Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025

Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025

Kikosi kazi cha CCM, Kimekamilisha mapendekezo yake kwa kumshauri Mwenyekiti wao aachane na mambo ya KATIBA kwa sasa.
 
Hiyo 2025 itafika tu. Wasidhani iko mbali sana
 
 
Kwa hiyo Professor Mkandara na wenzake hawaoni umuhimu wa katiba mpya?Sasa usomi wao mbona wanauzalilisha .
 
Nikisikiaga jina na Profesa Mkandala huwa namkumbuka Profesa Bana.😄😄

Hii title ya Uprofesa sijui ina laana gani kwa Watanzania.
 
Hao jamaa na alio watuma kuja na hayo maapendekezo ni wa....

#MaendeleoHayanaChama
 
Mambo ya ajabu kabisa, yaani CCM wanatuamulia sisi watanzania lini watupe katiba na lini wasitupe?
 
Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kilichoundwa na Rais Samia Suluhu leo kinawasilisha taarifa ya yake na mapendezo kwa Rais Ikulu, Dar es Salaam.

Kikosi kazi chini ya mwenyekiti wake, Rewakaza Mkandala kimependekeza Tanzania ianze mchakato wa kupata katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu 2025.
======

Rwekaza Mkandala: Mwisho mheshimiwa Rais ni suala la muda mrefu, mwaka 2011 Tanzania ilianza mchakato wa kutunga katiba mpya kwa kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba namba 83 ya mwaka 2011.

Oktoba 2, 2014 Bunge maalum la katiba lilipiga kura kupitisha katiba inayopendekezwa ambayo ilipaswa kupigiwa kura ya maoni na wananchi ili kuithibitisha lakini mpaka sasa suala hilo halijafanyika.

Changamoto mheshimiwa Rais ni mbili
  1. Kuna wale ambao wanasema hakuna haja kuwa na katiba mpya kwani katiba ya sasa inaweza kufanyiwa marekebisho kukidhi mahitaji ya sasa na baadae.
  2. Mchakato wa kupata katiba pendekezwa haukuwa shirikishi vya kutosha kwasababu baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba walisusia hivyo katiba hiyo kupitishwa na wajumbe waliobaki.
Pia kuna madai mchakato wa kupata katiba mpya haujakamilika, umesimama muda mrefu tangu mwaka 2014 hivyo unapaswa kukwamuliwa.

Pia kuna maoni katiba pendekezwa imeacha mambo ya msingi yaliyomo katika rasimu ya katiba pendekezwa.

Pia kuna suala la katiba mpya kwamba ni muhimu lakini halina haraka kwakuwa katiba ya sasa inafanya kazi vizuri.

Kuna wale wanaosema kuna mahitaji mengi ya wananchi ya maendeleo kuliko uhitaji wa katiba mpya hivyo ni vyema kutumia muda huu kujikita katika kuleta maendeleo ya wananchi.

Mwisho kuna wale wanaodai katiba mpya sio suluhisho ya kila changamoto zinazotukabili, zipo nchi zinazosemekana kuwa na katiba nzuri lakini bado kuna malalamiko kuhusu masuala kadhaa ikiwemo masuala ya uchaguzi.

Hapa suala la kufanyiwa kazi mheshimiwa Rais ni kupendekeza utaratibu wa mchakato wa kutiba mpya na muda wa kufanyiwa kazi.

Kikosi kazi kinapendekeza kwamba Tanzania ianze mchakato wa kupata katiba mpya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Mapendekezo ya namna mbalimbali ya kushughulika na suala la katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu wa 2025

Pendekezo linatokana na sababu kuu nne
  1. Kuna haja ya kuanisha dira kuu ya maendeleo kwa miaka ijayo itakayotoa muelekeo kwa katiba mpya.
  2. Kukosekana kwa muda wa kutosha kuanza kutumia katiba mpya ndani ya kalenda ya uchaguzi wa 2025
  3. Kuna haja ya kutoa fursa kwa marekebisho ya sheria ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa.
  4. Kuna haja ya kutoa fursa ya kutosha kufanyia kazi masuala ya muda wa kati ikiwa ni pamoja na kuanisha dira mpya ya maendeleo.

Kamati hii ipo kuhakikisha Katiba mpya inacheleweshwa hadi baada ya uchaguzi mkuu 2025.

Lengo kuu likiwa kuhakikisha rais mwanamke mzanzibari anaendelea madarakani baada ya 2025.

Bila ya kujizatiti kweli kweli hapa tutagonga mwamba tu.

Umoja wetu ndiyo hivyo tena, mwingine yeyote kwa mtu ni mtuhumiwa wa usaliti isipokuwa yeye.

Kazi kweli kweli.

Cc: Babati
 
Kweli Waaafrika si watu kamili.
Watu watabisha ila huo ndio ukweli.
Kwanini wasiseme tu kuwa katiba mpya sio kitu cha maana au ni kitu cha maana.
Sio mara mchakato ufanyike baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Ni watu kamili labda ungehoji uwezo wa akili na kufikiri.
 
Back
Top Bottom