Kikundi cha washangiliaji wa Taifa stars chaomba msaada bungeni kipelekwe Misri wenyewe hawana hata senti moja!

Kikundi cha washangiliaji wa Taifa stars chaomba msaada bungeni kipelekwe Misri wenyewe hawana hata senti moja!

Wao si wanavaa mijezi yenye rangi ya CCM?wachangiwe na hao hao wanaowapromote indirectly.😀😂😂.

Kwanza rangi hiyo ni mkosi tupu.Angalia karibu timu zote zinazovaa mijezi yenye rangi hizo zimekuwa zikichakazwa vibaya.Waulize Yanga,waulize Brazil,nk.
 
Mwenyekiti wa kikundi cha wahamasishaji na washangiliaji wa Taifa stars wameomba kuchangiwa na wabunge, wanasiasa na wananchi ili waweze kwenda Cairo, Misri.

Kikundi hicho kina jumla ya vijana 30 wa amsha amsha ambao wote hawana passport hivyo kwa kuanzia wameomba jumla ya sh milioni 5 ili wapatiwe passport. Mwenyekiti amesema RC Makonda amewasaidia kwa kiasi fulani taratibu za pale Uhamiaji na kilichobakia ni malipo tu.
Baada ya hapo bunge linaweza kuwasaidia tiketi za ndege ili wananchi wengine wawachangie gharama za hoteli na usafiri wa ndani wakiwa Cairo.

Mwisho Mwenyekiti wa kikundi hicho amedai hii ni vita kama ile ya Kagera iliyomfurusha nduli Amini hivyo shime wananchi wachangieni vijana hawa 30 wakatutoe kimasomaso.

Source ITV kumekucha michezo

Maendeleo hayana vyama!
Steve nyerere atakosekana hapo kweli??
 
Aisee kama kuna nchi inaongoza kwa kuchangiana basi ni Tanzania. Ila ni vizuri kusaidiana sisi kwa sisi.
Hiyo ni sawa na omba omba tu ipigwe marufuku mbona omba omba huwa wanaondolewa mitaani sasa hii nchi tunakwamba wapi kila kitu ni michango tu?
 
Hiyo ni sawa na omba omba tu ipigwe marufuku mbona omba omba huwa wanaondolewa mitaani sasa hii nchi tunakwamba wapi kila kitu ni michango tu?
Lipende taifa lako mkuu...... Zamani Chadema walikuwa wanapitisha kikapu cha sadaka kwenye mikutano yao!
 
Hivi tutaweza piga vita USHOGA kweli?...vijana wanapenda kutelemka sana...wanapenda sana kulipiwa...kama huna kitu tulia..ukipenda kupokea penda na kutoa pia..shauri yao
 
Kama nawaona hao vijana ambao hawajawahi kupanda ndege.😀😀
Mbona waashangiliaji wengine wao wana vigezo special?😂
 
Yaani nichangie hao vijana wakatalii?? Washangilie kwenye runinga kama wananchi wengine tutakavyokuwa kwenye vibanda umiza.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Tufungwe tu, tufungwe kabisa, hadi akili zitukae sawa.....

Taifa Stars ingekuwa timu bora watu wangefurika kwenda kuishangilia kwa moyo mkunjufu kabisa na wala sio mambo ya uhamasishaji na blaa blaa kibao zisizokuwa na mashiko..

Muarobaini katika hili ni kufuma kikosi imara chenye kuleta ushindani, hapo mashabiki watavutiwa na kwenda kuishangilia wenyewe popote itakapoenda kupambana.
kwa jinsi vyuma vilivyokaza hata wakifika fainali ni ngumu kwa wapenzi wa mpira kwenda
 
Back
Top Bottom