Elections 2010 Kikwete afichua anamiliki ng’ombe bora 400

Elections 2010 Kikwete afichua anamiliki ng’ombe bora 400


Na Mgaya Kingoba,
Ngorongoro

Mgombea urais wa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonesha mfano katika kuhimiza ufugaji wa kisasa na usio wa kuhamahama kufuata malisho, akimiliki ng'ombe 400 ambao malisho yake yanalimwa katika shamba lake.

Amewaambia wafugaji nchini kwamba kama hawajui ng'ombe wao watakula nini, ni bora wasifuge.

Alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti mjini Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya wiki hii na juzi alikuwa Loliondo wilayani hapa, kote akiomba kura kwa wananchi.

Rais Kikwete alieleza hayo wakati akifafanua kuhusu ilani ya Uchaguzi ya CCM, inavyoelekeza juu ya ufugaji wa kisasa na hasa kuhakikiksha wafugaji hawaendelei kuhamahama kwa nia ya kusaka malisho.

"Mimi pia nafuga, nina ng'ombe si haba. Sasa nimelima majani, nina ng'ombe 400 na ekari 600, na nimechimba kisima napata maji pale," alieleza Rais Kikwete bila kufafanua lilipo shamba lake.

"Katika kiangazi kikali cha mwaka, hakuna ng'ombe wangu hata mmoja aliyekufa. Sina ugomvi na jirani yangu. Ni kitu kinachowezekana tunaposema ufike wakati wafugaji wasihemeane na wawe na malisho ya mifugo yao.

Alisema kama mfugaji hajui ng'ombe wake watakula nini, ni bora asifuge kwa sababu kwa mwenendo wa sasa, ufugaji wa kuhamahama hauna muda mrefu……

Chanzo: HABARILEO Jumapili.





Aisee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Swali moja tu. Amepata hizo ng'ombe na hilo shamba kihalali?
 
unajua huyu mzee anaona watu wapumbavu sana..kweli mfugaji wa kule Isevya Tabora anaweza kulima shamba la majani na kulisha ng;ombe?kweli???? mi nataka kutapika kwa kweli
 
Sisi tuna hawa.....hawakai bandani hawa lazima waende machungani

Heardofcattle_wide-vi.jpg


Yeye Bwana Mkubwa ana hawa....mazezeta yanatulia tu bandani

cattle-herd.JPG
 
duu, na hao ngombe anakuwa nao kwenye kampeni? nao anawavalisha kijani?
 
Kikwete mtu mmoja hekari 600 za kuchungia ng'ombe wake wakati Wamasai wanahangaika na ngombe wao hawana sehemu za kulishia, wamenyang'anywa na Kikwete, na serikali yake.

If George Bush owns a ranch in Crawford, Texas, then why is it that people make it a big deal for JK?
Is it a sin for anybody to own a farm or cattle?
 
Kama kuna mfugaji atampa kura JK sijui bse amewatenda sana hawa watu
 
I don't see anything wrong if JK owns a farm or cattle.
Former presidents Bush and Carter own ranches in Crawford, Texas, and Plains, Georgia. So why not JK?
Is it a sin for a government official to own even a farm inTanzania?!!
This is very ridiculous and cheap shot
 
Yaani wewe kiongozi wa nchi badala ya kutoa ushauri kwa wafugaji jinsi ya kujiendeleza unawaambia kama hawajui ng'ombe wao watakula nini basi wasifuge. Halafu unategemea hao hao unaowakatisha tamaa wakupigie kura? Only in Tanzania.
 
Hahahaha
I loooooooooooove JF
Watu wana mawazo chanya dhidi ya tabia hasi
 
Mkuu upo sahihi kabisa..........Pia on the way to Handeni, you can see this just besides the road. Inasikitisha sana.
inasikitisha zaidi ukifika,wananchi wa muheze,handeni wanavolima machungwa mpaka yanaozea shambani hakuna wateja leo hii wanaambbiwa walime majani....walishe ng'ombe,masoko mabovu,sijui huyu jamaa anaongea nini sera zao mbovu....eti kilimo kwanza....kilimo bila masoko??yeye hapo anatenda kusambaza maziwa hospitali fulani......iko siku ntajitoa akli na kushika bunduki!!!
 
I don't see anything wrong if JK owns a farm or cattle.
Former presidents Bush and Carter own ranches in Crawford, Texas, and Plains, Georgia. So why not JK?
Is it a sin for a government official to own even a farm inTanzania?!!
This is very ridiculous and cheap shot

Since human have unequal opportunities hence inequality exists in any society depending on how one uses the opportunity............plz read between the lines,sioni tatizo la kikwete kuwa na ng'ombe wote hao,kwasababu yuko kwenye pahali aweza wapata,the only thing inanisumbua mimi....aliwapataje hao ng'ombe??Ardhi je??kitendawili cha ajabu.....analima majani kwaajili ya ng'ombe while kunawatu wanakufa na njaa sio sababu wavivu wa kulima bali sababu ardhi yao ni duni mvua hakuna......usishangae majani yakawa yanamwagiliwa.Nausimlinganishe yeye na Bush ama Carter unaichekesha jamii..........
 
Back
Top Bottom