Elections 2010 Kikwete ana washabiki wengi sijui ni kwanini

Elections 2010 Kikwete ana washabiki wengi sijui ni kwanini

mbali na wananchi wa tz kuwa katika shida kubwa katika kipindi cha kwanza cha kikwete lakini ni umati mkubwa ulijitokeza jana kumuunga mkono mjini morogoro , sijui ni kwanini watu wamefurahisha na yeye anavyoonekana bila ya sera au nini wanachokiona ambacho ni kikubwa toka kwake.

JK anakubalika sana, JK amefanya mengi hata wewe unayaona lakini kutokana na imani ya chama chako umepaka macho kiwi. CCM NI NAMBARI WANI JK. HOYEE.
 
JK anakubalika sana, JK amefanya mengi hata wewe unayaona lakini kutokana na imani ya chama chako umepaka macho kiwi. CCM NI NAMBARI WANI JK. HOYEE.
kuna mambo nayaona ameyafanya lakini kama rais alitakiwa kufanya zaidi kwa mfano kulinda rasilimali zetu hasa madini na gas, kingine daima mimi ni mtu neutral kwahiyo sitoegemea upande wowote, ninachokiona katika nchi yetu ni kushindwa kwa mfumo wa kisiasa ambacho kinaweza kuleta matatizo kwa taifa letu, bado nadhani hata wewe unatambua maisha bora kwa watanzania bado
 
JK anakubalika sana, JK amefanya mengi hata wewe unayaona lakini kutokana na imani ya chama chako umepaka macho kiwi. CCM NI NAMBARI WANI JK. HOYEE.

Itafaa kutupa mifano miwili mitatu hivi ya mazuri yake ndani ya miaka 5 aliyokuwa rais wa Tanzania.
 
Watanzania wengi wetu tumesoma lakini hatujaelimika. Sababu kubwa ni kwamba hatuna kipimo cha kumjaji mtu kama JK huko uswahilini. Watu wanaangalia anavyocheka na kudanganya watu kuwa ndio kipimo chao. Mmi nadhani tumpime JK kwa kona mbili kuu, mosi kwa kumlinganisha na maraisi waliopita kiutendaji, pili, nini amewafanyia watanzania katika miaka mitano hii.

Kwa maoni yangu binafsi nampa 1/6 (moja juu ya sita).
 
JK anakubalika sana, JK amefanya mengi hata wewe unayaona lakini kutokana na imani ya chama chako umepaka macho kiwi. CCM NI NAMBARI WANI JK. HOYEE.

Mkuu husilete ushabiki usiokuwa na maana twambia KAFANYA NINI CHA MAANA KWA MIAKA 5??

kAMA unafikilia UDOM JK kaimba mawazo haya toka kwa chadema, mana hii kitu haipo kwenye irani ya CCM
 
:jaw:Jaji Warioba avunja ukimya
• Asema uongozi umebinafsishwa kwa wenye fedha

na Bertha Mwambela na Violet Tillya, Tanga


amka2.gif
WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amekemea matumizi mabaya ya fedha katika uchaguzi, akisema yameingiza sumu mbaya katika mchakato wa kuwapata viongozi na kulifanya taifa litawaliwe na ‘wafadhili’ badala ya viongozi.
Jaji Warioba, alisema hayo jana wakati akifungua kongamano la mwaka la maadili ya waandishi wa habari mjini hapa, lililoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Alisema uongozi umebinafsishwa na kugeuzwa biashara ya wenye fedha na kwamba ndiyo chanzo cha siasa za chuki, kashfa, malumbano na mgawanyiko.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, hali hii ndiyo imeleta mgawanyiko na hali tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Hali hii ikiendelea nchi itafikishwa pabaya. Ni lazima kutafakari na kuchukua hatua. Nchi inahitaji viongozi badala ya wafadhili… uchaguzi, hasa uchaguzi wa kutumia fedha na kashfa, ndiyo umetufikisha hapa,” alisema Jaji Warioba.
Akitoa mfano, Jaji Warioba alisema huko nyuma hali hiyo iliwahi kutokea.
“Kumbukeni vizuri mwaka 1995 walijitokeza wanachama 19 waliopendekezwa kugombea urais, hata walipopunguzwa na kubaki watatu na hatimaye mmoja, chama hakikugawanyika maana hakukuwa na makundi,” alisema Jaji Warioba.
Alisema, hata walipotolewa nje ya ukumbi na kuanza kujadiliwa na vikao vya juu, walikuwa wanacheka na kutaniana kwa maneno kama: “Unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.”
“ … lakini hali ya sasa ni tofauti kwani ushindani wa kisiasa unaelekea kugeuzwa uadui.”
Jaji Warioba aliwakejeli wanasiasa wanaotangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, wakidai wamechangiwa fedha na wananchi ili walipie fomu za kugombea, akisema fedha hizo ni zao wenyewe, si za wananchi maskini wanaosingiziwa kuchanga fedha hizo.
Kwa mujibu wa Warioba, fedha zimemaliza hata nguvu ya kamati za maadili ndani ya vyama, ambavyo badala ya kuwachukuliwa hatua wanachama kama ilivyokuwa zamani, vinaishia kuwashtaki Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Kongamano hilo lililokuwa likijadili wajibu wa vyombo vya habari katika uchaguzi, lilishirikisha wahariri, wamiliki, viongozi wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Bara na Visiwani na wadau mbalimbali wa habari nchini.
Walijadili, pamoja na mambo mengine, Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambayo Jaji Warioba alisema ina madhumuni mazuri, lakini matendo ya viongozi yanaonyesha kuwa hayaendani na matakwa ya sheria hiyo.
Alisisitiza, hata Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ndiye msimamizi mkuu wa utekelezaji wa sheria hiyo, hana uwezo, hana zana za kutosha za kuitekeleza.
“Ofisi yake iko Dar es Salaam, uchaguzi uko nchi nzima, ana wafanyakazi wachache, raslimali chache… ni mtumishi wa serikali…hana ubavu,” alisema Jaji Warioba.
Alisema hata TAKUKURU, haiwajibiki kwa Msajili na Vyama vya Siasa, nayo haina uwezo wa kuwabana wanasiasa ambao tayari wanagawa pikipiki na baiskeli.
“Ni vigumu kwa chombo cha umma kuwadhibiti viongozi walio madarakani, ndiyo maana hata katika mapamabano ya ufisadi, walio madarakani hawakuguswa,” alisema Jaji Warioba.
Jaji Warioba alieleza kuwa katika miaka ya nyuma mgombea yeyote aliweza kupita bila kupingwa kutokana na kukubalika katika jamii tofauti na sasa ambapo wagombea wengi wanaonekana wamekuwa wakinunua uteuzi katika vyama vyao na kuwanunua wapinzani ili kuvuruga taratibu za uchaguzi.
Alisema, uteuzi wa mgombea ni hatua muhimu katika mchakato wa uchaguzi kwenye majimbo mengi ambapo uchaguzi unaishia kwenye uteuzi.
Akitoa mfano, alisema Tanzania Bara CCM ina nguvu kubwa katika majimbo yalio mengi, jambo ambalo linamfanya mteule wa CCM kwa nafasi ya Rais kuwa na uhakika wa kushinda.
“Kwa sababu ya umuhimu wa uteuzi, fedha nyingi zinatumika, CCM imeamua kura za maoni iwashirikishe wanachama wake wote kwenye ngazi ya kijiji, kuna imani kuwa mgombea hawezi kuhonga wanachama wote ngazi ya kijiji. Imani hii ni potofu, kwani hivi sasa kuna watu wanatamba watatumia sh milioni 200 kwenye jimbo la uchaguzi,” alisema Jaji Warioba.
Alisema wagombea hao wana uwezo wa kuhonga kila mwanachama hata sh 1,000 kila mtu na wana uwezo pia wa kununua mamluki. Alisisitiza kuwa tayari kadi za vyama vya siasa hasa CCM zinauzwa kwa madhumuni hayo.
“Hakuna uchaguzi ambao hauna udanganyifu, kwani wanaogombea
uongozi hutumia kila mbinu ili kushinda na wakati mwingine mbinu zisizo halali hutumika; inawezekana udanganyifu ukaanzia kwenye zoezi zima la uandikishaji hadi kwenye hatua ya kupiga, kuhesabu na kujumlisha kura. Udanganyifu umekuwepo kila uchaguzi unapofanywa,” alisema Jaji Warioba.
Alisema viongozi wamekuwa wakikiuka maagizo ya Rais na hawachukuliwi hatua yoyote. “Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni na hasa baada ya kutungwa kwa sheria za gharama za uchaguzi, amekuwa akilaani vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi, lakini viongozi walio chini yake ndani ya CCM na serikali kwa ujumla wao wako kimya badala yake wanagawa vitu majimboni,” alisema Jaji Warioba.
 
Watanzania wengi wako kati ya kundi la asilimia 70 aliyosema kikwete................................. aliwafahamu vizuri!
 
Hata hapa kaangalie alivyopigiwa debe katika thread ya Marilyn Mashiba sijui kwa kikubwa kipi alichokifanya. Mitanzania ndivyo ilivyo!


Aaaah, kumbe wewe PELE hujaona JK kaalikwa kwenye sendoff ya huyo Marylin, thats y kampigia debe sana ili ahudhurie hiyo send off yake.

IMG_0414+-+Copy.jpg


JK akimlisha keki Marilyn Mashiba kwenye mnuso wa send off
 
kwa kuwa watanzia wengi hamna kitu kichwani.

jiulize wewe uliyekuwa na shahada za kisomi..................lini ilikuwa mara ya mwisho kusoma kitabu chochote? kwa jamii inayoogopa vitabu tusitegemee miujiza. watampenda kikwete, karamagi na wenginewe coz they dont know better.
 
mbali na wananchi wa tz kuwa katika shida kubwa katika kipindi cha kwanza cha kikwete lakini ni umati mkubwa ulijitokeza jana kumuunga mkono mjini morogoro , sijui ni kwanini watu wamefurahisha na yeye anavyoonekana bila ya sera au nini wanachokiona ambacho ni kikubwa toka kwake.


Wabongo wengi ni bongolala haiwezekani pamoja na matatizo yote hayo bado watu wananunuliwa kwa kofia,fulana na khanga kwenda kumuunga mkono muungwana.
 
lakini wachangiaji wengine wanatumia pointi ya kuwa wananchi wetu hawana elimu lakini cha kushangaza wanachuo wa UDOM nao walikuwa kwenye mkumbo wa kujianika juani kumshangilia kikwete mbaya zaidi wanachuo hawa ambao wanalalamikia bodi ya mikopo kutowapa pesa ya kutosha na wanajiita watoto wa wakulima walimchangia kikwete mamilioni ya kuchukua fomu na kufanya kampeni hapa wajumbe suala hili mnalionaje?
kwa taarifa yako zile hela walipewa na ccm wenyewe,na ili kudhibitisha hili tafuta mwanachuo mnaejuana mwulize atakuambia ni mambo ya ridhiwani hayo.
 
Katika post fulani, mjumbe mmoja amesema, "Tanzania is full of plastics" nina uhakika hakumaanisha planics hizi za mitaani, bali tools of analysis katika vichwa vya watu.
 
Wenye hekima walikwisha sema huyu jamaa ni "Msanii", msanii anaweza kuwa hana jipya ila kwa vile watu hawajui au kuona mbadala, wakaendelea kumshabikia. Pia msanii akiona ameishiwa sanaa, anaanza mbwembwe zisizokuwa na maana ilimradi tu, aonekane kama bado wamo!
Ila pia tukumbuke nchi zetu viongozi wengi bado wanatumia "kamati za ufundi" kuwaongezea mvuto. Pale Bagamoyo siyo mchezo, lazima kuna kamati za ufundi zinafanya mambo! Haiwezekani jamaa hajafanya chochote cha maana katika kutimiza ahadi zake, leo wananchi wanakuwa kama wamelogwa kumshabikia bila rekodi. Kwa staili hii tusitegemee kupiga hatua ya maana kimaendeleo katika kipindi kijacho.
 
Inawezekana Ndg. Ladslaus unanufaika binafsi kwa njia moja ama nyingine kwa CCM kuwa madarakani, haiwezekani kwa mtu anaeifahamu nchi hii ilivyo barikiwa kwa rasilimali nyingi, mtu safi mzalendo anayewapenda wananchi wenzake hata kama si ndugu zake, mtu mwenye uchungu wa maendeleo ya pamoja na mtu mcha Mungu wa kweli, haiwezekani kabisa kabisa akaishabikia CCM kuendelea kuongoza. Kama chama kinacho ongoza serikali kingekuwa makini kwa kulinda na kutumia vizuri rasilimali zote nchini, kuanzia rasilimali watu, vitu, ardhi, hali ya hewa, maliasili, maziwa na bahari. KWA JINA LA YESU, leo tusingekuwa hapa tulipo. Tusingetegemea wafadhili watunakshie bajet ya serikali ya mwaka. Kwa vile shetwani katushika pabaya, ndo maana unaona harufu mbaya za ufisadi, rushwa, elimu ya kisanii(tunatengeneza mafisadi wengine), huduma duni za afya-mpaka chandarua, vyoo vya shule tunasubiri wahisani na mambo mengine yanayofanana na hayo! Ndg. Ladislaus mpende jirani yako unaemuona anasota na maisha ndipo utaweza kumpenda Mungu asiye onekana.
 
Aaaah, kumbe wewe PELE hujaona JK kaalikwa kwenye sendoff ya huyo Marylin, thats y kampigia debe sana ili ahudhurie hiyo send off yake.

IMG_0414+-+Copy.jpg


JK akimlisha keki Marilyn Mashiba kwenye mnuso wa send off

Hii ni send off au harusi? Kwani kwenye send off mwanaume umlisha keki bi harusi mtarajiwa? Na huyo mume mtarajiwa atakuwa Bushoke tu! Au ni ndugu yake?????
 
watu wanafuata sura....na alivyojipiga ma scrub ndo mng'aro unazidi basi walugulu ni vigeregere mwanzo mwishoo..lakini mwisho wa siku ni kuwa upumbavu wetu ndo unaotuponza
 
Back
Top Bottom