Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

wameendekeza wizi...kitendo cha kuwa wazazi wao walikaa sirikalini miaka mingi wakafa maskini wao wamekiona ni upumbavu kwa hiyo wakaamua kuiba mchana kweupe na wengine wakawa wanakula bila hata kunawa mfano Maige na Ngeleja.

walitakiwa badili ya kuiba watengeneze social security sytem nzuri ambayo itamfaa kila atakayefanya kazi mpaka kustaafu ili asishawishike kufanya wizi, wao wakafanya kinyume yaani CHUKUA CHAKO MAPEMA(CCM).

na katika michakato hiyo wakasahau kuwa...what goes around, comes around.
 
JK anadai hakuwa mnyenyekevu kwa chama cha magamba (CCM) licha ya kuuhadaa umma siku ya mei mosi kuwa alifurahishwa na mjadala bungeni uliopelekea kubadilisha baraza lake la mawaziri. Huu ndio unafiki wa ccm na viongozi wake. Hawako wakweli kabisa.
 
Tunaemjua kigwangala tumetulia toka awe kiongozi pale MUCHS,toka akiwa mwanafunzi hatabiriki ktk kugeuka, si wa kumwamini kwamgu namchukulia ni mtafutaji wa fursa zaidi kuliko mpiganaji, pole sanaaa, usijali ukikomaa kisiasa na kuwa na msimamo wa kueleweka utakuja kuingia ofisini.
 
Mbona bado wapo mkuu, January makamba, Emmanuel Nchimbi, Adam Malima, Lazaro Nyalandu,......

Malima ni mwizi sema bado hajajulikana.Makamba ni mnafiki nae ni mwizi mjanja tu,period.Lazaro nae hayuko safi.Mkuu,hawa ni wenye nafuu tu.

Mimi hoja ya kuwa na raisi kijana kama kina makamba sikubaliani nayo kwa sababu ya mambo haya tu.Vijana wana expectations nyingi,kwa hio ni rahisi kuiba
 
Kuondolewa kwa mawaziri vijana kwenye baraza la mawaziri ni changamoto kubwa na inaleta maswali mengi. Je ni kukosa viongozi vijana walio tayari kwa madaraka hayo?

mbona kuna wengine wameletwa???

Pia vijana wengi makini hawawezi kukubali kuwa kenye mfumo tulionao sasa wa kisiasa, kwani uko corrupt sana.... na mtu makini hawezi kuingia kwenye platform ya siasa ya sasa............. ni bora kufanya mambo mengine
 
Ofisi yake ipo wapi huyo Waziri Asiye Na Wizara(WANW)?

Waziri ofisi ya rais asiye na wizara maalumu. Kwanza atakuwa karibu na rais pili atakuwa na uwezo wa kuingia wizara nyingine kwa maana nyingine ni kama kiranja wa mawaziri nyuma ya PM.

Mawaziri waliowahi kuwa wizara hiyo ni Kingunge na marehemu Rashid Mfaume Kawawa
 
[h=3][/h]

Kwa waliosikia au kusoma orodha ya baraza la mawaziri tuliloahidiwa kuwa lingesukwa upya na kuja na mapya watakuwa wamepigwa na butwaa juu ya kiburi na ugumu wa rais Jakaya Kikwete kujifunza. Kimsingi alichofanya Kikwete ni kile watoto wa mjini huita changa la macho. Kwa blogu hii kilichofanyika ni usanii na dhihaka kwa watanzania. Tuna sababu za kusema hivyo;
Mosi, zimerudishwa sura zile zile hata ambazo zina madhambi ya wazi wazi na ya muda mrefu.
Kwa mfano unategemea jipya gani kutoka kwa watu kama Stephen Wassira, Jumanne Maghembe, Matayo Matayo, Mathias Chikawe, Celina Kombani, Sofia Simba, Adam Malima na wengine wengi.
Pili hatukuamini kama rais angewarejesha watuhumiwa wa kughushi ambao wanajulikana kuwa ni Makongoro Mahanga, Mary Nagu na Wiliam Lukuvi.
Tatu, rais amelazimika na kupoteza imani na muda wetu bure. Tulitegemea mapya lakini ameturejeshea mvinyo ule ule kwenye chupa ile ile. Hivi rais wetu atajifunza lini wakati muda ukizidi kuyoyoma? Je wabunge waliotunisha misuli na kuondoa baadhi ya mawaziri wataridhika na dhihaka hii? Kwanini rais hakufanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri badala ya kutupotezea muda na kutuweka kwenye sintofahamu kwa muda mrefu. Hakika kilichofanyika licha ya kuwa dhihaka na usanii, ni taarifa kuwa Tanzania itazidi kuendelea kuelekea kuzimu.
Tumewahi kusema kuwa serikali ya Kikwete ni ya ubia na kuna watu wenye shares nyingi. Nao ni hao ambao hawagusiki bali huwa recycled kila mara.
Mfano mdogo ni kwamba kwa mazabe na madudu aliyotenda mtu kama Adam Malima, kama siyo kulindana kwa misingi yoyote iwayo hakupaswa kurejeshwa au tuseme kuwa recycled.
Hakika hili si baraza jipya la mawaziri bali baraza kuukuu na la kishikaji na Jakaya Kikwete. Kweli Tanzania tunayo safari ndefu.
 
[h=3][/h]

Kwa

waliosikia au kusoma orodha ya baraza la mawaziri tuliloahidiwa kuwa
lingesukwa upya na kuja na mapya watakuwa wamepigwa na butwaa juu ya
kiburi na ugumu wa rais Jakaya Kikwete kujifunza. Kimsingi alichofanya
Kikwete ni kile watoto wa mjini huita changa la macho. Kwa blogu hii
kilichofanyika ni usanii na dhihaka kwa watanzania.
.

sijui jk angefanya nini ili amridhishe kila mtu. kwa dunia hii hilo haliwezekani!
 
MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3. OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi

Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira

Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji

Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum

Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Eng. Christopher Chiza, Mb.,

Waziri wa Uchukuzi

Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara

Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha

Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini

Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

5. NAIBU MAWAZIRI

OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI

6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

7. OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8. WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,

Wataapishwa Jumatatu tarehe 8 Mei, 2012 saa 5.00 asubuhi katika viwanja vya Ikulu
 
mbona wote umeandika mbunge?
kuna wengine hawajaapishwa na spika kuwa wabunge,naombeni msaada kama hii kitu imekaa vizuri.
 
[h=3][/h]

Kwa waliosikia au kusoma orodha ya baraza la mawaziri tuliloahidiwa kuwa lingesukwa upya na kuja na mapya watakuwa wamepigwa na butwaa juu ya kiburi na ugumu wa rais Jakaya Kikwete kujifunza. Kimsingi alichofanya Kikwete ni kile watoto wa mjini huita changa la macho. Kwa blogu hii kilichofanyika ni usanii na dhihaka kwa watanzania. Tuna sababu za kusema hivyo;
Mosi, zimerudishwa sura zile zile hata ambazo zina madhambi ya wazi wazi na ya muda mrefu.
Kwa mfano unategemea jipya gani kutoka kwa watu kama Stephen Wassira, Jumanne Maghembe, Matayo Matayo, Mathias Chikawe, Celina Kombani, Sofia Simba, Adam Malima na wengine wengi.
Pili hatukuamini kama rais angewarejesha watuhumiwa wa kughushi ambao wanajulikana kuwa ni Makongoro Mahanga, Mary Nagu na Wiliam Lukuvi.
Tatu, rais amelazimika na kupoteza imani na muda wetu bure. Tulitegemea mapya lakini ameturejeshea mvinyo ule ule kwenye chupa ile ile. Hivi rais wetu atajifunza lini wakati muda ukizidi kuyoyoma? Je wabunge waliotunisha misuli na kuondoa baadhi ya mawaziri wataridhika na dhihaka hii? Kwanini rais hakufanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri badala ya kutupotezea muda na kutuweka kwenye sintofahamu kwa muda mrefu. Hakika kilichofanyika licha ya kuwa dhihaka na usanii, ni taarifa kuwa Tanzania itazidi kuendelea kuelekea kuzimu.
Tumewahi kusema kuwa serikali ya Kikwete ni ya ubia na kuna watu wenye shares nyingi. Nao ni hao ambao hawagusiki bali huwa recycled kila mara.
Mfano mdogo ni kwamba kwa mazabe na madudu aliyotenda mtu kama Adam Malima, kama siyo kulindana kwa misingi yoyote iwayo hakupaswa kurejeshwa au tuseme kuwa recycled.
Hakika hili si baraza jipya la mawaziri bali baraza kuukuu na la kishikaji na Jakaya Kikwete. Kweli Tanzania tunayo safari ndefu.
Ahsante sana Mpayukaji ninakubaliana na kukuunga mkono 101% ubarikiwe sana!
 
January Makamba a.k.a mathread aligushi na kuiba mtihani wa Form 4 pale Galanos. Rungu la necta likamuangukia lakini leo hii anatuongozea science na teknolojia. Hii nchi usanii mtupu na ninaamini kuwa hili baraza ni mpango wa Mungu kuiua kabisa ccm
 
Je baraza lote umelipitia? ok lipo humuhumu JF pitia mkuu faster then rudi kurekebisha
 
Matakwa ya Raisi yanawezeka yakawa tofauti na matakwa yako,kwaa uraisi nasi tulonge mkuu.
 
Pole na kazi ngumu sana ya kuchambua nani anafaa kuwa Waziri na Hatimaye umefanikiwa kwa kiasi fulani
Mh Rais nakumbuka umemteua mh Mark Mwandosya kuwa Waziri asiyekuwa na Wizara maalum,je katibu mkuu wake na ni katibu Mkuu asiye na wizara Maalum?
Ofisi zake zitakuwa wapi?au pia ni ofisi zisizokuwa Maalum?je atatumia Gari Maalum?au atakuwa na gari lisilokuwa maalum?
Je kwa kuwa Mawaziri wanapewa nyumba na wizara na yeye itakuwaje? Au atakaa nyumba isiyokuwa maalum?
Atawasilishaje bajeti yake?au atawasilisha katika kipindi kisichokuwa Maalum?
Atajibu Maswali yapi Bungeni?au atajibu hoja zipi bungeni? Au yote yasiyokuwa maalum?
Akikosea atawajibika kwa nani? Au kwa Waziri mkuu asiyekuwa maalum!?
Kwa umemteua bila lengo Maalum b asi najua Hatofanya kazi Maalum ila bora ungemtamka kama Naibu Waziri Mkuu..
Hoja hii sio Maalum..
Haiitaji majibu maalum
Karibu kwetu Tanga ulipopokelewa na wanachama wa chama kisichokuwa Maalum
Ni mimi nisiyekuwa Maalum mgosi Mgeni wenu Maalum wa JF
 
Kikubwa nitakachoki-miss ni Sauti yake ya ukali na Jazba mara anapojibu hoja za Wabunge.

Kwaheri Agrrey Mwanri.

leroy................kwa kheri ya kwenda wapi?
 
Last edited by a moderator:
ooh, unanikumbusha maandiko ya Shabaan Robert; yaani ujumbe, mkong'oto, kejeli na mafumbo humo humo. Ujumbe self contain!!!
 
Back
Top Bottom