Kikomo cha amkio la shikamoo

Kikomo cha amkio la shikamoo

Magane

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
202
Reaction score
57
Hivi ni umri gani mtu atakoma kuamkia amkio la shikamoo? Utaona mtu mzima yuko kwenye 50s bado anarusha shikamoo kwa watu ambao kwakeli hapishani sana nao.Au ndiyo hawa wamepewa roho ya ujana hata kama umri wao umeshapita?
 
ukifikisha miaka 70 ndo mwisho wa kusema shikamoo lol
 
Nadhani shikamoo hutolewa kwa mtu aliyekuzidi umri au ndugu yako wa karibu kama vile baba, baba,mjomba au ndugu yako mkubwa..So, haijalishi una umri gani provided hao wapo wewe endelea kuzimwaga tu!
 
kwanza hii salamu ni ya kikoloni,hivyo inapaswa kuachwa. Ilitumiwa enzi za waarabu kumaanisha,"nipo chini ya miguu yako" ni salamu ya kikoloni zaidi.
 
Mwisho ni pale ukikuwa hadi kufikia umri wa kuitwa MAREHEMU!
 
Mimi huwa sitoagi shkamoo kwa mtu ambae sina uhakika na umri wake, especially wanawake.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kwa sababu kila mtu ana mkubwa aliyemzidi umri,hili neno basi halitakuwa na mwisho..
Mwisho ni pale utakapo toka duniani
 
nafikiri hii kitu haina umri....ni mpaka unakufa kama kuna mkubwa zaidi yako lazima umsalimie
 
ukifikisha miaka 70 ndo mwisho wa kusema shikamoo lol

jamani anaweza kuwa na wakubwa na wazazi wake asisalimie kisa 70 au wewe upepata wapi haya ndo uliko mnaishia kuwa na 70 na kufa au
 
Mimi huwa sitoagi shkamoo kwa mtu ambae sina uhakika na umri wake, especially wanawake.

Haahaa mkuu hii ilinikuta nikamsalimia mtu nayemzidi miaka mitano yaani ni mdogo wa rafiki yangu anayemfuata mara 2 that day jamaa kanambia mama yake amekuja so nilipomwona huyu mdada Bongee na uso umemparama nikamwaga shikamoo yangu just to realise later kuwa yule ni mdogo wangu.Ila nilimdai akairudisha.
 
Aisee hata mimi ishanikuta sana hii.....kupima umri wa mwanamke kwa kutizama tu inabidi uwe makini sana! Wengi wanaonekana wakubwa kuliko umri wao halisi!
 
Kwa sisi wachaga shikamoo anapewa mwenye pesa zaidi.
Nasikia kwenu ukiwa na pesa babako anakuwa mdogo na anakuamkia?

Kikweli hii salamu siipendi, nahisi inaudhalilishaji bwana. Nini maana ya shikamoo, haina maana halafu imekaa ki-master and servant. Yaani mdogo tu amsalimu mkubwa, hapa bado sijaona kama kuna kutendeana haki katika kujuliana hali.
 
Shkamoo mwanangu.....dah....
 
Mimi binafsi siipendi kabisa salamu hii. Licha ya kuhusisha udhalilishaji (ubwana na utwana) pia haitoi jibu sahihi kwa hali ya mtu. Mwamkiaji akisema "shikamoo", mwamkiwa hujibu "marahaba". Hata kama anaumwa au ana tatizo lolote la hali au mali, bado atajibu "marahaba". Mwamkiaji hawezi kutoa msaada wowote kwa kuwa salamu aliyoitoa haijampa nafasi ya kupata jibu lenye taarifa kamili kuhusu afya au hali ya mwamkiwa. Vinginevyo utumie muda wa ziada kumhoji mtu kama anakuhusu. Tunaambiwa "Wakati ni mali". Tuko busy kufukuzia shilingi.

Nangojea Tume ya Katiba ikija mtaani kwangu, nitaomba hili liwekwe kwenye Katiba mpya. Shimamoo marufuku.
Msinicheke, hapo ndo ukomo wangu wa kufikiri. Lol!
 
Nasikia kwenu ukiwa na pesa babako anakuwa mdogo na anakuamkia?

Kikweli hii salamu siipendi, nahisi inaudhalilishaji bwana. Nini maana ya shikamoo, haina maana halafu imekaa ki-master and servant. Yaani mdogo tu amsalimu mkubwa, hapa bado sijaona kama kuna kutendeana haki katika kujuliana hali.

Ndiyo maana mimi kwangu awe mkubwa au mdogo huwa nasalimiaga ASSALAM ALEYKUM ikiwa na maana AMANI YA MUNGU/BWANA IWE NAWE
 
ukifikisha miaka 70 ndo mwisho wa kusema shikamoo lol

sina hakika kama ni utaratibu au la, lakini uzoefu wangu unaonyesha kuwa unampa mtu shikamoo yule aliyekuzidi umri. kwa hiyo hata ukiwa na miaka 80 na ukakutana na aliyekuzidi umri bado shikamoo iko pale pale!
 
Back
Top Bottom