Hoja ya nyumba si ngeni machoni mwa wengi,mengi yamesemwa,wahusuka walikaa kimya kama kawaida yao,na watanzania wajifanya wameyasahau au walikubali yaishe.
Sasa kwakuwa yameanza kusemwa na kigogo ndani ya sisiem,na muhimu zaid ndani ya bunge,nafikiri hii ni hatua muhimu sana.Naamini aneongea ni kimaro kwa sauti,lakini sauti hiyo bila shaka ni kilio cha wengi na inawezekana labda ukombozi unaanza.
Swali je hiyo ngoma wazee huko wabunge wataicheza??,maana sidhani kama kuna kiongozi wa ngazi ya juu ndani ya serikali ya mkapa hakufaidika na ukwapuaji wa nyumba hizi.
Tumsaidie kimaro na wenzake wenye nia safi kama wapo kuendeleza libeneke la kupinga uhujumu wa mali ya walalahoi.