What?. Sasa mbona kipindi chote watu wanaumia na mgao wa umeme wao walikuwa wanavuta miguu tu, kweli bongo tambarare!.
Wana JF naomba kama kuna mtu anayejua ni kiasi gani au wastani wa fedha TANESCO wanazokusanya kwa siku kutokana na mauzo ya umeme basi atufahamishe ndipo tuendelee na mjadala wa matumizi ya fedha yanayolipwa makampuni mbalimbali yanayoiuzia umeme tanesco.
Ninajiquote nilichosema tarehe 15/10/2009
Ninapendekeza;
Mnisamehe kwa kujiquote!
- Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.
- Sikutaka kusema chochote nikiamini kwamba Shirika la TANESCO, Serikali, na kwa upande wa bunge, Kamati ya masuala ya Nishati na Madini, wangeweza kutoa majibu ya tatizo linatukabili. Badala yake, juhudi nyingi zimetumika kutafuta chanzo cha tatizo na kuchelea kutoa suluhuInaumiza sana kuona kuwa tunaendekeza siasa rahisi tunaposhugulikia masuala mazito ya kitaifa kama Nishati. Inasikitisha zaidi pale tunapoona kuwa serikali inashindwa kuchukua hatua mahususi za kuhami uchumi wa Taifa letu. Serikali na Bunge hazitoi suluhisho la hali hii na ni wazi kuna kutupiana mpira wakati nchi inaumia. Serikali imewekwa madarakani ili ifanye maamuzi na tuihukumu kwa maamuzi hayo. Serikali ni lazima sasa iamue.
- Mazingira magumu kama haya yanahitaji maamuzi magumu (extra ordinary circumstances require extra ordinary decisions). Ninaamini serikali itazingatia ushauri wangu.
Ikulu inasema wafanyabiashara ndio wamemwomba Rais. Ni sawa tu........
link yake hii link imetolewa na mkandara kwenye post zake za nyuma
Part D of the Project relating to the IPTL fuel conversion from HFO to gas has not been implemented to date.
However, TANESCO has engaged a consultant-contractor to carry out the engineering and detailed design work for the conversion of the lO x lO MW IPTL power plant to use natural gas from HFO. The engineering detailed design has been completed and successfully
tested for conversion of the Wartsila 38, lOMW units.
A detailed timeline has been drawn up. It is expected that works on conversion will begin when gas is available to allow the converted IPTL plant to operate using natural gas, which is expected after the third and fourth gas processing trains are commissioned at the Songo Songo island and the rental emergency gas fired
power plants are decommissioned at Ubungo. Current projections are that work on conversion would begin in January 2009 and IPTL units would be converted to gas firing in a phased mamier. TANESCO expects to complete the conversion of all units by the end of 2009. This conversion will allow for significant reduction ofenergy charges for the IPlL plant (cost of HFO vs indigenous gas) and after conversion it is expected that the IPlL plant will continue to be dispatched at fairly high load factors. The payback period for this investment, at current HFO prices at 50% load factor, is expected to be less than 1 year..
Kayataka mwenyewe kwa kuunda serikali ya kishikaji, bila kuangalia kama mtu anaweza kumsaidia.Hivi nini maana ya kuwa rais kuwa na wasaidizi????????
Maana kila kitu saa hivi ni JK!
Tumeambiwa kuwa kuendesha mitambo ya IPTL kwa kutumia mafuta ina cost Tshs. 23 Billion kwa mwezi. Jee kuendesha mitambo ya Dowans ambayo inatumia gas ita cost kiasi gani kwa mwezi?
Naomba mwenye takwimu hizi anijulishe ili nijue rationale ya kuwasha mitambo ya IPTL badala ya kuwasha ile ya Dowans na kupata kiasi kile kile cha umeme kwa bei nafuu!!
ZITTO aliongea wakasema ni mambo ambayo hayapelekwi tu kijuujuu, WAFANYABIASHARA!!!! wameongea tu na JK amereact. SO IT MATTERS NI NANI KASEMA!!! Tutafika???
Tumeambiwa kuwa kuendesha mitambo ya IPTL kwa kutumia mafuta ina cost Tshs. 23 Billion kwa mwezi. Jee kuendesha mitambo ya Dowans ambayo inatumia gas ita cost kiasi gani kwa mwezi?
Naomba mwenye takwimu hizi anijulishe ili nijue rationale ya kuwasha mitambo ya IPTL badala ya kuwasha ile ya Dowans na kupata kiasi kile kile cha umeme kwa bei nafuu!!
..kwa bei hiyo kwa miezi minne tuu tunaweza kununua mtambo mpya unaotumia gas kutoka GE or Rolls Royce wa 100MW,viongozi wetu ni hopeless kabisa!
TK naona wewe ni mpiga debe wa DOWANS tokea mwanzo.
Siku mkiwasha hiyo dowans yenu mimi nitatumia solar sitaki kudhalilika
nikiwa hai.
Jamani tusichanganye capital costs na operating costs. Hata ikinunuliwa hiyo mitambo ya gas operating costs zitakuwa pale pale. Hapa la kilinganishwa ni tofauti katika operating costs na ndio maana nikauliza suali na mpaka sasa sijapata mtu wa kunijibu.
...acha spin wewe,wote tumesoma tunaelewa mambo yanavyokwenda na hakuna mtu kasema operating cost zitakuwa zero!