Kikosi bora cha timu ya Mpira wa Miguu cha England kuwahi kutokea

Mwaka 96 mmmh,aiseee
Tatizo Jf tumechanganyikana sana,
 
Naamini kikosi bora ni kile kilichobeba kombe la dunia 66..

Kisha kinafata hiki... Wote wacheze ila chapombe gazza alikuwa hatari huyu jamaa...
Namuona mbabe baba mwenye nyumba kitasa mwenyewe tony adams
Golie mzuia magoli david seaman, career yake iliharibika kwa ronadinho 2002
Fundi steven mcmanaman waingereza itawachukua muda kupata fundi kama huyu, ni muingereza lakin anaujua mpira kama muhispain au muitaliano.
Kibabu sheringham
Alan shearer kibabu cha nyavu
Southgate
Mkorofi stuart pearce
Gary neville
 
Gazza alikuwa kituko chapombe yule.
 
Kabla ya fainali hiyo kikosini wingereza aliachwa midfielder mmoja matata sana wa new castle wakuitwa Peter Beardsley Gazza akatoa maoni yake "pamoja na kuwa na kikosi kizuri lakini Peter alitakiwa awemo kuna pasi huwa anatoa Peter karibu na goli nakiri hata mimi siwezi Gazza anasema Peter na Brian Laudrup alie cheza nae rangers ya uskochi ndio wachezaji wawili sio wachoyo duniani Gazza aliwahi kucheza nao "
 
Gazza alikuwa mtu wa vituko sana. Nakumbuka alivyomwaga chozi World cup ya 1990 pale Italy. Moja ya matukio ya kukumbukwa ktk World cup.
 
Mwaka wa 1966 golie Gordon banks huko mbele akisimama bobby Charlton mkungu Bobby moore pana nobby style maneno hayo ila walikuwa na mtu mmoja wa kuitwa Terence paine (terry paine )MBE (member of British empire )ambae sasa ni mchambuzi wa soka supersport wananyanyua kwapa wingereza.
 
bila kumsahau Sir Geoff Hurst, Mchezaji pekee mpaka sasa kufunga hat trick katika fainali ya World Cup.
 
Lakini wachambuzi wengi wa soka wanadai England ya 1966 iliyobeba kombe la dunia katika ardhi ya nyumbani ilibebwa mno mpaka wakachukua ndoo.

Rejea mechi ya Nusu Fainali iliyopangwa ifanyike Goodison Park jijini Liverpool kati ya England Vs Ureno ya Eusebio ilihamishwa masaa 24 ili ipigwe Wembley jijini London, ikawalazimu Ureno wasafiri tena kutoka Liverpool kurudi London na ikawagharimu kwa uchovu wa safari.

Ukija kwenye Fainali yenyewe England Vs Germany, mpaka leo inabaki kuwa mechi yenye utata mkubwa.
Matukio mawili makubwa yalitokea.

Mosi, England walifunga goli ambalo halikuvuka mstari na refa akalikubali na kuwarudisha mchezoni huku matokeo yakiwa ni 2-2.

Pili, kwenye extra time ikafanyika blanda ya karne, refa alikubali goli la England ambalo lilifungwa huku baadhi ya watazamaji wakiwa wameingia ndani ya Uwanja.

England akashinda 4-2 dhidi ya Ujerumani na kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Dunia huku wakitumia vyema usemi wa " Mcheza kwao hutunzwa "

Kutoka Maktaba.
 
Wakiongozwa na foward machachari gary leneka
 
Paragraph yako ya Mwisho kwa kifupi tu, wapenzi wa soka tunaibiwa siku hizi!
 
England ya 90, itabakia kua bora kuliko zote. Ila Nakubali Shearer na Sheringham na Mcmanaman vipaji vao vikubwa.
Sheringham alikua Class ya aina yake very joyful kumtizama. Best England No 10.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…