Hili ndilo baraza lililokuwa linasukwa kwa week mbili? Unampaje unaibu waziri wa nishati na madini Steven Masele na kumuacha geologist Dr Peter Kafumu? Na Mwandosya afya yake inaendeleaje maana naona yumo kwa mtindo wa kizamani wa wizara isiyokuwa na kazi maalum?
Ukweli hili baraza litaharakisha kifo cha CCM. Limejaa wapambe na marafiki! Ni watu wachache sana watakaofanya kazi. Kwa mbunge yoyote wa CCM anayetamani kurudi bungeni 2015 basi aanze kufanya tararibu zingine. Hakuna namna, CCM itapata shida.
Pia, naomba ufafanuzi. Dr Hussein Mwinyi ni mbunge toka Zanzibar, sasa anasimamiaje wizara ya Afya ambayo sio ya muungano?