Mimi naona jambo hili lina mitazamo mchanganyiko wa masuala ya kimwili na ya kiroho.
Imekuwa ni mazoea kuona watu wakinywa dawa kwenye kikombe. Sikumbuki siku gani niliona picha ya babu na mtu mmoja mwenye asili ya ki asia. Katika hiyo picha kulikuwa na caption inayosema "Babu akimwombea mgonjwa". Nikajifunza kumbe siyo kikombe peke yake na kuna maombezi pia. Lakini kwa kuwa masuala ya imani ni ya rohoni, dawa na maombezi bado kwangu siwezi kutamka kama ni nguvu ya Mungu ama shetani inatumika. Babu anakiri kwamba Mungu kampa hiyo huduma. Bado kukiri huko kunachukuliwa na mitazamo tofauti kulingana na imani za watu mbali mbali ambao ni Wakristo.
Ndipo utaona watu wengine wanakaa kimya kwa hofu ya kumkosea Mungu. Pengine mim naomba wale waliokwisha kwenda Loliondo, watumegee yanayojili huko kwamba babu anafanya fanya mambo yapi labda.
Kuokotwa kwa kikombe is not an issue kwa Mkristo. Elisha na wanafunzi katika mto Jordan, shoka la kuazima lilipozama, walitumia mti shoka likaelea. Wanafunzi wa Yesu walipokosa hela ya kulipa kodi ya Kaizari, walikwenda kuvua samaki ndani ya tumbo la samaki wakakuta hela wakalipa kodi. Sijui kama fimbo ya Musa alikuwa kaiipata wapi hadi ikatumika katika kufanya maajabu mengi vile. Pengine wajuzi mnisaidie.
Nisiwachoshe. Ninachoona mimi ni vigumu kujudge uwepo wa Mungu katika huduma kwa kuangalia source ya nyenzo inayotumika kwa kuwa Mungu amekuwa akitumia vitu mbali mbali kufanikisha malengo yake na mara nyingi vikiwa vitu na watu dhaifu sana katika macho ya binadamu. Hivyo tuendelee kumwomba Mungu aponye taifa letu.
Kuhusu Babu wa Loliondo, nashauri kwamba tusinajisike kwa jambo hili. Wanaoenda kupata tiba huko, waende kama vile wanavyokwenda ama walivyohangaika kutafuta tiba mahospitalini na wengine kwenye dawa za wachina, wakorea n.k ambazo nazo ni miti shamba. Lakini tuwakumbushe kwamba "Kufa ni mara moja na baada ya kufa ni hukumu hivyo wanapaswa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu hata kama maradhi yote yatatibika".
Nawaomba wahubiri endeleeni kuhubiri habari ya toba, msamaha wa dhambi na ufufuo wa wafu, Yesu Yu karibu.
Sasa hivi nimepata taarifa kua mwingine kaibuka Iringa - Makambako. Yeye anachoma sindano kwa namna ya tofauti na tulivyozoea!.
Tumwacheni babu kama vile tusivyoingilia tiba zinginezo lakini tuhubirini injili ya Yesu Kristo tukijua tutato hesabu zetu mbele za Mungu.
Nawasilisha