Mtemikwila
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 1,389
- 1,063
Umewahi sikia shule za middle school??? mtu wa darasa la nne kipindi hicho ni kidato cha nne kwa sasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ulikuwepo TMA Monduli 1970s?Kwanza si kweli, lakini pia maisha bila fitna hayaendi. Kina chausiku ni fitna tupu mpaka mwenyekigoda wao amekuwa wa maisha.
Aaaaaaa jamani! Yaani apewe nafasi hiyo, hata kama "HAKUWA AMESONA", basi hata awe hata kusoma hajui kweeliii!!!!?
NdiokIPINDI HICHO KULIKUWA NA FOTOKOPI MASHINE KWELI?
mgazeti yalikuwa yanachapwaje?...mitihani je?hearsay and gossip. fotokopi monduli miaka ya 70 wadanganyika bana!
Mzee wa figisu😂😂Kipindi hicho mkuu wa chuo alikuwa Gideon Sayore, Kikwete alikuwa ni mmoja wakufunzi wa siasa chuoni hapo.
Sasa ilikuwa hivi,
Mzee Sayore alikuwa anafuga ng'ombe wengi pamoja kufanya shughuli za kilimo kwa wingi wakati huo huo akiwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli.
Hivyo basi baada ya kuona ng'ombe wanatoa maziwa mengi mno na mazao yametapakaa mashambani akaamua kuwa awe analiuzia jeshi mazao kama vile maharage na mahindi pamoja na maziwa na nyama kutoka kwenye mifugo yake.......na pesa anachukua yeye mwenye mazo.
Aliendelea kufanya hivyo kwa kipindi kirefu tu.. ikiwa ni kama sehemu yake ya maisha....
Sasa bwana kumbe Kikwette (JK) ilikuwa inamuuma sana sana, yaani mno! Sasa haieleweki kama ilikuwa kweli ni kwa uzalendo ua wivu tu....akaandika barua kwa Rais kipindi hicho JK Nyerere.
Katika barua hiyo akaandika lawama nyingi mno na majungu mengi sana dhidi ya Sayore, akimwita bepari, bwenyenye, mnyonyaji n.k huku akisema hafai kuwa mkuu wachuo hicho kwa kuwa inavunja miiko ya uongozi na mambo mengine mengi (si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna!)...
Basi bwana, akamalizia mwisho kwa kujiandika jina lake na sahihi yake huku akijiita mzalendo kamili barua ikapostiwa ikiwa imeadresiwa kwa Rais wa nchi wakati huo!......
Mwalimu, aliipata barua ile aliifungua akaisomaaaa kisha akapiga hesabu zake....sijui aliwaza nini mzee yule, akaihifadhi ile barua ikaa sana ofini kwake bila kuchukua uamuzi wowote.
Siku moja alipokuja mkuu wa majeshi wakati huo "General Mtukula" (David Musuguli) ofisini kwa Mwalimu eaisi kipindi hicho, mwalimu akampa ile barua kutoka kwa Kikwete "akisema hayo ni mambo yenu kayamalizeni hukohuko".
Basi bwana ile barua Mkuu wa majeshi alikaa nayo muda hivi kwenye makabrasha yake. Sasa siku moja alikuja Mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli(Sayore) Dar es salaam kufanya shughuli za kikazi akaenda hadi ofisini kwa Mkuu wa majeshi.
Baada ya shughuli kwisha na Sayore akiwa anajiandaa kwenda Monduli Mkuu wa majeshi alimwita, akampa ile barua ya Kikwete aliyomwandikia Rais!!
Sayore akaisoomaaa we akashangaa mno!! Na akafura kwa hasira yule mmasai...., akuliza mwalimu kasemaje? Akaambiwa mwalimu kasema yamalizeni wenyewe!!.... Akasema naam, na akaondoka na ile barua hadi Monduli...
Alipofika tu yule mmasai aliitisha kikao cha wakufunzi wote na wakuu wengine pale chuoni, wakati wanajikusanya kwenda kwenye chumba cha mkutano yeye aliamua kwenda kutoa copy ile barua ya Kikwete, kopi nyingi idadi sawa na wajumbe wa mkutano ule....
Alipoingia mkutanoni akawaona wakuu na wakufunzi wote wameketi wakimsubiri wajue alicho waitia,.. akaanza kwa kuwauliza..jamani kama kuna mtu ana matatizo, au anaona kuna jambo haliendi sawa anyooshe mkono na saemekinacho mkereketa......watu wote wakawa kimya huku wengine wakisema hamna mkuu akiwemo Kikwette!!!
Basi bwana, tumalizie mkasa huu wa mkwere...
Sayore akaanza kuwagawia zile nakala (copies) za ile barua ya Kikwete kwenda kwa rais akawagawia wooote including Kikwete!!! Huku yule mmasasi Sayore akiwa amefura kwa hasira, macho mekunduuu! Akagonga ngumi juu ya meza kwa hasira na kusema someni hiyo barua!! kisha akatoka na kusema anakuja muda si mrefu...
Hapo Kikwete akajua kifo chake kimefika, akikumbuka macho ya yuile mmasai! akatetemeka macho yakamtoka lip! kwa woga!.. na wenzie wakamwanzishia zogo mle ndani......
Alichokifanya ni kuondoka haraka pale kikaoni wenzie wakajua bado yupo chuoni, kumbe safari ya Dar ikawa imeanza...!! Jamaa alitembea uchochoroni kwa muda mrefu sana huku akiogo kabisa kuingia barabara ya kuu...
Mashuhuda wanasema yule bwana akaja kupanda lift ya gari za vyama vya ushirika maeneo ya USA RIVER, hakukumbuka kubeba mzigo wowote!! Just imagine kutoka Monduli hadi hapo jamaa aliteseka sana... lakini yeye hakujali, cha muhimu ilikuwa kusalimisha maisha yake......
Basi huo ndiyo ukawa mwisho wa JK Monduli,........... hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama... lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!!
Hicho ndicho chanzo cha JK kumchukia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadi leo! Yeye humwita mzee Nyrere tu au mwalimu baasi...na mara chache akiwa nje ya nchi humwita 'Father of our Nation', lakini ni pale anapotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu....
**Ndugu zangu hiki ni kisa cha ukweli kwa 100%, inawezekana uandishi wangu ukawa na upungufu, lakini niemekipata kutoka watu mbalimbali waliowahi kuwa karibu sana na mkasa huu.
Barua za kijeshi bila file. Badala ya kwenda kwa IO. inazunguka mkononi kirahisi hivyo. Ni kweli General alikuwa akifanya biashara, mkewe na sio General. Mkumbuke mkuu alikuwa aruhusiwi kufanya biashara. Wakati ule.Jamani kama mnakumbuka ilishakuja thread ya Kikwete na monduli sio siku nyingi sana na nilicomednt kuwa hakustaafu ila alikimbia, it true story and frankly i got the info from my father who is a friend and neighbour of Gen. Sayore, BIG UP mwanzisha sredi
Funga Domo weweWabongo kwa kupenda majungu, sasa kisa hicho kitawasaidia nini hata kama ni kweli.
Mtoa mada kaandika uongo wa kimajunguVIPI MONDULI UMBALI WAKE NA USA RIVER SIO KWELI UTOKE MONDULI KWA MIGUU UPITE MJI WA ARUSHA USIPATE LIFT BADO UENDELEE KUTEMBEA MPAKA USA RIVER WAPI NA WAPI SIO KWELI
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hahahahaha ww mjeshi akwambia subiri hapo nije nikuoneshe afu unabaki kabisa.....hahahhaha utakuwa hujipendiHahahaa ni noma sana,hapo aliona mmasai anaenda kuchukua BOMBA akona bora ajikatae.
Barua lazima kupitia file. Ndipo ipitishwa kwa Rais. Sio barua ya kishikaji, ni barua ya kishushushu. Na Gen aliasing fomu ya kiapo cha kutokuwa na hisa wala kipoto cho chote njee ya Utumishi wake. Na hii ilikuwa taarifa kwa Mkuu wa nchiMh. Kikwete na Mwalimu Nyerere, usiseme usilolijuwa mpaka Mh. Kikwete kufika madaraka ya juu toka chini ni mkono wa Mwalimu ulihusika kwa asilimia kubwa sana.
Viongozi wengi wakubwa walipikwa na kuandaliwa na Mwalimu tena kwa mapenzi makubwa.inawezekana ilikuw kweli ila njia za Mwalimu kufundisha mtu zilikuwa ngumu sanaaa.
Vipi kuhusu mzee Mwamindi na ishu ya ujamaa!Unahisi haikuwa wivu pia?.dU...hII NI KALI!
Ingekuwa ni sasa tungepata hiyo barua ikawa scanned na kuwekwa hapa!
Usikute Mkapa alipokuwa anasemea "wivu wa kike" alikuwa kiaina anamng'ong'a jamaa!
Kumbe hakuondoka kwa mema Monduli huyu!...nitafuatilia kisa hiki maana kuna wazee waliokuwa naye enzi hizo Monduli!
Ukizingatia na sakata la mzee Mwamindi kuchabanga somebody kleruu.Licha ya kwamba siufagilii uongozi wa sasa unachofanya,bado nadhani mwenye kosa alikuwa mwalimu Nyerere hapo,tuondoe upofu wa chuki then tu analyze without bias...Mbona kuna wanasiasa kibao tu wamepitia misukosuko similar?Kina Sitta,Zitto nk.
Kwanini hatushangazwi kuwa pamoja na yote hayo sasa amekuwa mkuu wa nchi?
Kwa wakati ule taarifa kama hiyo ingetemewa kuwa itamfurahisha mwalimu,ama mwalimu alishindwa namna ya kumwajibisha mjeshi?Kiukweli alichofanya Sayore kilikuwa ni kinyume na siasa mwalimu alizokuwa akizi preach kwa wakati ule,je ni kosa kwa JK kumshtua kuwa kuna tabia za kibwanyenye at the time when nchi iliendeshwa kiujamaa?
Kuna tofauti ya "kutoa copy" na " ku-fotokopi". Kumbuka ku-fotokopi ni subset/kipengere ndani ya kutoa copy.kIPINDI HICHO KULIKUWA NA FOTOKOPI MASHINE KWELI?
Sababu gani? Maana mimi nilikuwa sijazaliwaUnajua sababu za Kifo cha Malima Kighoma?