Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

TUMETIWA moyo na kauli ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka aliyoitoa bungeni mjini Dodoma mwezi uliopita, kwamba anakusudia kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho Aprili mwaka huu, kulitaka Bunge lipitishe azimio la kurudishwa kwa nyumba za Serikali zilizouzwa na Serikali ya Awamu ya Tatu katika mazingira ya kutatanisha.

Mbunge huyo ambaye amejipambanua kwelikweli kama mmoja wa wabunge ambao wanapambana na vitendo vya ufisadi nchini, alisema hatua hiyo ya Serikali kuuza nyumba za watumishi wake haikubaliki siyo tu kwa sababu siyo endelevu, bali pia ina kila dalili za ukiukwaji wa misingi ya uadilifu na utawala bora.

Tunampongeza mbunge huyo kwa kauli yake hiyo ambayo hapana shaka itakuwa imewaliwaza wananchi wengi ambao walipinga kwa nguvu zote pasipo mafanikio kitendo cha Serikali kuuza nyumba hizo. Itakumbukwa kwamba uuzwaji wa nyumba hizo ulipingwa vikali katika kila kona ya nchi yetu siyo tu kwa kuwa ziliuzwa kwa bei ya kutupwa, bali pia kwa zoezi hilo zima kutofanyika kwa uwazi na kutofuatwa kwa taratibu zilizowekwa kuhusu uuzwaji wa mali za serikali.

Siyo siri kwamba uuzwaji wa nyumba hizo ulionekana dhahiri kufanywa kibabe. Katika macho ya wananchi wengi waliopaza sauti zao kulaani kitendo hicho ambacho bila shaka kilipata baraka za Baraza la Mawaziri, kitendo hicho kilikuwa ni unyang’anyi na ukwapuaji wa wazi wa mali ya umma kinachoweza kufananishwa na uhaini. Tunasema hivyo kwa sababu viongozi wa serikali ambao ndiyo waliokuwa na dhima ya kulinda mali hiyo ya umma ndiyo waliokaa na kula njama za kujigawia nyumba hizo, ambazo zilijengwa sehemu maalumu katika miji yote nchini ili kuwawezesha viongozi wa serikali kuishi karibu na sehemu zao za kazi kwa lengo la kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi zao.

Safu hii haitoshi kuorodhesha madudu yote yaliyotokana na kitendo hicho ambacho kimepewa jina la ufisadi. Hata hivyo, yafaa kusema tu hapa kwamba uuzwaji huo ulifanyika katika staili ya chukua chako mapema na pengine ndiyo sababu nyumba hizo hazikuuzwa kwa viongozi wa serikali pekee kama ilivyotarajiwa, bali pia kwa baadhi ya viongozi wa chama tawala, ndugu, jamaa na marafiki wa viongozi hao.

Hoja ya Mbunge Sendeka ambayo inaungwa mkono na umma wa Watanzania ni kwamba uuzwaji huo haukuwa halali, bali ulikuwa ni wizi. Wananchi wangevumilia wizi huo iwapo angalao ungekuwa umeidhinishwa na Bunge ambalo mamlaka yake yanatokana na wananchi wenyewe. Kitendo cha wateule wachache serikalini kukaa na kula njama za kujigawia nyumba za umma hakika hakielezeki hata kidogo kama ambavyo hakikubaliki kwa namna yoyote ile.

Njama zilizofanywa na viongozi hao ni kukarabati nyumba hizo kwa mamilioni ya fedha za serikali kabla ya kugawiana kama njugu na baadaye kuziuza kwa watu binafsi kwa mabilioni ya fedha. Hata nyumba zilizokuwa nyeti, kwa maana ya kuwa karibu na vituo vya polisi au majengo ya vyombo vya ulinzi na usalama ziliuzwa kiholela. Ebu fikiria hili: Nyumba za mawaziri; makatibu wakuu; wakuu wa mikoa na wilaya; maafisa usalama; makamanda wa polisi wa mikoa na wilaya; mahakimu na majaji; na wakuu wengine muhimu ziliuzwa.

Matokeo ya hatua hiyo ni kwamba viongozi walioteuliwa na serikali ya Awamu ya Nne walijikuta hawana nyumba, hivyo kulazimika kuponda mamilioni ya kodi za wananchi katika mahoteli ya kifahari. Kwa mfano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha aliripotiwa kuishi katika hoteli moja jijini Dar es Salaam na kulipiwa Sh60 milioni kwa mwezi.

Hayo ndiyo matokeo ya uuzwaji wa nyumba za Serikali. Ni matumaini yetu kwamba hoja binafsi ya Mbunge Sendeka itaungwa mkono na Bunge. Ni matumaini yetu pia kwamba Watanzania kwa umoja wao watazidi kupaza sauti kupinga uuzwaji wa nyumba hizo hadi zitakaporudishwa serikalini.

Mwananchi
 
Ni kweli mkuu, naunga mkono hoja! Mie daktari nyumba za nje ya gate la hospitali zilizokuwa za madaktari zikauzwa na sasa wanaishi wafanyabiashara na walioweza kuzinunua, nimeajiriwa nina miaka miwili kazini nimepangisha mtaani mbali kidogo na hospitali nikiwa zamu usiku na kuna emergency hadi nifatwe nyumbani kwani hata pa kupumzika hapo hospitali hakuna, wagonjwa Wengi wamepoteza maisha kusubiri daktari afatwe kwake
 
Wimbo wa Jagular.......kigeugeu......mwenye nao tupia hapa uende sambamba na huu uzi!:target:
 
habari hii ni ya zamani ,waziri wa uchukuzi .basili mramba .lowasa waziri mkuu ,tunataka kuona tangazo la serikali .
 
kama taarifa hii ni ya kweli basi utakuwa ni uamuzi wa kwanza mzuri kufanywa na rais kikwete.
tunaomba urudishwaji wa nyumba hizo usiwe wa upendeleo, tunaomba mawaziri woote walio nunua nyumba hizi wazireje serikalini,
na mfano mzuri uanze kwa kikwete mwenyewe kuirudisha ile nyumba yake.
na zaidi wale waliohusika kuuza nyumba hizi lazima wachukuliwe hatua kali.
tunaomba mheshimiwa raisi usiishie hapo tu endelea kufatilia mambo muhimu yanaonendelea kudhoofisha taifa hili.
watu waache kuleta mchezo na mali za serikali, tunaomba mrudishe nidhamu ya hali ya juu inapokuja kwenye mambo ya serikali na kodi za watanzania.
na hata hapo kwako ikulu matumizi kama hayo ya mkeo kutumia ndege ya serikali kwenda kuhudhulia vituko vya dictator mfalme swazi tunaomba muache,badala yake hizo pesa zitumiwe kwenye kutatua matatizo ya umeme nk.
nawakilisha

Naona mnamsahau JK kwa ahadi nzuri zisizotekelezeka!!!!
 
Hivi hiyo ni akili au matope?Serikali iliuza nyumba kwa watumishi wake,pengine kwa kisingizio kwamba imeshindwa kuziendesha.Leo hii muuzaji anataka kununua alichokiuza kwa madai ya kubadilika kwa mazingira ya wakati mauzo yanafanyika!!!Tanzania haiishi vituko.Kwa taarifa yenu,hata kama zoezi hilo litafanyika (i doubt if it will ever) utafanyika usanii hapo wa watu kujichotea mamilioni ya fedha kama fidia.Huu ni mradi wa kisanii uliobuniwa kuwasaidia vigogo (ambao ndio asilimia kubwa ya wanunuzi wa nyumba hizo) kupata fedha za kulipa madeni waliyotengeneza kwenye kampeni.

Very well said! Hivi kuna mtu anaamini kweli linawezekana?
 
Hadithi za Alfu lela ulela.hadithi hii ilianza 2006 hadi leo 2012 hajaisha? Hii itakuwa imevunja record ya maana ina siku zaidi ya 2000 wakati ile ya alfu lela ulela(siku 1001)ndiyo record ya dunia.
 
Nimeshtuka sana......kumbe nilipata na mtelezo wa macho....sikuona tarehe....
 
Jamani nani kaleta hii hoja ambayo haiwezi kutekelezwa?. Hii ni hoja ambayo hatupaswi kuijadili tukiwa bado tupo katika utawala huu chama cha NYINYIEM. Labda wabadilike
 
Ndo amekumbuka leo,kwani zilipokuwa zinauzwa hakuwa mmojawapo katika baraza la mawaziri?
 
Alikuwa wapi kuzirudisha? Inatakiwa wajiandae kukabidhi nchi kwa amani sasa wanataka kuanza kutekeleza dhamira za CDM waache kutapatapa, ipo kwenye irani ya ccm? Cdm walikuwa na mikakati ya kujenga chuo kikuu Dodoma wakiingia Ikulu, matokeo yake wakakimbilia kutekeleza ilani ya cdm wakati ahadi zao wanazo hazitekelezeki, wasipoteze muda ni mali waanze kujiandaa na kuandaa Police kisakolojia na taasisi nyingine ili watii utawala mpya unaokuja kuwakomboa wa Tz maana Hon. Lema waziri wa mambo ya ndani kunyosha magumashi yao sipati picha Mungu nipe uhai nishuhudie raha duniani. Madaktari na walimu watapata ukombozi wa kudumu. Tunalalia dhahabu, gesi, mafuta, uranium, makaa ya mawe, mlima k'njaro, mbuga za wanjama za ukweli, maliasili mbao, madini ya chuma, tanzanite, ukimuuliza dhaifu kwann nchi masikini hata yeye hajui,unakuta waziri hachaguliwa hata hajui Tz ni muungano wa Tanganyika na Znz tena waziri wa elimu, ajui historia ya darasa la nne. 2015 inachelewa.
 
siasa sa mafumbo kama taarabu ndio anazo weza JK nyumba azitarudi kamwe
 
Yaani walioba wanaambiwa warudishe, nakumbuka wale wababe wa EPA waliambiwa hivi hivi.
 
Huu ni uongo. Hadanganywi mtu hapa...
 
"Tumefika hapa kwa sababu ya serikali DHAIFU ya CCM,wabunge DHAIFU wa CCM na rais DHAIFU wa CCM"

J.J. Mnyika
 
tumoongezee jk muda atekeleze hii ahadi yake
 
Back
Top Bottom