Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe


Na ni yupi alie msafi amepata nguvu kama hii ya kuongea haya aliyoyaongea Kimaro??? Hebu mpe sifa yake ili apate nguvu ya kusonga mbele

Viva kimaro!!!
 
Bwana Luyungu nisaidie kidogo mkuu, unajua hii ishu ya ngumba sijaichimbua kiundani, sasa swala ni nyumba za serikali, nyumba za mashirika au zote mkuu???

Naongelea nyumba za serikali ambazo Mkapa na washikaji waliamua kugawana mwisho kabla hawajamaliza kula .
 

Kwa hiyo wewe na akili zako , tena nzuri tu ,unapendekeza vipi kuhusu hizi nyumba? Maana mada hapa ni ya kuhusu hizo nyumba.
Mimi naona aendele sasa kama wewe una issues zake ziweke kunako husika.
 
Hoja ya nyumba si ngeni machoni mwa wengi,mengi yamesemwa,wahusuka walikaa kimya kama kawaida yao,na watanzania wajifanya wameyasahau au walikubali yaishe.

Sasa kwakuwa yameanza kusemwa na kigogo ndani ya sisiem,na muhimu zaid ndani ya bunge,nafikiri hii ni hatua muhimu sana.Naamini aneongea ni kimaro kwa sauti,lakini sauti hiyo bila shaka ni kilio cha wengi na inawezekana labda ukombozi unaanza.

Swali je hiyo ngoma wazee huko wabunge wataicheza??,maana sidhani kama kuna kiongozi wa ngazi ya juu ndani ya serikali ya mkapa hakufaidika na ukwapuaji wa nyumba hizi.

Tumsaidie kimaro na wenzake wenye nia safi kama wapo kuendeleza libeneke la kupinga uhujumu wa mali ya walalahoi.
 


Najua Bubu bado unamategemeo hasa sasa hivi tukielekea kwenye uchaguzi
 
Hii ni dili.

Wapo watakaofaidi kwa kurudishiwa mara 3 au aidi ya pesa walizotumia kununua hizo nyumba.
 
kweli usanii ni kiboko... unaweza kukuta akatoa agizo jipya wakati hili halijatekelezwa

mzee kweli wanamuonea
 
kweli usanii ni kiboko... unaweza kukuta akatoa agizo jipya wakati hili halijatekelezwa

mzee kweli wanamuonea

Mkuu,

Nimecheka sana kuna mtu kwenye post ya Mh. Rita; alisema nanukuu "angekuwa JK angetembea uchi toka chumbani kwake had sebuleni".
Kwa jinsi alivyorudisha fomu kwa mbwembwe vile; na jinsi Caterpillar linamvyomfagilia yeye ndo kwanza anakaza buti asonge...

Na bado tutazisikia zingine nyingi tu mwaka huu!!!! Tehe tehe teheeee....:biggrin1:
 

Hii tu inatosha kumnyima kura mwaka huu. Je, ya kwake atarudisha vipi wakati alikwisha ivunja na kujenga jumba la nguvu pale mtaa wa Ursino? Labda atarudisha ile plot na kilichopo juu yake bila kujali ni mjengo gani!!!
 
Hii tu inatosha kumnyima kura mwaka huu. Je, ya kwake atarudisha vipi wakati alikwisha ivunja na kujenga jumba la nguvu pale mtaa wa Ursino? Labda atarudisha ile plot na kilichopo juu yake bila kujali ni mjengo gani!!!

Hiki ndichi kinachoudhi!!! awa jamaa wametufanya sisi watoto!! Danganya toto!!!
Mi nahisi wakikutana off records, ndo wanachosema!!!

Arrrgg......... :mmph:
 
cha ajabu na zile nyumba ni kuwa mtu unauziwa halafu wewe huyo huyo uliyeuziwa wapewa masharti eti simuuzie mtu sasa mfano umekosa pesa za kusomesha wanao na nyumba title unayo ufanyeje?

Huu ndio udikteta tusipenda wengine
 
Kwa kuwa Magufuli alikuwa Waziri (kabla ya kupata PhD) wakati wa mpango wa kuuziana nyumba za serikali kindugu na kifisadi, na kwa kuwa sasa amerudishwa wizara hiyo hiyo (wakati huu akiwa na PhD), na kwa kuwa anafikiriwa na watu wengi kuwa mwadilifu, ninamuomba amshauri Rais nyumba za serikali zirudishwe.

Akishindwa hilo, basi na ikulu iuzwe kwa mwekezaji; tutajenga nyingine CHADEMA ikiingia madarakani.

Fanya kosa, rekebisha kosa, utaitwa shujaa.
 
..sijui baada ya uteuzi huu Magufuli atakuwa na kisingizio gani cha kutokurudisha serikalini nyumba za serikali alizoziuza kwa bei ya jioni/kutupa.
 
Huyu Magufuli watu wanamfanya mungu au mtakatifu wakati alichemsha wizara ya ujenzi Nyumba ya Masaki market value Tshs. 500m mtu anauziwa Tshs. 3m na kwa mkopo. Watu waache kumsifia bure si ndo huyo huyo alichemka na samaki
 
Kuuzwa hizo nyumba ilikuwa wazo na baraka za Presida wa wakati ule. Kuzirudisha lazima liwe wazo na baraka za Presida wa sasa hivi, JK. Lakini JK ile ya kwake pale Ursino alikwishaivunja na kujenga mjengo wa ki-Saudia baada ya kuongeza kiwanja kwa kumtoa kwa nguvu Mpemba mmoja aliyekuwa jirani yake. Je, watarudisha plots au Nyumba, kwani nyingi kwisha vunjwa na kujenga mi-apartments?
 
magufuli mwenyewe alineemeka kwa ugawaji wa nyumba za serikali. zingine aligawa hata kwa watoto wake wa kambo na wake zake wadogo. wala hii haikua siri baada ya baba wa mke moja mwanafunzi kuja juu kuhusu suala hili.

macinkus
 
Mnanitia machungu mkizungumzia mambo haya, kwani ni huzuni sana kwa nchi hii ukitazama maamuzi yaliyowahi kufanywa na hawa jamaa ambao mumewarudisha wenyewe madarakani ili watumalize kabisa.

Kuchagua ndio kupanga.
 
Izo nyumba ziliuzwa kwa mwongozao wa Ben.
Kumbuka kuwa kama Ben angekataa manake izo nyumba zisingeuzwa,
Ata ingekuwa wewe mkuu wako kaidhinisha uuzwaji wa nyumba lazima nawe ungejimegea tuu tuache unafiki as long as baraka za mkuu zishatolewa
 
Binafsi, kitendo cha huyu Bw. Magufuli kutetea na kusimamia uuzwaji wa nyumba za serikali (whether lilikuwa shinikizo la rais or not) kinanifanya nimchukulie kuwa kiongozi hatari zaidi niliyepata kumfahamu. Kama angekuwa ni mtu safi, asingekubaliana na wazo la kuuza nyumba za serikali. Hivyo, nilitarajia ajiuzulu na kuwaeleza wananchi kuhusu mpango huo hatari usiokuwa na manufaa kwa nchi. Now that he has been given a second chance, let him redeem himself!
 


dONT TELL ME!!!!!!!!!!!!!! Kumbe ukiwa raisi ni kama Mungu, unaweza kumwambia mtu timka akatimka. Taratibu zilifuatwa kweli kumuondoa huyu mpemba mkuu wangu?? Inauma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…