kikombe atumiacho babu Alikiokota nyumbani kwake!!!!!!!


Hivi mbeya si yule kijana aliyeoteshwa na marehemu mama yake, ambaye alikuwa ni mganga?

SWALI LA KUJIULIZA KWAMBA HAO WATU WALIOIBUKAA MIKOA MINGINE WALIKUWA WAPI SIKU ZOTE? Kwangu mimi naona ni utapeli ambao unakuja kwa lengo la kutengeneza mazingira yatakayoonyesha hata babu wa loliondo ni tapeli. Japokuwa babu wa loliondo ameanza kutibu agosti mwaka jana, hawa wengine wote wameoteshwa ndani ya wiki 3 zilizopita. Ni vizuri serikali ikawa makini katika kuthibitisha uponaji wa hao wagonjwa wanaopata vikombe ili kupata ukweli.
 
mimi ningekuwa miss judith ningeachana na habari za babu kwasababu kama ambavyo watu hawawezi kunibadilisha imani yangu maana nina msimamo mkali na ninachoamini ni sahihi ndivyo hivyo hivyo ambavyo mimi siwezi kubadilisha imani za watu.

mpendwa, kwa nini tuachane nazo wakati watu wanaangamia kwa kukosa maarifa? huoni kuwa hata wasipobadilika, lakini mbegu ya neno itakuwa imepandwa na inasubiri kuota?

huu sio mchuano kama wa mpira wa ligi ya premier hadi tuache eti kwa kuwa tu hatupati ushindi. sisi ni watenda kazi tu na hatutafuti ushindi wetu wenyewe. ushindi wowote katika hili ni wa Bwana Yesu ambaye ndiye mwenye shamba na mchungaji mwema na mkuu wa kondoo

ubarikiwe sana
 

Kwani babu alikuwa wapi siku zote? Au yeye ndio amekuwa nabii wenu wa mwisho hata muwakane wengine?

Huyo mchungaji wa Mbeya ni mwingine kabisa. Gazeti la majira la leo limeripoti habari zake. Anaitwa mchungaji Kennedy Mwasomola wa kanisa la mitume wapya kusanyiko la Tukuyu mjini. Ameoteshwa na Mungu mti na majani yake yanayotibu magonjwa sugu baada ya kuchemsha na kunywa kikombe. Aliota yuko kwenye foleni ya babu Loliondo. Alipokaribia kufika kupata kikombe akagundua kuwa hana hela (500). Akatoka kwenye foleni na kusimama pembeni. Ndipo akaona umbo mithili ya malaika. Akamponya uvimbe mkononi. Akamchukua mpaka kwenye mti uitwao mpandapanda. Akamwambia, " kwa kuwa wewe ni mwenyeji mwombe mzee mwenye mti huo uitwao mpandapanda ili ukatwe kwa ajili ya dawa." Mzee huyo akakubali kutoa mti bila kinyongo. Ndipo mchungaji akaamka. Akautafuta mti huo na ameshaanza kugawa dozi ya kikombe. Zaidi ya watu 2000 tayari wamekunywa. Anasema ameonyeshwa kuwa ni tawi la babu wa Loliondo.

Mwingine ni John Agunda mkazi wa Ruvu Darajani. Kaoteshwa na malaika. Ameshatoa tiba kwa zaidi ya watu 100. Hatozi hata senti moja. Haulizi mtu anaumwa nini. Ukienda kwa imani tu utapona.
 
Unaweza na ufahamu mkubwa kuhusu biblia,ukaitafsiri kutokana na akili zako,lakini kuna uhitaji wa Roho mtakatifu akuongoze,wako wapi waliojawa na Roho wa Mungu ambao kila siku anawashukia? Watumbie anasemaje kuhusu tiba hiyo,au mengi ya makanisa ya kiroho ni ya uzushi?
 
Huwa sipendi mijadala inayohoji imani ya watu wengine.
 

NAshukuru kwa ufafanuzi
Naona sasa hawa wawili watakuwa wame amua kuondoa swali la kwa nini babu anatoza 500, tuendelee kufuatilia hizi habari, na mimi naamini cha muhimu ni watu kupona, na kutokwenda kinyume na matakwa ya Mungu. Kama ni mtindo mpya wa shetani kuwarubuni watu, sisi tuendelee na maombi, ili shetani ashindwe
 
Kwa wanafunzi makini wa Biblia:
Hu ni mwendelezo wa utimilivu wa kilicho andikwa na Johana, katika
Ufunuo 16:13,14 (13And I saw three unclean spirits like frogs come out of the mouth of the dragon, and out of the mouth of the beast, and out of the mouth of the false prophet.14For they are the spirits of devils, working miracles, which go forth unto the kings of the earth and of the whole world, to gather them to the battle of that great day of God Almighty. ).

Soon mtasikia mtakatifu fulani amefufuka/yupo semu fulani anasema hivi na hivi.
Yesu alisema katika Mathayo 24,' angalieni mtu asiwadanganye' tuwe makini tuchunguze maadiko, otherwise tutakwenda na maji

Ufunuo (14:12) Here is the patience of the saints: here are they that keep the commandments of God, and the faith of Jesus

What is right is not always popular and what's popular is not always right. God is not after the majority, He is after those who diligently seek Him.
 
Nikiwa na mke wa aina ya Miss Judith ni mwanzo wa kukesha bar tu!....
 
Huwa sipendi mijadala inayohoji imani ya watu wengine.

kaka yangu hujitendei haki kwa kuwa na hulka ya namna hii!

imani za watu wengine zinahusu na kuwaathiri watu wengine tena wengi zaidi. kama imani yako haimuathiri mtu mwingine basi labda twaweza kusema tukuache, lakini kwa kuwa nawe tunakupenda, hatutakuacha upotee! sasa angalia imani ya mtu kama babu inazoa maelfu kwa maelfu ya ndugu zetu na kuwapeleka kusikojulikan, kwa nini sisi kama wapendwa wao tusione kuwa tunahusika kuziponya roho zote hizo za wapendwa zinazoangamia kwa kukosa maarifa?

Yesu alisema tupeleke neno lake na tuwafundishe watu kulishika hata miisho ya dunia na ukamilifu wa dahari. na ndio maana tunapeleka. imetupasa kumtii Mungu zaidi ya wanadamu hivyo hatutanyamaza mpendwa

enendeni duniani kote mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu
mkiwafundisha yote niliyowaamuru nilipokuwa ningali pamoja nanyi
na tazama niko pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari
 
How? Anayerudisha sifa ni yule aliyepona, aliyeponywa au wote?

Babu anasema tiba imetoka kwa Mungu na sifa irudi kwake. Yeye hataki chochote kile. Wewe nenda Youtube andika Loliondo Wonders au Maajabu ya Loliondo. Kwenye hiyo video anasema kabisa haya maneno. Sasa watu kama Miss Judith wanakwepa hayo na kuangalia machache. Sijui sasa tuwaonaje.
 


kipi kilianishwa kuwa ni cause of death ya huyo mama?

Lakini hata ivo nina swali hili: wale wote walioponywa kwa miujiza ya Yesu ktk biblia waliishi milele ama hatimae nao walikufa?

Ukijibu hilo utakua ktk nafasi ya kuelewa pia kwa nini mama huyo alifariki
 
Mungu wetu ni mwema, hawezi kufanya maovu kwa binadamu, au kumpa kikombe babu ni uovu?
Kwani kitu gani katika dunia hii Mungu hawezi kufanya. Tusaidie kutafakari vizuri hili

Judy unalo lako jambo

you wanna walk high above God

unazidi mpaka hata chembe ya nia yako njema inapotea




Miss Judith Kwanza nakupa pole kila unacho dadisi kuhusu Babu kila mtu anakupinga na kukuona MJINGA Tuliokunywa tumepona Kama wewe huumwi shida yako nini?


Namuliza Miss Judith kama ana uelewa ni wapi maandiko yanaonyesha kuwa Mungu ni careless? So why does she expect watumishi wawe kuwa careless.

Dada yangu Judith...

Kwa busara za kawaida na hekima ya kiwango cha kati........ hebu soma posts hizi na uzitafakari....Mimi pia sina uhakika wala imani juu ya tiba ya babu, lakini sauti ya watu ni sauti ya Mungu.........kama umeshindwa kabisa kuamini, basi tafadhali nakusihi, kaa kimya kuliko kuwakwaza watu.

What if hii huduma ya babu ikawa ni kweli ina baraka za Mungu, utapata muda wa kutubu dhambi ya kumwekea Mungu mashaka?
 

Miss Juddy..... kuangamia unamaanisha nini? Hao wanaopona wameangamia?

Miss Juddy....kikosa maarifa mana yake nini? Unahisi wewe una maarifa kuliko watu wote wale wanaopiga foleni kwenda kwa babu na hawa unaobishana nao kwa hoja hapa JF?

Miss Juddy.............mshukuru Mungu kwa kuwa una afya njema na wala huna ndugu unayemuuguza kwa magonjwa haya anayoyatibu babu.......tema mate chini yasikutokee kwa sababu utajikuta uko kwenye foleni Loliondo, bila kujua umefikaje pale.....Mungu apitishe mbali.
 
mkuu!! Shetani amepata kuponya! amepata kufufua! amepata kutenda miujiza mingi sana! Tazama wakati wa Mussa na Firauni pata picha...

Well, I guess you are not trying to prove kwamba shetani ana nguvu kushinda Mungu! Labda twende na hypothesis kwamba babu ametumwa na shetani (kama unavyoashiria hapa), je, motive ya huyo shetani kuwaponya (kama kweli wanaponna) ni nini?


Why do we doubt God? Hivi kifo ni kazi ya Mungu ama ya shetani? Kama watu wanakufa in maana Mungu ameshindwa kazi yake au hayupo fair au uwepo wake is simply a myth?

Kwa uzoefuu wangu watu tangia enzi hizo wanakufa, hata sasa wanakufa na wataendelea kufa whether kuna tiba ya ukimwi/kisukari ama la pamoja na kuwepo kwa Mungu kwa kipindi chote hicho. Lakini hili halina maana Mungu hatendi kazi yake.
 
Unataka na yeye aseme AMEOTESHWA NA MUNGU!?

Tumepewa AKILI, ili TUFIKIRI na KUAMUA...

Tumepewa MACHO ili KUONA....

Tumeumbiwa JUA ili LIMULIKE...

Tumepewa MAAMUZI, ili TUCHAGUE...

KUMSHUKURU MUUMBA ama KUMKUFURU.. basi!

Unataka na yeye aseme AMEOTESHWA NA MUNGU! = Kwa nini anadhani yeye (Judith) ni wa kuaminika zaidi kuliko wengine??

Tumepewa AKILI, ili TUFIKIRI na KUAMUA...= Waendao Loliondo wamefikiri na kuamua, shida iko wapii??

Tumepewa MACHO ili KUONA....= Kizuri kwako haimaanishi kitakuwa kizuri kwangu na kinyume chake ni sahihi, ingawa wote tuna macho.

Tumeumbiwa JUA ili LIMULIKE...= Na nyota ziangaze usiku, kwa hiyo hata ktk giza (shida, maradhi, uovu n.k) Mungu hutupa nuru.

Tumepewa MAAMUZI, ili TUCHAGUE...= Iweje mwenzio akiamua wewe uone kakosea wakati power ya maamuzi na kuchagua ni yake na matunda ya maamuzi/uchaguzi iwe mazuri/mabaya ni yake pia??

KUMSHUKURU MUUMBA ama KUMKUFURU...= Angalau mpaka sasa hakuna (kwa walioenda Loliondo) aliyesikika hadharani akimkufuru Mungu
 
Hommie na wewe umeingia kwenye mtego wa huyu Miss? wala usijisumbue kutoa busara zako maana yeye amaeshakiamua kile akitakacho kwa hiyo useme usemavyo hata kusikia kamwe na atandelea kupiga kelele as if yeye ndo nabii wa kweli. lol
 
hahahaha you have nailed it down. Kudos!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…