Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

Great thinkers hebu angalieni hiyo post ni ya mwaka gani.Unajua ugonjwa unamuua mbwa haraka,huwa ni wa kushindwa kusikia harufu au kuziba pua.huishia kula sumu.
 
Great thinkers hebu angalieni hiyo post ni ya mwaka gani.Unajua ugonjwa unamuua mbwa haraka,huwa ni wa kushindwa kusikia harufu au kuziba pua.huishia kula sumu.

Suala siyo ya mwaka gani,
Suala ni je, kuna nyumba hata moja iliyorudi baada ya agizo hilo ?
 
Uzuri wa jf. JK ukimuuliza sasa atakwambia sijawai kutamka hayo. Hata zilee ahadi watazikana lakini jf itawaumbua.
 
Hana kumbukumbu alisema mwenyewe dipinti Kile cha campen zake za mwanzo kuwa hata yy amenunua basi hata yy arudishe ili awe mfanow
 
weka current issue,usipotoshe watu as if ni issue ya leo kumbe ni old version.
 
JK arudishe kwanza nyumba aliyonunua ndipo aanze kufikiria kurudisha zilizobaki!
 
Kama habari hii ni ya kweli narudia tena kama habari hii ni ya kweli huu hutakuwa ni uamuzi wa kwanza mzuri kufanywa na JK.

Lakini nani kaandika hii habari?

Wewe ndio mbaya kwa kuona zuri moja. Mbona yapo mengiiii
 
Ukisoma vizuri naona hii ilikuwa taarifa wakati Lowasa akiwa waziri mkuu na mramba waziri wa miundombinu. Imepita miaka mingapi hadi kufikiri uamuzi huu bado utatekelezwa? Hizi ni siasa tu! Labda tusubiri uongozi ujao kunaweza kuwa na mtizamo tofauti.
 
Hatimaye Kikwete Afanya Kweli


  • Aagiza Nyumba za Serikali Zilizouzwa Zirejeshwe

Na Mwandishi Wetu

Rais Jakaya Kikwete ameanza mchakato wa kuhakikisha nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wake wakati wa uongozi wa Awamu ya Tatu, zirejeshwa serikalini.


Habari za uhakika kutoka baadhi ya maofisa waandamizi serikalini zinasema Rais Kikwete ameamua kuzirejesha nyumba hizo katika mikono ya serikali kwa kuzinunua upya kutoka kwa watumishi waliokwisha kuzinunua.


Kwa mujibu wa habari hizo Rais Kikwete ameiamuru Wizara ya Miundombinu kufanya tathmini ya kina ya ununuzi wa nyumba hizo kubaini ni kiasi gani kinastahili kurejeshwa kwa wote walionunua nyumba hizo ili hatimaye zirejeshwe Serikalini.


Inaelezwa ya kuwa kitakachotathmiwa ni kiasi gani cha fedha kilichokwisha lipwa na kila aliyenunua, ikizingatiwa ya kuwa si wote ambao wamekwisha kumaliza kuzilipia nyumba hizo.


Habari ndani ya Wizara ya Miundombinu zinaeleza ya kuwa waliozinunua watatakiwa kuzirejesha na kulipwa kiasi ambacho kila mmoja alikuwa amekwishalipa kwa mujibu ya mikataba waliyopewa.


Inaelezwa kwamba Rais Kikwete ameamua kuzirejesha nyumba hizo Serikalini kwa vile hivi sasa Serikali inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba kwa watumishi wake wanaoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali na wanaohamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


Kwa sababu hiyo serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwapangisha katika hoteli wafanyakazi wengi wapya wanaokosa nyumba katika maeneo wanayopangiwa kufanya kazi, kimesema chanzo chetu cha habari.


Sababu nyingine ni kwamba Serikali imeona kwamba nyumba hizo bado zinatakiwa kuendelea kubakia katika mikono ya serikali kwa sababu ziko katika maeneo yaliyotengwa na maalumu kwa ajili ya viongozi na watumishi wa Serikali.


Chanzo chetu cha habari kilisema kwamba tathmini ya nyumba hizo imeanza kufanywa na Wizara ya Miundombinu ambayo itawasilisha ripoti yake kwa Rais Kikwete kwa ajili ya utekelezaji.


Waziri wa Miundombinu, Basil Mramba hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kwa vile anafuatana na Waziri Mkuu Edward Lowassa katika ziara Mkoani Kigoma.


Naibu Waziri wa Miundombinu Dk Makongoro Mahanga alipoulizwa hakukataa wala kukubali kuhusiana na suala hilo.


Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa nyumba za serikali zilizouzwa nchi nzima tangu mwaka 2002 ni 6,000.


Mauzo ya nyumba hizo yalikuwa yakifanywa kwa awamu na Wakala wa Nyumba za Serikali chini ya Ofisa Mkuu Mtendaji wake, Togolai Kimweri.


Serikali ya awamu ya Tatu ilisema wakati huo ya kuwa fedha zilizopatikana zingetumika kujengea nyumba nyingine kwa ajili ya watumishi wa serikali katika maeneo mbali mbali kama Dar es Salaaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.


Baadhi ya nyumba hizo zimekwisha kujengwa Dar es Salaam kwa ajili ya maofisa waandamazi wa Serikali wakiwamo Mawaziri.


Uchunguzi unaonyesha ya kuwa wakati Kikwete akidhamiria kuzirejesha nyumba hizo Serikalini, baadhi ya watumishi wa Serikali waliozinunua wamezifanyia ukarabati.


Wengine wamejenga nyuma nyingine ndani ya viwanja vya nyumba hizo ambavyo ni vikubwa, yaani ‘low density’


Vivyo vivyo wengine wamepangisha kwa makampuni binafsi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na nyingine zimejengwa maduka ya biashara na ofisi kwenye uzio wa nyumba hizo, hususan zilizopo karibu na barabara.


Uuzaji wa nyumba hizo za Serikali ulioanza mwaka 2002 ulisababisha malumbano na mzozo mkubwa miongoni mwa watanzania, wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, baadhi wakipinga kuuzwa kwake.


Baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya siasa walionyesha masikitiko yao kwa hatua ya kuuzwa nyumba hizo, hasa kwa bei ndogo, wakisema haikulingana na thamani na tathmini ya nyumba na viwanja vya nyumba hizo, kwa pamoja.


Wananchi pia walitaka uwepo uwazi wa majina ya watumishi waliouziwa nyumba hizo na bei waliyonunulia, jambo ambalo Serikali ilikataa kulitekeleza.


Serikali ya Awamu ya Tatu ilisisitiza kuziuza nyumba hizo, ikisema itakuwa ikijenga nyingine kutokana na malipo ya ununuzi wa nyumba hizo.


Miongoni mwa walionunua nyumba hizo ni mawaziri wengi, kama si wote, wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, hasa katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma, kwa kuwa walikuwa wakiishi katika nyumba hizo.


Chanzo: Mtanzania Jumapili Toleo Namba 3784

Waziri Mramba? Halafu Waziri mkuu Lowasa!?!! Kwani habari hii ni ya mwaka gani?
 
Wewe ndio mbaya kwa kuona zuri moja. Mbona yapo mengiiii
chanyera1, hii ahadi aliitoa mwaka 2006 lakini wengine tukasema ni usanii; hivi sasa imepita miaka saba na bado mwaka moja tu Kikwete anaachia madaraka apende asipende, je nyumba zimerudishwa? Sasa hilo zuri moja ni lipi?
 
Kikwete haonagi haibu juu ya ahadi!tokea 2006 mpaka leo
 
Serikali ya Tanzania inaweza fanya chochote vipi imetaifisha majumba itashindwa ku revoke house ownership. Hakuna sheria Tanzania kuna nyumba zimenyanganywa mwenye nyumba kwa manufaa ya umma na serikali ikawamilikisha wapangaji wa hizo nyumba kuna dhuluma nyingi zimefanywa nchi hii.
 
wale waliomalizia malipo yao, wanahaki za nyumba zao lakini wale walio default payments wanyanganywe. Pia Mheshimiwa Raisi, arudishe mgodi wa makaa ya mawe wa mlima wa Kabulu ambao ni sehemu ya Kiwira Coal mine, ambao uliuziwa kinyemela kwa Austrlian majangili ambao toka wapewe coal reserves za Ngaka, hakuna lolote walilofanya.

Kiwira bila Reserves za kabulu hauna mvutio kwa mwekezaji, hilo wanalijua akina Mwakaluka - MD wa Stamico, Maswi. NDC Nao warudishe machimbo ya Ngaka ambao una reserves za makaa ya mawe ambayo yanaweza kuzalisha 900 - 1000 MW ya umeme kwa miaka zaidi ya 50, na ambao umekaliwa na hao specalutaors waki Australia. umeme leo ungekuwa rahisi na tusingekuwa na mgao hata siku moja.

Mheshimiwa Raisi zingatia hili.
 
Zipo zile nyumba akina mkapa ma akina mwapachu wamezinunua huku kikwete akisema zimejengwa kwa lengo la watu wanaotoka nje wakija hawana Sehem za ukisha(wabongo haishi nje) nchi hii duh
 
Back
Top Bottom