Niliyoyaona kwenye TV siku hiyo:
1) Rais hajausoma waraka wa katoliki. Waraka ule hakuna unapozungumzia wakatoliki au wakristu kuwachagua wakristu; unachoeleza ni wananchi kuchagua watu watakaojali vipaumbele vya taifa, wasio mafisadi. Watu wanahitaji elimu ili waweze kuchagua viongozi wazuri, hivyo waraka unazungumza juu ya elimu ya katiba. Ebu niulize swali rahisi. Viongozi wetu tukishawachagua wanaapa kuilinda katiba ya nchi - je ni wananchi wangapi wanayo hiyo katiba? Ni wananchi wangapi wanajua katiba inasema nini? Sasa waraka ukizungumzia suala la elimu ya katiba kwa wananchi kuna kosa gani.
Shame on you JK, ulipaswa kusema kipengele so and so ni kibaya kwa sababu fulani. No research, no data, no right to speak. JK aliongelea kitu asichokijua na kuishia kuwatishia wananchi kuwa nchi itagawanyika kidini. Tunachomwambia - nchi imeshagawanyika kati ya mafisadi na wanaopinga ufisadi.
2)Ni aibu kushindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi iliyokuingiza madarakani na kuleta kisingizio cha eti hukushiriki kuiandaa. Sasa ulipokuwa unasimama majukwaani unainadi, na kusema ni nzuri na kuahidi kuitekeleza ulikuwa mwendawazimu (kutoelewa ulichokuwa unafanya)?
30 Bado JK anaendele na mkakati wa kumtakasa Lowassa katika suala la Richmond. Alichosema JK ni kwamba baada ya bunge kujadili ripoti ya kamati ya Mwakyembe na kuiagiza serikali ichukue hatua, bado serikali ililirudisha suala hilo Takukuru ambayo imerudi na majibu yake yale yale kuwa hakukuwapo rushwa. Je ni kwa nini suala hilo lilirudishwa Takukuru wakati Hosea naye alitakiwa achukuliwe hatua kwa kumdanganya rais? Hivi serikali ilitegemea majibu gani toka Takukuru?
Mpira upo kwako Mwakyembe: Wakati fulani kuna watu walitaka kumtakasa Lowassa bungeni na wewe ukasema kama mkileta mambo hayo basi tutafunua hata yale tuliyoamua tusiyaseme ili kuinusuru serikali. Tunaomba sasa uyaweke wazi maana serikali hiyo uliyoamua kuilinda inataka kukuangamiza! wawahi kabla hawajakuwahi!
4) Kuhusu suala la Zombe, tumuombe JK atoe ushahidi mahakamani, maana anakiri kuwa Zombe alimwambia TUmeua majambazi, yaani yeye Zombe na wenzake, na baadae ikaonekana kuwa wale hawakuwa majambazi! HATUHITAJI USHAHIDI ZAIDI YA HUO!
5) Mwisho ni usanii aliouonyesha wa kuchekacheka wakati nchi imeshaelekea kubaya.JK Hajui sababu ya watu kutaka kumuona kwenye TV. Sababu kubwa si kutaka kusikia tu bali ni kuona pia body language. Huwezi kusema sina urafiki katika vita vya ufisadi huku unachekacheka. The body language lazima ionyeshe seriousness ya unaloliongelea. Kusemasema eti hili mimi halinisumbui! wakati wananchi ndio wamekuuliza! ulitaka kuonyesha nini? kwamba wananchi wako ni mazoba? Hivi huyo aliyekuuliza swali ambalo kwake ni kero wewe unamjibu kuwa kero hiyo haikusumbui, atakuelewaje?