Kikwete ashusha bei vifaa vya ujenzi

Kikwete ashusha bei vifaa vya ujenzi

Ndo unaamka nini unatuletea ndoto yako ya mchana.
 
Viwanda vya simenti kama 6 vipya vinakuja, ni lazima itashuka, lakini si ile ya Slaa.
 
Ni kweli mfuko wa cement umeshuka mpaka shilingi 12,500/=?
 
Mkuu ni viwanda sita au kimoja tu kila cha Alhaj Aliko Dangote cha Mtwara?
 
...kapunguza kwenye maduka yake au nchi nzima!?
 
Kikwete sasa ameanza kazi, Nondo mm 12 ef 14500, sementi mfuko sh 12400,misumari,bati bei ni bwereree,hadi raha.kama una ujenzi wako wakati ni huu.

kwa wale wanaotaka kujenga,tuwasiliane,nakuletea cement kutoka china bei yangu ni 10,000/50kg,hakuna punguzo hapo
 
baadhi ya hoja zinaishushua hadhi na heshima JF! nikumbukavyo mimi JF ilikuwa chanzo cha habari nyingi sahihi,sasa weledi huu unaanza kutoweka taratibu.
Tusifanye hivyo ndugu zangu,tumuulize mleta mada kwa lugha nzuri ili kama hata alikuwa anatania ama vyovyote tumuombe aiondoe mada.ila kama ana uhakika atuletee ili JF ibaki chanzo sahihi za habari vunjifu na muhimu kuzipata
 
Magamba its time you go now, hata mkishusha mfuko wa cement ukawa shs 10, hatudanganyiki wezi wakubwa nyie
 
Whether hii stori ni kweli au la, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa:

  1. CCM imekurupushwa usingizini na kuanza kuendeleza infrastructure (barabara) kwa kasi sasa hivi. Good!
  2. baadhi ya mawaziri wa CCM wameamka usingizini sasa wameanza kuchapa kazi (hope it lasts though). Excellent!
  3. watendaji wengi kwenye taasisi za umma wameanza kuogopa ku-chop (kuiba ovyo). Splendid!
  4. frequency ya safari za JK walau kidogo inaanza kupungua. Encouraging!
  5. hakuna ubishi kuwa hayo yote hapo juu 1-4 yameletwa kwa hisani kubwa ya Operation Sangara, Vua Gamba Vaa Gwanda & sasa M4C
  6. simple logic arithmetic.....kama wabunge less than 50 wa Chadema wameweza kusababisha mabadiliko yote haya ndani ya miaka 2 tu, vipi wakipewa kuongoza nchi walau kwa miaka 5? Fanya extrapolation mwenyewe hata kama hisabati haipandii!!
 
Kikwete sasa ameanza kazi, Nondo mm 12 ef 14500, sementi mfuko sh 12400,misumari,bati bei ni bwereree,hadi raha.kama una ujenzi wako wakati ni huu.

Weka takwimu zako sawa maana unaposema bwerereeeee unamaanisha hakuna malipo, ni bure? Hizo gharma ni fixed kwa mikoa yote ama ni kwa DSM pekee? (Kule mkoani e.g. Mwanza bei ya mfuko wa cement ni 20,000/=). Tupe valid and reliable data and source of information mkuu. Funguka zaidi tafadhali
 
Viwanda vya simenti kama 6 vipya vinakuja, ni lazima itashuka, lakini si ile ya Slaa.
Sure. System at work. Maana hata comment yako ni ya matumaini zaidi, kutia ari zaidi na nguvu zaidi za kusubiria ndoto hizi
 
Hiyo saruji naona ni ile ya"re-bag" ambayo haina nguvu na ubora;na nondo ni zile zinazoumuliwa kutokana na chuma chakavu ambazo zimetumika sana kwenye majumba ya ghorofa Dsm ambayo yanaporomoka kila wakati!
 
Wakuu msibishe kila kitu. Ni kweli bei imeshuka ila Ameanza na Msoga kwanza
 
Magamba its time you go now, hata mkishusha mfuko wa cement ukawa shs 10, hatudanganyiki wezi wakubwa nyie

aisee kiboko, hata shs 10 hamtaki... lakini kweli bana, hawa jamaa wanazuga tu, mkishawachagua ngoma inapanda twice.
 
Back
Top Bottom