Lord Delamere in Kenya
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,988
- 8,021
Steve nyerere atakosekana hapo kweli??Mwenyekiti wa kikundi cha wahamasishaji na washangiliaji wa Taifa stars wameomba kuchangiwa na wabunge, wanasiasa na wananchi ili waweze kwenda Cairo, Misri.
Kikundi hicho kina jumla ya vijana 30 wa amsha amsha ambao wote hawana passport hivyo kwa kuanzia wameomba jumla ya sh milioni 5 ili wapatiwe passport. Mwenyekiti amesema RC Makonda amewasaidia kwa kiasi fulani taratibu za pale Uhamiaji na kilichobakia ni malipo tu.
Baada ya hapo bunge linaweza kuwasaidia tiketi za ndege ili wananchi wengine wawachangie gharama za hoteli na usafiri wa ndani wakiwa Cairo.
Mwisho Mwenyekiti wa kikundi hicho amedai hii ni vita kama ile ya Kagera iliyomfurusha nduli Amini hivyo shime wananchi wachangieni vijana hawa 30 wakatutoe kimasomaso.
Source ITV kumekucha michezo
Maendeleo hayana vyama!
Hakosekani mkuu!Steve nyerere atakosekana hapo kweli??
Hiyo ni sawa na omba omba tu ipigwe marufuku mbona omba omba huwa wanaondolewa mitaani sasa hii nchi tunakwamba wapi kila kitu ni michango tu?Aisee kama kuna nchi inaongoza kwa kuchangiana basi ni Tanzania. Ila ni vizuri kusaidiana sisi kwa sisi.
picha???Ujenzi wa reli umefikia 48%!
Lipende taifa lako mkuu...... Zamani Chadema walikuwa wanapitisha kikapu cha sadaka kwenye mikutano yao!Hiyo ni sawa na omba omba tu ipigwe marufuku mbona omba omba huwa wanaondolewa mitaani sasa hii nchi tunakwamba wapi kila kitu ni michango tu?
waache ujinga wanatakiwa washangilaji maarufu kama kibajaji,mlinga,Jah people maana hao kwa kushangilia wanatishaWale akina Ndugai, Ngeleja, Mbowe nk.....wanaenda kutalii tu makoo yamejaa bia watashangilia nini!
kwa jinsi vyuma vilivyokaza hata wakifika fainali ni ngumu kwa wapenzi wa mpira kwenda[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Tufungwe tu, tufungwe kabisa, hadi akili zitukae sawa.....
Taifa Stars ingekuwa timu bora watu wangefurika kwenda kuishangilia kwa moyo mkunjufu kabisa na wala sio mambo ya uhamasishaji na blaa blaa kibao zisizokuwa na mashiko..
Muarobaini katika hili ni kufuma kikosi imara chenye kuleta ushindani, hapo mashabiki watavutiwa na kwenda kuishangilia wenyewe popote itakapoenda kupambana.