Ushirombo
JF-Expert Member
- Jan 22, 2013
- 3,558
- 2,702
Mwaka 96 mmmh,aiseeeNilikuwa mtoto tu wakati huo.Niliwapenda sana, kitendo cha Gareth Southgate kupoteza penalty na wao kutolewa kiliniumiza mno. Nakumbuka kabla ya kufikia hatua ya matuta Gazza alikosa goli la wazi. Kwa wakati huo nilikuwa nawafahamu wachache tu kwani ilikuwa ni mashindano yangu ya kwanza ya kimataifa kufuatilia live. Niliokuwa nawafahamu walikuwa David Seaman, Gazza, Shearer, na Southgate (baada ya kukosa penalty). Wengine nimekuja kuwafahamu baadaye baada ya kuwa mfuatiliaji mzuri wa soka. Kwa hapo nawaona Gary Neville, Steve McManaman, David Seaman, Alan Shearer, Gazza, Teddy Sheringham, Tony Adams, Mkorofi Stuart Pearce na Southgate. Nakumbuka kulikuwa nakipa anaitwa Flowers na pia Paul Ince na Fowler. Sijui kama ni kikosi bora zaidi cha England lakini kinanikumbusha mbali kwa kweli!
Tatizo Jf tumechanganyikana sana,