Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Mgaya Kingoba,
Ngorongoro
Mgombea urais wa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonesha mfano katika kuhimiza ufugaji wa kisasa na usio wa kuhamahama kufuata malisho, akimiliki ng'ombe 400 ambao malisho yake yanalimwa katika shamba lake.
Amewaambia wafugaji nchini kwamba kama hawajui ng'ombe wao watakula nini, ni bora wasifuge.
Alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti mjini Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya wiki hii na juzi alikuwa Loliondo wilayani hapa, kote akiomba kura kwa wananchi.
Rais Kikwete alieleza hayo wakati akifafanua kuhusu ilani ya Uchaguzi ya CCM, inavyoelekeza juu ya ufugaji wa kisasa na hasa kuhakikiksha wafugaji hawaendelei kuhamahama kwa nia ya kusaka malisho.
"Mimi pia nafuga, nina ng'ombe si haba. Sasa nimelima majani, nina ng'ombe 400 na ekari 600, na nimechimba kisima napata maji pale," alieleza Rais Kikwete bila kufafanua lilipo shamba lake.
"Katika kiangazi kikali cha mwaka, hakuna ng'ombe wangu hata mmoja aliyekufa. Sina ugomvi na jirani yangu. Ni kitu kinachowezekana tunaposema ufike wakati wafugaji wasihemeane na wawe na malisho ya mifugo yao.
Alisema kama mfugaji hajui ng'ombe wake watakula nini, ni bora asifuge kwa sababu kwa mwenendo wa sasa, ufugaji wa kuhamahama hauna muda mrefu……
Chanzo: HABARILEO Jumapili.
Kikwete mtu mmoja hekari 600 za kuchungia ng'ombe wake wakati Wamasai wanahangaika na ngombe wao hawana sehemu za kulishia, wamenyang'anywa na Kikwete, na serikali yake.
inasikitisha zaidi ukifika,wananchi wa muheze,handeni wanavolima machungwa mpaka yanaozea shambani hakuna wateja leo hii wanaambbiwa walime majani....walishe ng'ombe,masoko mabovu,sijui huyu jamaa anaongea nini sera zao mbovu....eti kilimo kwanza....kilimo bila masoko??yeye hapo anatenda kusambaza maziwa hospitali fulani......iko siku ntajitoa akli na kushika bunduki!!!Mkuu upo sahihi kabisa..........Pia on the way to Handeni, you can see this just besides the road. Inasikitisha sana.
I don't see anything wrong if JK owns a farm or cattle.
Former presidents Bush and Carter own ranches in Crawford, Texas, and Plains, Georgia. So why not JK?
Is it a sin for a government official to own even a farm inTanzania?!!
This is very ridiculous and cheap shot