Kikosi cha wachezaji 25 wa Simba SC kinachosafiri kuelekea Sudan kuwakabili Al Merreikh

Kikosi cha Mabingwa wa Nchi Simba SC kimefika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa ajili ya safari kwenda Khartoum Sudan kupitia Addis Ababa Ethiopia.
 
Hivi wachezaji wale ambao hawapo kwenye benchi siku husika ya match wanakuwaga wapi wakati wa mchezo?
Jukwaani??
Au wanakuwa kambini wakifatilia match kwenye ndani katika mwenye tv?
Wachezaji wanaoanza na wanaokaa kwenye benchi siku ya mchezo wote wanakuwepo uwanjani.

Ama wale wasiokuwepo siku hiyo ya mchezo wanakuwa kambini kwa wenyeji au Hotelini kama timu ikienda ugenini.
 
Naongezea swali pia, hivi jezi wanabadilisha mpya kila mechi? Na baada ya mechi zinaenda wapi?
Jezi zinabadilishwa mpya kila mechi kwa zama hizi tofauti na zamani.

Na jezi akikabidhiwa mchezaji na Manager wa Timu ni mali yake, inakuwa tayari kuitumia na baada ya mchezo ni ruhusa kuihifadhi (kumbukumbu) au kuweza kufanya vinginevyo.
 
Huyo Morrison nini tena mpaka aachwe! Au lile busha limemrudia kwa mara nyingine tena!!
 
Na Mimi naongeza swali!
Baada ya pre match warm ups huwa wanaoga kabla ya kuvaa jersey na kuingia uwanjani?
Na mimi naongezea swali!!
Ikitokea makipa wote wakapewa kadi nyekundu hivi kocha wa makipa anaruhusiwa kuingia kudaka?
 
Yule Chikwende tulimsajili ili acheze na kina Ihefu, Mwadui, Biashara....!
 
Lukosa kaishaambaa,morisson kapigwa pin na caf
 
faida ya game hili naona ipo upande wa simba mpinzani licha ya kwamba yupo kwake ila mpira atacheza kwa pressure kubwa ukizingatia na record ya simba kuto poteza mechi

Record ya simba kuweza kupata matokeo hadi ugenini na kama walifatilia mechi ya al ahly nadhani watakua washakata tamaa kwa kupoteza tumaini
 
Naona kuna watu wanashindana kuuliza maswali
 
Bahat
Bahati mbaya ana leseni....Sijaelewa!
 
Na mimi nauliza swali
Kama refa ni mchezaji kwa nini jezi yake ina mifuko..? Wakati jezi za wachezaji wengine hazina mifuko!!
Sababu refa ni mchezaji asie na mchezaji mpinzani, Wachezaji wengine wote wana wachezaji wapinzani....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…