Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

Kama huna hoja bora usiandike. Hata Mzee mwanakijiji anakushinda kwa unaa.

Hivyo, kwa Serikali mbona ni vijisenti tuu. Unaishi karne ipi wewe?
vijisenti?Our govt is broke!....na mabasha zetu wanapunguza misaada
 
Kama huna hoja bora usiandike. Hata Mzee mwanakijiji anakushinda kwa unaa.

Hivyo, kwa Serikali mbona ni vijisenti tuu. Unaishi karne ipi wewe?
Me Nakuita Ndegemshindo Mwenye akili za kufundishwa. iweje useme ni vijisenti wakati kila kukicha serikali inasema haina fedha. Migomo ya wafanyakazi walisema pesa hakuna wanafunzi kama kawaida wimbo ule ule unamzodoa mwenzako wakti wewe ni bure kabisa yaelekea ulikuwepo kwenye maandamano ya kusapoti ufisadi
 
Uamuzi wa mkapa 'ben' kuamua kuuza nyumba za serikali kwa watumishi wa serikali umesababisha hasara kubwa kwa nchii hii .
Miaka 5 ya mwanzo kulikua na mawaziri na manaibu wao pamoja na makatibi wakuu ambao takriban 25 hawakua na makaazi ya serikali hivo walikua wakiishi mahoteli kwa gharama za serikali.
Na sasa kipindi cha pili kuna mawaziri wapya wanakaa hotelini. New africa pekee yake kuna vigogo 10 na familia zao wanaishi katika suites ambapo bila ya chakula bei yake ni usd 300 kwa siku na watoto wao wanakaa room za kawaida . Wengine wana ma body guard wao wanakaa humo kwa gharama za serikali pia.

Wako wengine wanakaa golden tulip , wapo wanaokaa double tree hilton na wengine holiday inn.
Kwa siku gharama kwa walalahoi inawatoka kama usd $ 30,000.00
kwa mwezi kama $ 900,000/ zinatumika sasa fanya kwa mwaka $ 10,800,000/

tunaweza kununua dowans mpya
laiti nyumba zile hazikuuzwa haya yasingekuwepo....usiseme uuzwaji wa nbc, mashirika ya umma na km

Halafu mnasema mnasema nchi yetu masikini. Huyo mwenye jina lenye tafsri ya kilevi si alisema watajenga nyingine? Ziko wapi? Ben Mkapa Oyeee! John Walker Magufuli Oyeeeeeee! Naomba munielewe sina bifu na John. Jamaa anachapa kazi ila huwa napata shida sana na maamuzi yake ya haraka haraka.
 
Kama huna hoja bora usiandike. Hata Mzee mwanakijiji anakushinda kwa unaa.

Hivyo, kwa Serikali mbona ni vijisenti tuu. Unaishi karne ipi wewe?

nilishawahi kuandika .... huyu jamaa sio mtanzania mzalendo ama yu mwenye asili ya taifa lingine aliyejaa chiki na wivu juu ya nchi yetu iliyojaa neema ......kama mmnezoea chuki (martyrdom) huko kwenu basi ujue hakuna mtanzania mwenye roho mbaya kama hii ..... hata mafisadi hawana roho mbaya ila wana tamaa ya fedha na utajiri ..... nimekosa kundi la kukuweka

nahisi kuna satanic influences over your medulla oblongata

God forbid
 
nilishawahi kuandika .... huyu jamaa sio mtanzania mzalendo ama yu mwenye asili ya taifa lingine aliyejaa chiki na wivu juu ya nchi yetu iliyojaa neema ......kama mmnezoea chuki (martyrdom) huko kwenu basi ujue hakuna mtanzania mwenye roho mbaya kama hii ..... hata mafisadi hawana roho mbaya ila wana tamaa ya fedha na utajiri ..... nimekosa kundi la kukuweka

nahisi kuna satanic influences over your medulla oblongata

God forbid
Magufuli na che mkapa wana kesi ya kujibu kwenye hili.
 
Wazo la Kuuzwa Kwa Nyumba za Seikali Ni Sahihi?

Natumia uhuru wa kujieleza nikiwa na swali dhidi ya mkakati au mpango wa kuuza nyumba za Serikali kwa Watumishi wa Serikali ulikua sahihii au la?

Chini ya usimamizi wa Waziri Mh John Pombe Magufuri nyumba hizo mali ya UMMA ziliuzwa na waliofaidika kwa kuuzwa huko ni watumishi wa serikali ambao wengiwao ni viongozi wa Serikali.

HOJA:
Wazo la kuuza nyumba za UMMA ni sahihi, Ndio na Hapana ni majibu yangu kwa vigezo vifuatavyo.

HOJA YA NDIO
1: Kuwainua kiuchumi watendaji au wafanyakazi wa Serikali [Civil Servant empowerment ] waliotumikia nusu ya maisha yao yote kwa kutumikia UMMA.

2: Kutoa nafasi ya Serikali kutekeleza na kuibua mikakati ya ujenzi wa nyumba mpya [MIJI MIPYA] katika maeneo mapya yenye ubora na miundo mbinu mipya na ya kisasa na kuwa mwasisi wa maendeleo ya maeneo au mazingira ambayo hapo awari hayakufikilika kama yangeweza kuwa makazi ya kisasa na bora. Moja ya Sifa kubwa kwa Serikali kuuza Nyumba za UMMA ingekua ni Kuamia makao MAKAO MAPYA DODOMA.[utetezi huo leo hii ungekua halali na mashiko mbele ya UMMA].

Kwa maana nyingine ni serikali kuwa mwasisi wa miji mipya na si kuibuka kwa miji kutokana na mahitaji ya raia.

3: Kuunda ajira kwa jamii kwa misingi ya kuwa mwajiri na mlipaji kwa kipindi chote Serikali inapohusika kujenga makazi ya wafanyakazi wake mapya.

4: Kuondoa fikra ambazo ni hasi [Negative] kama vile kuyaita baadhi ya makazi kwa vigezo vya vipato na hadhi kama Kama Uzunguni, Uhindini, Kwa Vigigo nk. Hili ni la Kisaikolojia zaidi.Kuna watanzania wanaoishi ndani ya nchi hii ni waoga kupita mitaa kama ya Uzunguni [Mfano Oysterbay in Dar es Salaam na Uzunguni Mikoani]. Kwa sababu za kihistoria zaidi,mpaka sasa wanaamini ukikatiza ama kupita mitaa hiyo unaweza kukamatwa ]Mtoe Mkazi wa manzese kamuache Kaunda street Oysterbay uone utakavyo mpa shida, ukiwabahatisha kuwaona wanaopita mitaa hiyo wakienda Coco Beach week end utawahurumia utafikiria wako kwenye maandamano tena yenye nidhamu ya hali ya juu.

5: Kutoa nafasi kwa Serikali kuwa Mwasisi au kinara [Model] wa usanifu wa majengo na ujenzi wa nyumba zenye hadhi ya makazi kwa kuhamasisha [Entice] kupitia nyumba hizo mpya wananchi kuvutika kuiga ujenzi wa mifano na michoro ya nyumba hizo za Serikali.Hivyo kuwa chanzo cha kuondoa ujenzi holela na si tu mgawaji wa viwanja visivyo na mapangilio wa ujenzi miji [Township Plan].

6: Ni mwanzo au sehemu nzuri ya kipimo cha serkali kutathimini maendeleo na makazi ya watanzania wake.Ni sehemu ambapo pia Serikali itaibua na kutekeleza mikakati ya kujenga na kuuza nyumba kwa raia wa kawaida kwenye makazi yake iliyoyabuni mapya. Sio tu raia pia mashirika na makampuni kuwa wapangaji wa Serikali. [Hapa ndipo uwanaumia Serikali inapojitoa hata katika mambo ya Msingi kuwa Serikali haifanyi biashara.].

Ujenzi wa Nyumba za Serikali kwa kuziuza na kupangisha [Real Estate] utaipunguzia nini Serikali? kama si zaidi kuimarisha kwani itakua imewajali wananchi wake kwa kuwajengea nyumba za kisasa na kuwauzia kwa bei za haki na si kama bei za uchakachuaji unaofanya na makampuni binafsi.Hapa ndipo ustawi na maendeleo ya wananchi unapoitaji kupewa kipaumbele.

Chukulia Kijana anamaliza chuo anapata ajira na nakuta Serikali yake imemtayarishia makazi kulingana na mahitaji ya wakati huo [Bachelor Quarters or Single Quarters] na kwa bei sahihi ya serikali,hakika serikali itakua imetoa ukombozi wa maendeleo ya kijana huyu na taifa kwa Ujamla.Baada ya miaka mitatu ya ajira yake kijana huyu anaweza kuanza kulipia nyumba yake ya mkopo kati ya nyumba za makazi mapya hadhi ya familia ambazo serikali imezijenga.

HOJA YA HAPANA

Hoja hii imezingatia kuwa haiukua sahihi kuuza kama Serikali haikuzingatia yafuatayo

1:
Kama Serikali haikujitayarisha na Ujenzi wa Makao Mpya ya Watumishi wa UMMA tena bila mapungufu na katika mazingira au maeneo ambayo imetayarisha miundo mbinu na vitu vyote vya muhimu kuwepo kama Maji, Umeme, Simu, Balabala, Hospitali na huduma zote muhimu kama Mabenki,Maduka, Masoko nk.

2: Kama Mpango wa kuamia Makao Mapya unakinzana na utashi wa baadhi ya watendaji au viongozi. Mfano ilikua sahihi kuuza nyumba za Serikali na Serikali hiyo kuamia Dodoma kwenye MAKAZI MAPYA ILIYOASISI YENYEWE.

3: Kuondoa hoja ya kuwa Serkali haifanyi Biashara hata kama kuna muhimu wa kufanya hivyo kwa faida ya wanachi wake. Biashara maana yake ni kuuza na kununua. Kwa kuuza nyumba hizo tayari Serikali iliingia kwenye Biashara japo kwa msisitizo ilikua inakanusha na kueneza yakuwa inajitoa kwenye kufanya biashara na hivyo kupelekea kuuza mashirika muhimu ambayo ilifikia hatua Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipigia kelele uhuzwaji wa mashirika hayo kama Sigara [TCC] na mabenki.Hivyo kwa kuuza nyumba hizo haikua sahihi kwa kuzingatia Serikali ilikua inajitoa kwenye kufanya Biashara.Na kujitoa kwenye Biashara Serikali ilikua inakosa uhalali wa kuziuza nyumba hizo.
 
Sio sahihi,..kwani ni nyumba za umma..future civil servant waishi wapi sasa.
 
DSN ni kweli umejitahidi kuitetea hoja yako kwa hoja yenye nguvu kwako ila dhaifu sana kwangu!Ni hivi,bora serikali ingebuni namna nzuri ya kuwapati watumishi wake mikopo ya muda mrefu ya ujenzi kuliko ule uuzaji wa nyumba zetu tena kwa bei cheee.Yamkini hujui kuwa kuna baadhi ya vigogo bado wanaishi kwenye hoteli kwa adha ya kukosa nyumba za serikali.WANALIPIWA TSH NGAPI KILA KUKICHA?je zile pesa nadhani zingeweza kusaidia kuboresha huduma muhimu kama vifaa vya shule -madawati,vitabu,maabara,dawa kwenye zahanati,kuboresha miundo mbinu .....nk......au we ndg zako wanaishi masaki na osterbay?Kuijifunza kuplani lazima watu wauziwe? watalaam wengi huenda nchi zilizoendelea kujifunza kwa kuaangalia na kupata uzoefu,hivi kweli wale walioplan maeneo hayo walijifunzia wapi?


kukaa muda mrefu ndani ya maji siyo kutakata
 
tunaangalia nia ya waliofanya uamuzi: wao walijichukulia nyumba zenye viwanja vya thamani kubwa kupunguza kelele wakaachi mahali pengine wachukue watu wadogo2.
 
Uzuri wa hoja yako Mwanajamii ni umeiweka pande mbili!!
Katika namna ambapo kazi za "Shirika la Nyumba la Taifa" limewekwa mochwari kama mashirika mengine, ni vigumu sana " HOJA NDIYO" kama ulivyoziita kukaa katika utekelezaji, ndio watu walipigia sana kelele suala hilo, lakini pia hata kama NHC yetu ingekuwa imara sana bado kungekuwa hamna haja sana ya kuziuza hizo nyumba kwani bado NHC ingeandaa makaazi bora zaidi kwa WATUMISHI WETU WA UMMA baada ya kazi yao nzito ya kujenga taifa, so makazi hayo ya wastaafu bado ingekuwa "uzunguni" nyingine (kwa mikoani) na dar es salaam kungekuwa na "hoysterbay" nyingine nyingi tu.
Huu uuzaji wa hizi nyumba haukuwa na tija kwakweli ni kituko kingine cha hivi viserikali vikwepa majukumu, wameuza hadi nyumba za maofisa wakubwa wa Jeshi la Polisi ambazo zipo karibu kabisa na maeneo yao ya kazi!!
Pia itakuwa poa tukijadili mchango wa NHC kwa mapana yake kuelekea Tanzania tunayoitamani
 
Jamani wana JF na Wa-TZ kwanini tusifungue kesi mahakamani kuwashtaki viongozi wetu walijiuzia majumba ya serikali masaki,osterbay,mikocheni,posta kwa bei rahisi kuanzia mil 3 hadi mil 9,CHADEMA tunaomba muongozo wenu

Shukrani
 
Kwa nini iwe chadema tu, waweza pinga kama mwananchi alie na uchungu na nchi yake sema unahitaji wanasheria kukuongoza.
 
Nyumba za oysterbay zenye viwanja vya ukubwa wa eka 1 zinauzwa kwa wawekezaji kwa bei ya hadi dola milioni 2!
 
Jamani wana JF na Wa-TZ kwanini tusifungue kesi mahakamani kuwashtaki viongozi wetu walijiuzia majumba ya serikali masaki,osterbay,mikocheni,posta kwa bei rahisi kuanzia mil 3 hadi mil 9,CHADEMA tunaomba muongozo wenu

Shukrani

Kwani majaji wao hawakuuziwa? Hiyo kesi itafunguliwa mahakama ipi?

 
Hiv ziliuzwa kipindi cha mkaahapa na mkufuhuli? Kwanin wasiwajibishwe hao watu?
 
Jamani wana JF na Wa-TZ kwanini tusifungue kesi mahakamani kuwashtaki viongozi wetu walijiuzia majumba ya serikali masaki,osterbay,mikocheni,posta kwa bei rahisi kuanzia mil 3 hadi mil 9,CHADEMA tunaomba muongozo wenu

Shukrani

Mkulu shukran kwa kukumbushia miongoni mwa wizi ambao ulifanywa na viongozi wa nchi (ukiachia mbali epa, richmond, deepgreen, n.k). Hili suala halija sahaulika mioyoni mwa wananchi....... bado linazunguka vichwani mwetu...... tusubiri muda.... ukifika kila kilicho cha wananchi kitakuwa mikononi mwao.... nyumba zitarudi tu...... is matter of time....

 
Kweli Tanganyika ni nchi ya vipofu na viziwi! haiwezekani kweli kabisa hao jamaa wafanye mabaya haya yote then jamii imekaa kimya kama imelogwa!
Nani kailoga hii jamii ndugu zanguni? mbona hatuoni wala kuskia haya yanayotokea? Tutasubiri mpaka lini kusema sasa Tumechoka?
Kama vitofali vitano au sita vya dhahabu vina thamani ya 4billion, kweli kimoja kisingeibadili Magu, ujiji, Sengerema na hata Mwadui kuwa mahali bora pakuishi?
Tunamsubiri nani wajameni?
Wameiba kuanzia mbugani,jangwani, mjini na vijijini bado hatushtuki?
Wamepora mali asili, vito vya thamani, wanyama,ndege, miti hata wake zenu, kumbuka kisa cha mwigulu, bado tuu hatuoni wala kuamka?
Kweli Fumbo mfumbie Mjinga........
Magufuli kawaamsha kataka muonyeshe japo hasira na kuamka kidogo still mmelala??
Mungu Futilia mbali hichi kizazi cha waoga na wanafki, walalaji na walalamikaji wakutupwa!!
Wasomi na wajinga wamekuwa wote wavivu wa kuona na kuchukua hatua, Wenyewe kwa wenyewe weusi tumeamua kudhulumiana na kufanyana watumwa!!
Mungu futilia mbali hichi kizazi cha waoga.
 
Walishindwa kuendeleza mipango miji, wakatamani kubaki katika makazi yaliyopangwa na wakoloni, wakapora nyumba za serikali.
Hata mafuriko yaliyotokea yamesababishwa na uzembe na akili zao mbaya zilizojaa tamaa na ubinafsi, kwani hawajali makazi ya raia wengine kwa kuendeleza mipango miji.
Vivyo hivyo msongamano wa magari jijini ni matokeo tabia hizo hizo.
Hata hivyo inawezekana kabisa kuwashughulikia watu hawa, ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia na mawazo kama hayo. Tusipojirekebisha yaweza kutokea wakajiuzia taasisi zote za umma zikiwemo shule, hospitali na hata barabara. (Reli, bandari na viwanja vya ndege walishaanza kuonja).
 
Sendeka akusudia kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge kuitaka serikali irudishe nyumba zote ilizowauziwa watumishi wake na zile walizouziwa ndugu wa vigogo ambao siyo watumishi wa serikali.
 
Back
Top Bottom