokototoo wakati anatarajia kustaafu miaka 20 -30 ijayo daah. Ukisubiri mpaka ugongwe na nyoka siku ya kustaafu matokeo yake ndiyo kama huyu komandoo/FFU wa Magereza yaani unalalamika wakati maji tayari yamemwagika.
 
Mkuu inasikitisha sana kwa kweli
Halafu hizo hela unaweza kuambiwa zimepelekwa kufanya hiki huku 75% wameiba wao
Hawa watu hawana uchungu na wananchi ila likija suala la kufyekwa kodi na hela zao za uzeeni wanapiga haswa
Na kweli hawa washamba wanaojifanya tunaandamana nchi nzima mbona hawawatetei hawa wastaafu
Kweli unapewa robo ya hela zako tena huna pa kushtaki
Ila lazima waamke na kudai haki zao ndio maana unaona wengi wanaamua bora akalime au afungue kiduka
 
Familia ndio inaumiza unajikuta pesa yote pata potea , wanaokopa kukimbilia kujenga ni shinikizo la familia.. Ukweli ambao hausemwi usikimbilie familia na kuwa na watoto weng.
Umesema la maana kabisaaàa actually kwa mambo yanayokuja dunian kwa mtu ambaye hana familia na umri mdogo angepause kwanza
 
😂😂😂😂😂 sasa kaka toka tisini mpk 2023 mshahara ni laki7 daah kuna muda unasema umasikini tunautaka sisi kwel miaka 33 unalipwa laki saba aaahah mamaee
Tatizo wabonge salarÿ hiyohiyo ya lak7 ana watoto 3, shule english medium, anahudumia mke, wazaz, wakwe, na ndugu kuna nini tena hapo kama si kuupalilià kuumwagilia na kuuwekea mbolea umaskini
 
Kwa mshahara upi uweke akiba ujenge na usomeshe watoto?
 
Hawa ndo huwa wanawapa kiburi ccm acha wamuonyeshe
 
Issue ni kutoa taarifa kabla na zinazoeleweka ili mtu ajue atapata nini na vipi kuanzia mwanzo na sio kubadilisha badilisha mambo katikati; kuna nchi hazitoi lumpsum lakini kama ulitoa ahadi kwa mtu wakati anaanza kazi atapata kiasi fulani au wenzake walipata kiasi fulani alafu kiasi kikawa pungufu lazima patachimbika..., ila kila siku nasema bora hawa....

 
Imekaa poa hii shida kusikilizwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…