Kikosi cha Simba Kifumuliwe

Kikosi cha Simba Kifumuliwe

binafsi napendelea viongozi waangalie zaidi nafasi hizi kwenye usajili

Backline--namba tatu, tano na mbili

Midfild--namba sita na nane

Huko mbele tuwaache kagele, okwi na bocco waendelee.
 
huyo kila Si ndio anaitwa Tanzania One? Ama nimechanganya!
Kwa Manula umekosea sana, huyu ni kipa mbovu sana na stars walimtumia afcon tutafungwa sana
 
Huyu niyonzima pamoja na kwamba ndiyr aliyoasist bao pekee la simba lakini mipira mingi amenyanganywa yeye na mwisho wa siku ikaleta maafa. Yeye amekariri kuwa anacheza na akina mbao na lipuli kila akipata mpira anataka kupiga chenga zake za kizamani za kurudi nyuma, yale majamaa yalishamjulia yanajichukulia mpira kiulaini mguuni mwake.
Kweli Haruna chenga zake na ukizingatia stamina hana... Pamoja na yote wajitahidi ila waongeze kujituma.. Kupambania timu .
 
Mnunueni Jackson Muleka Jana aliwakimbiza wale wazee akina na nyoni pia na kazaliwa nyoni akiwa anacheza mpira 1997. Punguzeni wazee
 
Nakubaliana na ww kutokukubaliana, naomba nisaidie kitu ili utoe solution ya tatizo baada ya hao unaotaka waachwe je ni mchezaji gani wa ndani au nje ya mipaka yetu ungependa asajiliwe??
Japo mm naomba wafuatao waachwe kabisa Gyan, kwasi, mo Ibrahim, Ndemla, mzamiru, Salamba, Okwi ,Wawa.
Halafu atafutwe mbadala wa mkude, mbadadala wa okwi,
Sent using Jamii Forums mobile app
Mzamiru na Okwi wabaki labda kama wanauzwa au kuondoka kwa kunyimwa mkataba.. tofauti na hapo huwezi kupata kiungo wa kibongo mwenye uwezo kama mzamiru kirahisi.
ukumbuke nafasi za wageni ni 10 TU... Okwi labda kama anasepa sio kumkata bado ana uwezo mkubwa.. usimpime kwa game moja wkt amefanya makubwa mechi nyingi.
 
Kwa Manula umekosea sana, huyu ni kipa mbovu sana na stars walimtumia afcon tutafungwa sana
Ubovu wake ameipeleka timu Q'FINAL... Ameipeleka STARZ AFCON.
Punguza unazi Fikiri vzr
 
Mnunueni Jackson Muleka Jana aliwakimbiza wale wazee akina na nyoni pia na kazaliwa nyoni akiwa anacheza mpira 1997. Punguzeni wazee
Kweli..wazee wanakata moto mapema mkuu.
 
Mnunueni Jackson Muleka Jana aliwakimbiza wale wazee akina na nyoni pia na kazaliwa nyoni akiwa anacheza mpira 1997. Punguzeni wazee
Ewaaaaaa,Jackson Muleka [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from Nokia 7 Plus
 
Mnashangaza sana,
Simba inahitaji muda kidogo na uwekezaji makini kuanzia kwenye usajili na benchi la ufundi.
Mtoa mada, nafikiri mihemko na hasira zakufungwa akazihamishia kwa wachezaji directly.

Simba ina wachezaji wazuri, wasio na uzoefu na mashindano ya kimataifa
Kwa sasa tunahitaji top level players walau 6 kikosini kwa ajili ya kuleta ushindani mkubwa kikosini.

Determination ya wachezaji wetu Ni muhimu sana, lazima wafahamu wapo uwanjani kwa sababu zipi na wanafanya nini wawapo uwanjani, hii inahitaji muda kidogo.

Si vyema sana Ku expose mapungufu ya mchezaji mmojammoja na kuwabebesha lawama.
Simba inahitaji nguvu maeneo yafuatayo;
1. Ufungaji, tusajili top players mfano wa Meshaki Elia kijana wa Tp Mazembe,
Au wachezaji wenye kariba ya vilabu tulivyokuwa tukipambana navyo kipindi hiki hasa kuanzia makundi

2. Usajili uzingatie vigezo muhimu katika kuimarisha nafasi muhimu kama
Ulinzi, na kiungo kwa kuzingatia scouting ya maana iliyofanywa kipindi chote.
Huu si wakati wa kujaribu wachezaji

3. Simba imefanya vizuri sana, kuliko matarajio ya wengi, wala hawakuwahi kuwa na ndoto za kutwaa ubingwa wa afrika!
Lakini wamejaribu kupenya mpaka walipofika,
Tutafika, lakini umakini unahitajika sana!

Unaweza kuona Mbwana Samatta alikuwa akishindana na wachezaji wa aina gani pale Mazembe,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina mitizamo tofauti kidogo. Shida kubwa ya Simba ni kiungo mkabaji hususani Kotei asipokuwepo au asipopangwa kucheza nafasi ya ukabaji,mfano mzuri ni mechi ya jana.
Kiukabaji,uwezo wa Mkude ni mdogo mno labda tuwe tunacheza na Lipuli.
 
Wakigeni wa kuachwa.. Juko murshidi..Giani..coulrybali..kwasi..kotei..okwi . wa ndani salamba..mohamedi Ibrahim..ndemla..bukaba,, mlipili..ally saleh...na yule alieingia Jana mwenye mbio nyingi
We hata wachezaji kumbe huwajui, unataka rashid juma aachwe we kweli umepotea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom