Kikundi kinachochukua hela za bodaboda na kuwakamata chanusurika kichapo Arusha

Kikundi kinachochukua hela za bodaboda na kuwakamata chanusurika kichapo Arusha

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kikundi kinachojulikana kwa jina la Operation, kinachodaiwa kufanya ukamataji wa pikipiki za waendesha bodaboda katikati ya Jiji la Arusha, kimenusurika kushambuliwa na wananchi waliokasirishwa na vitendo vya ukamataji huo.

Tukio hilo limetokea leo katika maeneo ya Kilimanjaro, jijini Arusha, baada ya mmoja wa watu hao, aliyetambulika kwa jina la Omari, akiwa na wenzake kwenda kukamata pikipiki ya kijana mmoja.

Wananchi walipohoji sababu za ukamataji huo, hali ilibadilika na kuwa ya mvutano baada ya Omari kudaiwa kuwa na kisu ambacho kilimjeruhi kijana huyo, hali iliyowapandisha hasira wananchi na kuanza kuwafukuza.

Waendesha bodaboda wanadai kuwa wamekuwa wakikumbwa na ukamataji wa mara kwa mara wa pikipiki zao, huku baadhi ya wanaohusika wakidaiwa kutaka rushwa ya Shilingi 20,000 ili kuachia pikipiki zilizokamatwa.

Wanasema wamechoshwa na vitendo hivyo ambavyo wanadai vimekuwa vikiendelea bila hatua madhubuti kuchukuliwa, huku wakitaka mamlaka husika kuingilia kati na kutoa ufafanuzi kuhusu uhalali wa ukamataji huo.

Soma Pia: Kuna rushwa kubwa na utaratibu usiofuatwa katika ukamataji wa Bajaj na Bodaboda

Hata hivyo, madai kuhusu vitendo vya ukamataji na rushwa yanahitaji uchunguzi na ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika.

 
Rushwa Imeota Mpaka Inalazimishwa Kutolewa Haa
 
Back
Top Bottom