Kikwete abariki kura ya wazi

Kikwete abariki kura ya wazi

nkomelo

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
216
Reaction score
44
Wadau heshima mbele. Kamati kuu ya ccm imemaliza kikao muda si mrefu usiku huu chini ya uenyekiti wa Dr. Kikwete, ambapo pamoja na mambo mengine mkuu wa kaya amehimiza msimamo wa chama wa matumizi ya Kura ya wazi wakati wote wa maamuzi ya bunge la katiba.
 
Haya mambo ya ajabu sana. Kwani Katiba inayoandaliwa ni ya nchi au ya CCM? Hivi mbona wanakuja na ulaghai wa wabunge wote wanapaswa kuwa wamoja kwa sababu ni suala la kitaifa ilhali CCM wana kundi na misimamo yao? Bado sielewi haya mambo ynavyopelekwa!
 
Safi sana mheshimiwa rais lazima wanafiki wajulikane na wanasiasa muflis wafyekwelewe mbali sioni mantiki ya kura ya siri kwenye maslahi ya kitaifa hapo ndo pa kuwasaga saga wenye ndimi mbili
 
Kamati ya maridhiano ilikuwepo kwenye kikao hicho. JK NI MJUMBE WA Bunge Maalum la katiba mpya? Ni bora wajumbe wote wasiotokana na CCM wakaondoka kwenye Bunge hili wabakie wajumbe wa CCM peke yao na katiba iwe ni ya CCM KULIKO KUBURUZWA NAMNA HIYO
Wadau heshima mbele. Kamati kuu ya ccm imemaliza kikao muda si mrefu usiku huu chini ya uenyekiti wa Dr. Kikwete, ambapo pamoja na mambo mengine mkuu wa kaya amehimiza msimamo wa chama wa matumizi ya Kura ya wazi wakati wote wa maamuzi ya bunge la katiba.
 
Haya mambo ya ajabu sana. Kwani Katiba inayoandaliwa ni ya nchi au ya CCM? Hivi mbona wanakuja na ulaghai wa wabunge wote wanapaswa kuwa wamoja kwa sababu ni suala la kitaifa ilhali CCM wana kundi na misimamo yao? Bado sielewi haya mambo ynavyopelekwa!

Kwani katiba inayoandaliwa ni ya wapinzani!!??, Mbona kila chama kina msimamo Wake, kwanini uone msimamo Wa CCM ndo m'baya!?��
 
Kamati ya maridhiano ilikuwepo kwenye kikao hicho. JK NI MJUMBE WA Bunge Maalum la katiba mpya? Ni bora wajumbe wote wasiotokana na CCM wakaondoka kwenye Bunge hili wabakie wajumbe wa CCM peke yao na katiba iwe ni ya CCM KULIKO KUBURUZWA NAMNA HIYO

Mbona siamini habari hii?
 
hatutaki mambo ya siri sir hapa,tunataka uwazi,anaye taka kufanya siri akafanye chumbani na mkeo
 
Kwani katiba inayoandaliwa ni ya wapinzani!!??, Mbona kila chama kina msimamo Wake, kwanini uone msimamo Wa CCM ndo m'baya!?��

Ndiyo maana tunataka maamuzi ya upatikanaji wa KATIBA MPYA uandaliwe na hili BUNGE maalumu la katiba, na siyo kundi lolote. Hivyo ni vema vyama ama makundi yoyote yasishinikize misimamo yao, ni vizuri wakubaliane kwa hoja za msingi katika mambo yote.
 
Kura iwe uamuzi kama umeamua kupiga kura ya siri ni juu ya mjumbe na sio wanasiasa kuamua. Kura ni haki ya mjumbe na sio haki ya kichama! wajumbe wanawawakilisha wananchi na sio chama . Chama ni chambo cha sera tu lakini uamuzi ni wa wananchi unao wawakilisha. Kama mjumbe anapiga kura kwa maelekezo ya Nape nchi imekwisha!!. Kikwete anafanya makosa ya kuwa na vikao vya Chama kila siku wakati wa mchakato wa katiba ni lazima ieleweke katiba ikitoka na kuonekana ya kulazimishwa italeta matatizo kuliko hata tulivyo sasa huwezi kulazimisha wananchi kwa dunia ya siku hizi. Huwezi kulazimisha mfumo wa serikali kama wananchi hawataki maana yake utakuwa na serikali inayoogopa wananchi badala ya serikali ya wananchi!
 
Kwa mtindo huo wa kura za wazi watu wataogopa kuonyesha msimamo wao na hivi watapiga kura kui-support CCM kwa kuwa wataogopa kung'olewa kucha na meno bila ganzi.
 
Ma ccm ni mijitu ya ajabu sana. wanachi watakataa katiba ya chama cha majambazi.
 
Haya mambo ya ajabu sana. Kwani Katiba inayoandaliwa ni ya nchi au ya CCM? Hivi mbona wanakuja na ulaghai wa wabunge wote wanapaswa kuwa wamoja kwa sababu ni suala la kitaifa ilhali CCM wana kundi na misimamo yao? Bado sielewi haya mambo ynavyopelekwa!

Mkuu hadi leo hujui unafiki wa ccm? Hawa jamaa mm huamini kama wametoa tangazo la kifo cha kiongozi mwenzao, maana najua hawawezi danganya kifo cha mwenzao lakini mambo mengine ucje poteza muda wako kuwaamini
 
Back
Top Bottom