Kikwete aamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja!

Kikwete aamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja!

Wakuu zangu serikali wamesha vuta mkopo wa Bank kuu wa maendeleo ya Umeme na report inaonyesha wazi kwamba mitambo ya IPTL inatakiwa kuwa tayari - converted to gas by December 2009. Haikutokea wala kufanyika lolote, mapesa yameliwa...Sasa mnataka serikali wafanye nini zaidi ya kuwabambikia nyie hizo gharama za IPTL?
Fedha hakuna, zimeshaliwa, alaa sasa bado mnataka nini zaidi!
Je, mnataka serikali ikose misaada mingine kwa sababu hawakufanya walivyoagizwa kufanya kabla hawajavuta mkopo!. Kama hawatawasha mtambo wa IPTL ni lazima wataulizwa maswali mengi sana na hakika Bank na wafadhili watasitisha misaada yao. By all means serikali itawasha mitambo ya IPTL na Dowans, fedha wamesha kula na hakuna mtakalo fanya!
 
Nakumbuka tatizo la mgawo wa umeme lilipotokea mwaka 2006 mhe. Rais J. M. Kikwete pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo walitangazia wananchi kuwa hakutatokea tena kamwe tatizo hilo. Alienda mbali zaidi na kusafiri hadi nchini Marekani akasema kwa kaka yake George W. Bush taarifa ya namna hiyo na kuwahakikishia wawekezaji mbalimbali kutoka Amerika waje kuwekeza maana umeme hautakuwa tatizo tena. Leo baada ya kipindi cha miaka takilibani miwili na kitu, tatizo hilo ndani ya uongozi wake limejitokeza tena kwa makali makubwa hata kuzidi ya kipindi hicho.

Ujumbe wangu ni kwamba, kama watanzania hatutabadilika na kuondokana na kutoa ahadi za maneno pasipo matendo yeyote, basi hata yote yaliyosemwa na serikali hakika hayawezi kufikiwa. Kuna semi mbalimbali kama "maisha bora kwa kila mtanzania, kilimo kwanza na mengine mengi". Hakika kwa mfumo huu uliopo maendeleo yatapatikana wapi. Napenda nikumbushe tu tatizo letu linalotusababisha tubaki hapo tulipo. Ni kuanzia Rais kushuka chini, tumepokonywa utambuzi wa nini tunatakiwa tuviweke kipa umbele kama uwekezaji wa kitaifa wenye manufaa ya kubadilisha maisha ya watanzania kwa muda mrefu (long run basis). Badala yake serikali na watendaji wake kwa shinikizo la "kushinda uchaguzi ujao" wamekuwa wakitupia nguvu ngingi katika kutekeleza Ahadi alizozitoa Mhe, wakati wa kampeni za uchaguzi zenye mtazamo wa makundi na siyo utaifa. Kwa mfano, kama wasukuma aliona hawapendi hiki, basi alisema tutakiondoa hiki na kuwaletea kitu mbadala. Hivi kweli huo ni msimamo anaopaswa kuwa nao mkuu wa nchi??.... Hata kidogo, hapa nayasema haya siyo kwa shinikizo lolote lile tofauti na Utanzania wangu.

Vipa umbele vipo vingi sana ambavyo kwa kipato kidogo cha taifa letu hatuwezi kuyatimiza yote mara moja. Hivyo tunatakiwa tutekeleze yale muhimu (First ranked Priorities) kwa malengo ya kuboresha uchumi wa pato kwa wakati mfupi na mrefu (short-run and long-run). Huwezi ukapata maendeleo ya uchumi wakati ukuaji wa uchumi utokanao wa kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji haufanyiki. Hadi hapo Rais atakapokuwa mwendawazimu wa maamuzi ndipo Tanzania tutaona maisha yetu ya baadaye yana dalili za kustawi. Uwendawazimu ninaousema hapa ni kuachana na mfumo huu uliochafuka kwa makundi yasiyo na uzalendo badala yake unatazama kwa jicho la "sisi na chama chetu" na siyo Watanzania na nchi yetu. Mara nyingi sana serikali hii hii ilishasema haina fedha za kuwekeza kwenye miradi mikubwa lakini utashangaa leo (juma hili), Rais anaamuru serikali igharimie kuwasha mitambo yenye kutumia fedha takiribani shilingi bilioni 23 kwa mwezi (chanzo: Magazeti ya Tanzania Daima na Mwananchi). Hii ni sawa na sh bilioni 276 kwa mwaka. Hivi, Rais angeamuru kujengwa kwa mradi wa umeme utakaogharimu sh. Tirioni 1 na ukatekelezwa kwa miaka minne tangu 2006, tungeshindwa kuutekeleza jamani? Leo wapi hizo fedha zimetoka kama siyo kupitia vyanzo vya kawaida vya mapata ya serikali yetu!

Huwezi ukasema unajenga mazingira ya kukuza uzalishaji nchini ikiwa ni lengo la kukuza ongezeko la uchumi nchini halafu kusiwe na vyanzo vya kuaminika vya umeme. Bila uwendawazi tu hakuna tunachofanya na ni aibu kusema Tanzania tuna nia ya kubadilisha maisha ya wananchi hali hakuna hatua tunazozifanya za makusudi hayo. Kwenye uchaguzi wa 2005 kulingana na vyanzo mbalimbali vya taarifa juu ya CCM ilivyochota fedha zaidi ya Trilioni moja Benki kuu kwa lengo la kununua tisheti, kofia, kanga na takrima kwa wananchi ili wawachague. Hivi uchaguliwa ndiyo imekuwa msukumo wa kuendesha nchi yetu. Hebu tusukumwe na hali mbaya ya maisha ya watanzania hivyo tunagombea ili tuwe na maamuzi ya kiwendawazimu kwa kudhibiti myanya yote inayosababisha pato la taifa lipotee pasipo kuwekeshwa katika miradi ya uzalishaji mali. Tupunguze gharama/matumizi ya kuziendesha serikali zetu.

Hata tukiwa na wataalamu wa uchumi wa kiwango gani kama haya hayatazingatiwa tutaishia tu kuzima moto kila mara kama inavyotokea ukurupukaji katika suala la kutatua mgawo wa umeme unaoendelea kwa sasa. Nani alaumiwe hapa kama siyo serikali iliyokuwa inafahamu hali ya uzalishaji umeme tangu iingie madarakani. Nayasema haya, si kwa wana CCM tu bali ni kwa Watanzania wote, kwamba yeyote anayefikiria kuwatumikia watanzania wa sasa walio ndani ya matatizo mengi likiwepo kubwa la umasikini wa kipato, basi wawe na msukumo wa kuyaondoa haya na siyo vinginevyo. Wawe CHADEMA, NCCR-Mageuzi, CUF, UDP, na vyama vingine, tuache ubabaishaji. Kama Rais alisema tatizo hilo la umeme halitatokea tena asingesubiri hali hii itokee ndipo aanze kutapatapa. Tukichezea muda hakika hatuwezi kuurudisha nyumba ili tuyafanye ambayo hatukuyafanya. Kama 2006 Rais alikuwa na dhamira ya kudhibiti tatizo lisitokee, hatua hiyo ilipaswa ianzie palepale kwa kutumia fedha ili fedha nyingi zije ziokolewe baadaye na kutumiwa kwenye miradi mingine ya kiuchumi.

NB: Naomba wasomaji wa habari hii waniwie radhi pengine lugha yangu si sanifu sana lakini ujumbe ni huo hapo!!!! Asanteni.
 
nchi hii imezidi sasa, yaani hata amri ya MKUBWA WA NCHI aliyoamuru itekelezwe mara moja nayo ni mbinde, mpaka wavvvvuuuuuttttteeeee miguu, kwani huo mtambo wa IPTL upo hapa tz au upo mwezini?? tangu aliposema siku ileeee hadi leo haujawashwa....!
 
Si mnaona sasa; mkuu alihitaji muda wa kupumzika kidogo tu ili akili itulie na kuweza kuangalia matatizo ya wananchi.....
 
Si mnaona sasa; mkuu alihitaji muda wa kupumzika kidogo tu ili akili itulie na kuweza kuangalia matatizo ya wananchi.....

Mwazange,

Una maana tumkwide shingo yake apepesuke na kuishiwa magoti ili akipumzika atafakari kile cha maana na cha umuhimu?
 
Mwazange,

Una maana tumkwide shingo yake apepesuke na kuishiwa magoti ili akipumzika atafakari kile cha maana na cha umuhimu?
U read between the lines....Kama idea hiyo mkuu itasaidia kumuweka muheshimiwa magogoni ili aweze kufikiria matatizo ya wananchi....Then I'm all for it...
 
Wakuu zangu serikali wamesha vuta mkopo wa Bank kuu wa maendeleo ya Umeme na report inaonyesha wazi kwamba mitambo ya IPTL inatakiwa kuwa tayari - converted to gas by December 2009. Haikutokea wala kufanyika lolote, mapesa yameliwa...Sasa mnataka serikali wafanye nini zaidi ya kuwabambikia nyie hizo gharama za IPTL?
Fedha hakuna, zimeshaliwa, alaa sasa bado mnataka nini zaidi!
Je, mnataka serikali ikose misaada mingine kwa sababu hawakufanya walivyoagizwa kufanya kabla hawajavuta mkopo!. Kama hawatawasha mtambo wa IPTL ni lazima wataulizwa maswali mengi sana na hakika Bank na wafadhili watasitisha misaada yao. By all means serikali itawasha mitambo ya IPTL na Dowans, fedha wamesha kula na hakuna mtakalo fanya!
Mkuu Mkandala,so far the episodes are keeping coming out.Huu mgao na bla bla zote was jus a stageshow...http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15535 .Yes by December yote yatakuwa yameishafanyika according to the SCRIPT.
 
Ndugu zangu,

Nimekuta suala hili katika nyaraka zangu nikaseme nishee nanyi. Hili ni moja ya pendekezo la Kamati yangu tulilotoa Bungeni Mwezi Aprili mwaka 2009 na kuazimiwa na Bunge kama Azimio.
...............................
Ugavi wa Umeme wa TANESCO: Kwa kutumia Kanuni 114(17) ya Kanuni za Bunge, Toleo la mwaka 2007, Kamati imeitaka Serikali kuhakikisha Watanzania hawakosi wala hawaingii katika shida ya mgawo wa umeme kwa Mamlaka husika kununua mitambo ya umeme itakayoona inafaa kwa maana ya ubora na uwezo wa mitambo hiyo pasipo kukiuka sheria za nchi – katika kutekeleza hili Serikali ijitahidi kwa uwezo wake wote kuhakikisha kuwa hata huu mgawo unaojirudia mara kwa mara kutokana na kuharibika kwa mashine za SONGAS unakoma mara moja na kuwe na mpango madhubuti wa kuhakikisha kuwa nchi haiingii kwenye giza tena; hali kadhalika Kamati inapendekeza yafuatayo kuhusu Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO): (i) Shirika linapaswa kuongeza juhudi za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kupunguza umeme unaopotea kwa kuwekeza katika kukarabati njia za kusafirisha umeme na juhudi zifanyike ili kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi kwani imeonekana kuwa umeme wake ni rahisi sana – Katika kutekeleza hili Kamati inapenda kurejea ushauri wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Ripoti yake ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2007 kwamba Serikali ipunguze kuingilia utendaji wa TANESCO ili ikitokea suala lolote TANESCO yenyewe iwajibike badala ya sasa ambapo hakuna wa kuiwajibisha kwa sababu ya menejimenti hodhi (micromanagement) ya Serikali kwa shirika hili; (ii) Suala la IPTL limalizwe kwa haraka nje ya mahakama ili kuharakisha ubadilishaji wa mtambo huo ili utumie gesi na hivyo kuongeza uzalishaji wa umeme wa 100MW ambao unatakiwa hivi sasa ambapo kuna nakisi kubwa ya umeme na hivyo kupelekea mgawo ambao unaumiza sana uchumi wa nchi - Katika kutekeleza hili la IPTL lazima izingatiwe kuwa IPTL iliitapeli nchi na TANESCO wamewalipa wamiliki zaidi ya kiasi cha fedha ambacho walipaswa kulipwa na Wanasheria wa TANESCO pia Serikali inatakiwa itumie ushahidi wote uliopo kuhakikisha kuwa kiwango cha fedha kilichopo kwenye akaunti maalumu (escrow account) ndicho hicho hicho kinatumika kumaliza madeni yaliyopo na vilevile kufanyia marekebisho mtambo huo ili utumie gesi bila kuhitajika kwa Serikali kutoa fedha nyingine; (ii) Kufuatia maelezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamati inashauri kuwa mkataba wa SONGAS upitiwe upya ili kupunguza gharama za umeme (capacity charges) kwani ni kubwa mno kuliko kampuni nyingine yeyote inayoiuzia umeme TANESCO na kwa kuwa Serikali kwa kupitia Mashirika yake matatu (TANESCO, TPDC na TDFL) inamiliki asilimia 46 ya hisa za SONGAS, hivyo majadiliano haya yanapata nguvu zaidi – Katika kutekeleza hili iwapo SONGAS haitakubaliana na Serikali katika azma hii ya kupunguza mzigo mzito kwa TANESCO katika gharama za umeme na hasa hasa suala la ‘capacity charges’ na kwa kuwa mkataba kati ya SONGAS na TANESCO unamalizika mwaka 2024, basi Serikali (au TANESCO) inunue hisa zilizobakia (54%) za SONGAS (hostile take over) kwa maana hatua hii ya kununua hisa za SONGAS na hivyo kumiliki mradi mzima ina manuufaa zaidi kwa Taifa kwani nishati ya gesi inakwenda kuwa biashara nzuri sana; (iv) Kutokana na utajiri mkubwa wa nchi katika eneo la nishati na hasa gesi na maporomoko ya maji, Kamati inaitaka Serikali ihakikishe kuwa uwekezaji mkubwa unafanyika katika TANESCO ili iwe kampuni kubwa zaidi ya umeme katika eneo la maziwa makuu – Katika kutekeleza hili TANESCO inapaswa kuendelea kuwa kampuni ya Umma yenye kuongozwa kwa misingi ya Biashara na kwa siku za baadae iwe ni mhimili mkuu wa nchi katika siasa za maziwa makuu (geopolitics) na hivyo kuorodhesha hisa zake katika soko la mitaji la Dar es Salaam, tena kuhusiana na hili ikumbukwe kuwa makampuni ya Umma nchini Afrika Kusini yanaunda 40% ya mtaji (capitalisation) katika soko la mitaji la Johannesburg, hivyo na TANESCO wanapaswa kupewa nguvu ili kutimiza azima hii; hali kadhalika ushauri wa kuunda kampuni mbili za Umma kutoka TANESCO, moja inayohusika na uzalishaji na usambazaji kwa wateja na nyingine usafirishaji (Transmission) unapaswa kufanyiwa kazi kwa maslahi ya nchi.
 
Back
Top Bottom