- Source #1
- View Source #1
Ikiwa ni siku chache tangu chombo cha habari cha kimataifa cha BBC News kuchapisha makala iliyomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, zimeendelea kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa kauli ya kutaka BBC Swahili ifungiwe kufanya kazi nchini Tanzania.
Chapisho hilo, ambalo limesambazwa kupitia Facebook, linaambatana na nukuu isemayo:
"Baada ya BBC Swahili kuchapisha video yenye habari ya Tundu Lissu kuhoji demokrasia ya Tanzania, Kikwete atoa tamko kuu kwa TCRA kuifungia BBC Swahili."
Hata hivyo, uchunguzi wa taarifa mbalimbali za umma, ikiwemo hotuba, mahojiano na taarifa rasmi zilizochapishwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, haukubaini ushahidi wowote unaoonyesha kuwa amewahi kutoa kauli ya hadharani akitaka BBC Swahili ifungiwe kufanya kazi nchini Tanzania.
Aidha, chapisho hilo limetumia mbinu ya clickbait kwa kuandika kichwa cha habari kinacholenga kuwavutia wasomaji kubofya kiungo hicho kwa madai yasiyothibitishwa, bila kutoa ushahidi wa madai yanayowasilishwa.
Wakati huo huo, kabla ya chapisho hilo kusambaa, Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ilikuwa tayari imetoa tamko kupitia mitandao yake ya kijamii ikiikosoa BBC kwa kile ilichodai ni kushindwa kuzingatia misingi ya uwiano na usawa katika kuripoti makala iliyomhusu Tundu Lissu, ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashitaka ya uhaini nchini Tanzania.
Hata hivyo, tamko hilo la Serikali halikumhusisha Rais mstaafu Jakaya Kikwete, wala halikuonyesha kuwa yeye ametoa wito wa kuifungia BBC Swahili.