Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kikiwa ndani ya ndege maalumu ya kukodi kuelekea nchi ya Cape Verde kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019.
Awali Taifa stars ilikuwa wasafiri na ndege ya Air Tanzania Boeing 787-8 Dreamliner, lakini imeshindikana baada ya kubaini kuwa uwanja wa ndege wa Cape Verde hupokei ndege kubwa kama Dreamliner.
Katika michuano hiyo ya mataifa ya Afrika, Taifa Stars inakwaruza na Cape Verde siku ya Ijumaa Oktoba 12, 2018 na itarudiana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Oktoba 16, siku nne baadaye.
View attachment 892852View attachment 892853View attachment 892854