Kwa Manula umekosea sana, huyu ni kipa mbovu sana na stars walimtumia afcon tutafungwa sana
Simba wamejitahidi sana. Kabla ya kufikiria nani atoke na nani asajiliwe kuna mlolongo wa mambo ambayo ni lazima yaangaliwe kwa mapana na marefu yake.
1. Kuuelewa vizuri mfumo wa mashindano haya na uwezo au ubovu wa kweli wa Simba. Hivi Simba, angepata zile pata kosa za Dar, matokeo yangekuwaje Lubumbashi? yangeweza kuwa mazuri zaidi, labda hata kwa penati. Simba iliendelea kufanya vibaya, kwa makosa mbalimbali baada ya Mazembe kusawazisha. Sababu mbalimbali ni kama zifuatazo, kuanzia no. 2,
2. Kuna uchovu wa jumla(general fatigue) kwa wachezaji ajili ya sababu mbali mbali.
a. Umri: Wawa, Erasto, Niyonzima,(coulybali sina uhakika), Kagere, Boko,Okwi. Kati ya hawa namuamini Kagere na Boko kwa kujilinda na kujijali kuhusu changamoto ya umri na wanaonekana kuimudu. Wawa pia anajitahidi ila inaonesha analemewa.
-- Erasto Nyoni kwa heshimna na taadhima; nahisi kidogo anajisahau, siamini kwa uwezo wake wa asili ange perform vile, aidha alikuwa anaumwa au ana mtindo wa maisha usiyo rafiki sana na michezo. Kama sivyo atanisamehe labda game ilimkataa kwani concentration (umakini) wake ulikuwa chini isivyo kawaida yake.
-- Niyonzima ana kipaji kizuri lakini haelekezwi vizuri. Hana nguvu, hivyo hatakiwi ku attempt kumpita mtu zaidi ya mmoja, hata huyo mmoja anatakiwa amuepuke. Location anayokuwepo anafanya moves ambazo being for example the last person, akinyanganywa ni hatari. Amefanya hivo mara nyingi. Kwa kiasi alichangia kuliweka lango la Simba hatarini. Kama ataendelea, awe yeye pekee mwenye shida hii katika kila line up. wengine wenye shida kama hii ni: Okwi na Hassan Dilunga. Penetration Pass ni nzuri sana ziki penetrate. Ikishindikana ni zahama. Hawa watu wanazipenda na zinaleta usumbufu.
Nikichanganya kidogo na Okwi na Boko, kulikuwa na dalili sana za untimely ulalamishi. Ile ulalamishi wa Boko dhidi ya refa haukuwa wa kimkakati. Ule ndiyo wakati Simba ilikuwa moto, badala ya kuwaongoza wachezaji wapate confidence zaidi anaanza kugombana na refa, sielewi faida ya mwenendo ule kwenye mazingira kama yale. Okwi sasa alianza tabia ya kucheza rafu za wazi akishapoteza mpira. Sielewi huo muenendo ameuanza lini.
Wachezaji hawa ni wale ambao wana umri uliosogea kidogo ambapo unaweza sema inabidi watumike kwa maarifa, hasa kwa kutetea ubingwa, wakati mkakati mzuri zaidi wa kuwachanganya na vijana walio tayari, ukifanywa. Hii ni kwa sababu, vijana waliopo Simba kwa sasa hawawezi kutetea ubingwa bila kundi hili. Ili kupata timu nzuri mbeleni, Simba lazima ikombe vijana wengi toka timu nyingine haraka iwezekanavyo la sivyo ijiandae kutumia pesa nyingi kupata wachezaji wa nje.
3. Saikolojia, utanzania na usimba
--- Usajili
Mfumo ambao ni kama professional una changamoto moja kwa Tanzania. Ukiishi Tanzania au ukizijua Simba na Yanga hata kama huishi Tanzania utajikuta umeishaipenda moja wapo. Sasa mchezaji analetwa kucheza professional soccer kwenye moja ya hizi timu aafu anaangukia mapenzi kwenye timu nyingine hususan Simba au Yanga ni Shiida. Huwezi ku predict performance hasa kama mapenzi ya kweli yako upande mwingine. Hii ipo hata kwa wachezaji wa kitanzania. Ni wachache sasa hivi wenye uchungu wa kama kina Haidari;Khalid;Baraza na Kajole kwa mfano kwa Simba au: Kapera;Kilambo;Gobbos; Kitwana kwa Yanga.
Hizi club ziwe na watu ambao ni kama mentors ( washauri au walezi kwa wachezaji) wawasaidie kujitambua kuwa hata kama hakuipenda klabu kabla, wajue namna ya ku perform ili wazisaidie timu na wasurvive.
Hii iwajenge pia wachezaji wa nje. Coulibaly pamoja na kutofanya vizuri juzi, ni mfano wa wafia timu tunaowahitaji.
-- Motisha
Nina mashaka na ukweli kuhusu motisha kwa wachezaji. Simba kwa mfano, sikuona wachezaji wakiwa na raha sana. Hata Okwi baada ya kufunga sikuona ufurahiaji wa pamoja kati ya wachezaji, Nahisi kuna kitu. Juuko alikuwa bench lakini hakuonekana kuelewa sababu ya kwenda bench.
--Team work
Sijui taaluma ya soka lakini naamini kuna kiwango cha pamoja cha ushirikishwaji wa wachezaji kuhusu mfumo unaotumika. Unaona mchezaji anaingia lakini haonyeshi kuelewa ameingizwa kwenda fanya nini! inashangaza.
4. Uchumi
Mfumo wa kampuni
Simba ikiwa katika mfumo wa kampuni, ni vizuri ikawa na kitengo cha utafiti ambacho kitakuja na majibu ya vipengere vya fursa za maendeleo ya mapato endelevu kwani ni wazi kuwa mapato ndiyo nguzo muhimu ya kuwezesha mipango mizuri kufanikiwa. Katika hili ni vizuri ikawekwa wazi na wapenzi wakaelimishwa kuwa ni nini wanaweza kuanza kufanya ili kupata au kushiriki katika asilimia yao 51 ya mali za Simba. Hapa ndiyo moja ya nguzo za maendeleo ya uhakika ya timu, uchumi, hatimaye mchezo. Vinginevyo unasikia mwenzio anasema thamani ya timu yake ni bilioni 200 unaanza kushangaa. Sababu ni kutoelewa vigezo na mipango pamoja na uhalisia wake.
Matayarisho
Pre-season, tuende nchi hizi hizi za Afrika. Lubumbashi; Kinshasa; Ndola; Luanda Morrocco, Tunisia hata Egypt. Hivi nani ametukataza kwenda huko? Hivi tukiomba friend match na Esperance de Tunisia; au na Nkana Rangers as well as Mamelodi watakataa kwa sababu gani?
Tunahitaji kuzoea washangiliaji wa ugenini kwa motisha maalumu. Hivi kuna shida kucheza tena na AS VITA? au Mazembe friend match? tuweke kambi kule tujue siri toka kwenye jamii, kama kweli ni mpira tu au kuna mambo mengine.
Hata hivyo hongera Simba, imeturdisha kama Tanzania tunapostahili na pa kuanzia ni Afcon. Sasa hivi hizi timu zetu kama zina sajili seriously zianzie Afcon, wakishindwa ndiyo washuke huko chini.