Kikwete awasha moto...

Kikwete awasha moto...

Does this man really deserves a second term?

is this a question or an answer??

“Our lives begin to end the day we become silent about things that matter”
Ndio swali inapaswa tujiulize wewe na mimi na Mamilioni ya Watanzania
 
Niliyoyaona kwenye TV siku hiyo:
1) Rais hajausoma waraka wa katoliki. Waraka ule hakuna unapozungumzia wakatoliki au wakristu kuwachagua wakristu; unachoeleza ni wananchi kuchagua watu watakaojali vipaumbele vya taifa, wasio mafisadi. Watu wanahitaji elimu ili waweze kuchagua viongozi wazuri, hivyo waraka unazungumza juu ya elimu ya katiba. Ebu niulize swali rahisi. Viongozi wetu tukishawachagua wanaapa kuilinda katiba ya nchi - je ni wananchi wangapi wanayo hiyo katiba? Ni wananchi wangapi wanajua katiba inasema nini? Sasa waraka ukizungumzia suala la elimu ya katiba kwa wananchi kuna kosa gani.
Shame on you JK, ulipaswa kusema kipengele so and so ni kibaya kwa sababu fulani. No research, no data, no right to speak. JK aliongelea kitu asichokijua na kuishia kuwatishia wananchi kuwa nchi itagawanyika kidini. Tunachomwambia - nchi imeshagawanyika kati ya mafisadi na wanaopinga ufisadi.

2)Ni aibu kushindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi iliyokuingiza madarakani na kuleta kisingizio cha eti hukushiriki kuiandaa. Sasa ulipokuwa unasimama majukwaani unainadi, na kusema ni nzuri na kuahidi kuitekeleza ulikuwa mwendawazimu (kutoelewa ulichokuwa unafanya)?

30 Bado JK anaendele na mkakati wa kumtakasa Lowassa katika suala la Richmond. Alichosema JK ni kwamba baada ya bunge kujadili ripoti ya kamati ya Mwakyembe na kuiagiza serikali ichukue hatua, bado serikali ililirudisha suala hilo Takukuru ambayo imerudi na majibu yake yale yale kuwa hakukuwapo rushwa. Je ni kwa nini suala hilo lilirudishwa Takukuru wakati Hosea naye alitakiwa achukuliwe hatua kwa kumdanganya rais? Hivi serikali ilitegemea majibu gani toka Takukuru?
Mpira upo kwako Mwakyembe: Wakati fulani kuna watu walitaka kumtakasa Lowassa bungeni na wewe ukasema kama mkileta mambo hayo basi tutafunua hata yale tuliyoamua tusiyaseme ili kuinusuru serikali. Tunaomba sasa uyaweke wazi maana serikali hiyo uliyoamua kuilinda inataka kukuangamiza! wawahi kabla hawajakuwahi!

4) Kuhusu suala la Zombe, tumuombe JK atoe ushahidi mahakamani, maana anakiri kuwa Zombe alimwambia TUmeua majambazi, yaani yeye Zombe na wenzake, na baadae ikaonekana kuwa wale hawakuwa majambazi! HATUHITAJI USHAHIDI ZAIDI YA HUO!

5) Mwisho ni usanii aliouonyesha wa kuchekacheka wakati nchi imeshaelekea kubaya.JK Hajui sababu ya watu kutaka kumuona kwenye TV. Sababu kubwa si kutaka kusikia tu bali ni kuona pia body language. Huwezi kusema sina urafiki katika vita vya ufisadi huku unachekacheka. The body language lazima ionyeshe seriousness ya unaloliongelea. Kusemasema eti hili mimi halinisumbui! wakati wananchi ndio wamekuuliza! ulitaka kuonyesha nini? kwamba wananchi wako ni mazoba? Hivi huyo aliyekuuliza swali ambalo kwake ni kero wewe unamjibu kuwa kero hiyo haikusumbui, atakuelewaje?
 
Nakubaliana na wewe kwa kila kitu maana niliona kuwa hajajibu hoja ya msingi
 
Sijui kama tye rais ambaye ni kiongozi. Nafikiri tuna rais ambaye anpelekwa na upepo unakovuma. Wapi has alipotaka kutupeleka kwa hii miaka mitano aliyonadiwa kuwa chaguo la Mungu? Hata masheikh waliompigia chapuo hii leo wanamkana na kuahidi kutompa kura mwakani.
 
Anancha mambo yaende kama yalivyo, na pia kwa kuwa katiba yetu sio Imara ya kuhimili mikikiki hii yote na ndio maana kuna Vacuum katika uongozi wa Taifa hili
 
binafsi sijaona kama kuna jibu lolote lililototela zaidi ya kutoa melezo tu ya jumla kitu ambacho ni kawaida kwa huyu mheshimiwa sana,maswali yaliyo ulizwa ni ya muda mwingi na yamekuwa yaliulizwa na kuchambuliwa na kutolewa ushauri kupitia vyombo mbalimbali vya habari wana jf ni mashahidi.ALICHOKIFANYA NI KUTAFUTA UPYA POPULARITY ILIYOPOTEA KITU AMBACHO HAKIWEZEKANA KWA MAELEZO MEPESI ALIYOYATOA.
 
Mimi nilitazama luninga hapa kijijini kwetu na kumwona rais wagu akijibu maswali. Mimi kama wewe nilimwelewa kwa upeo wa uelewa wangu lakini karibu wote tuliondoka nakukubaliana kuwa

1 Pinda nihodari zaidi kujibu maswali kama anavyoonekana kwenye bunge kumzidi.
2 Alitoa majibu marefu mno ya kuzunguka, tena hiyo ilizua hisia mpya ya mapungufu na maswali mengi zaidi. Tido alishiriki hisia zetu hizi pia.
3. Alijibu swala la uhuru wa maoni kwa ufasaha kuliko mengine yote.
4. Tuliona kuwa hakuwa nadhamira ya dhati kuutokomeza ufisadi wala kuwaachia maswahiba wake waliohusika wapimwe kisheria.
5. Alionyesha upungufu mkubwa wa serikali kushughulikia masuala yake na kuilaumu mahakama kama ndiyo sababu.
6. Anamtazamo wa uchaguzi ujao.
7. Mara nyingi ni kama myofu kidogo
Pamoja na hayo na mengine mengi tulijiuliza kama nia na lengo au matarajio ya kipindi hicho kilifikiwa na kwa kiasi gani? Je nini kiasi cha kukubalika kwake kabla na baada ya kipindi hicho yakoje?

Tunatamani kumsikiliza tena na kumwomba ajibu maswali mengi zaidi.
 
In the interim kitu cha kufanya kuikomboa nchi hii kutoka kwa hawa madhalimu; kwanza kuhakikisha kuwa mgombea binafsi anaruhusiwa hata ikibidi kuweka inJunction ili uchaguzi uahirishwe, kuanzia huu wa serikali za mitaa mpaka hapo rufaa ya serikali itakapoamuliwa juu ya kuwa na independent candidates; PILI ELIMU YA URAIA KAMA ILIVYOAINISHWA NA WARAKA WA KANISA KATOLIKI USAMBAZWE KOTE VIJIJINI ILI WANANCHI WAWE NA INFORMED DECISIONS ZA HAO INAOWACHAGUA. CCM inatumia mbinu chafu za kuchelewesha uamuzi wa mahakama ili tusiwe na independent candidates kwenye uchaguzi wa 2010 na hii ni kuwanyima haki yao wananchi na mahala popote watu wanaponyimwa haki yao amani hutoweka.
 
Does this man really deserves a second term?

is this a question or an answer??

“Our lives begin to end the day we become silent about things that matter”
It is a statement. He does not deserve a second term, but he is there to stay nakwambia, hadi kipindi cha pili kipite. We created our own monster, we have to live with it! Tujipe pole!
 
kikwete hajawasha moto ila anasaidia kuzima moto uliowashwa dhidi ya mafisadi.........kazi tunayo
 
Nimefurahishwa na JK kama Rais pekee tangu nchi hii kupata uhuru wake anazungumza na watu wake live katika masuala ya nchi.nimefurahia sana hasa kwa kuwa yeye pekee katika maraisi wote ambaye ameamua kuwashughulikia mafisadi kwa dhati na tangu tupate uhuru hatujawahi kuona watu mashuhuri 30 wanafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za rushwa.
Linalofurahisha zaidi ni kuwepo na uhuru mkubwa wa kutoa maoni kituambcho hakikuwahi kuwapo huko nyuma.

Hebu linganisha uhuru wa kutoa maoni wakati wa mwalimu hadi wa Mkapa na awamu hii.
Kwa wale wanaomshutumu na waendelee tu,lakini watu wenye akili zao timau tunafahamu kuwa rekodi ya JK inatufikisha katika Taifa lililo tranparent kuliko mataifa mengi katika Afrika.
 
Hapa nipige kwanza hongera za dhati kabisa kwa Raisi wa tanzania kuweza kuwakabili wananchi kwa njia ya TBC na huu uwe ni mwanzo utakaoendelezwa, na si kwa yeye tu hata pia ikiwezekana kuweza kuwa na vipindi ambavyo Mawaziri wataweza kupatikana moja kwa moja kwa njia ya kutumia simu zao ,na zaidi pia kuweza kuwapata wakuu wa idara mbalimbali hivyohivyo kupitia simu zao ili kuweza kujibu kero za wananchi wa mitaani ni vipindi ambayo nimeweza kuvisikia katika baadhi ya nchi ,mkuu wa idara anapigiwa simu kujibu suali lilioulizwa na mwananchi direct kupitia redio ni live kabisa ,yaani hata wakuu wa polisi nao huweza kusigezwa na wananchi kwa kutumia njia hii nasema raisi ameonyesha mfano mzuri kabisa na wa kuigwa na kufuatwa na walio chini yake bila ya kukwepa au kuonyesha wanapopigiwa simu huwa simu zao hazipatikaniki.
Hii ya Kikwete ilikuwa ni special event kinachotakiwa sasa kiwepo kipindi cha kila siku ambacho kitajumuisha simu za wananchi na kuwahoji au kujibu masuala kwa viongozi wote waliotayari kuwajibika katika kuliongoza Taifa hili.
Natumai hata debate katika uchaguzi ujao ,CCM hawatakimbia.
 
Linalofurahisha zaidi ni kuwepo na uhuru mkubwa wa kutoa maoni kituambcho hakikuwahi kuwapo huko nyuma.

Hebu linganisha uhuru wa kutoa maoni wakati wa mwalimu hadi wa Mkapa na awamu hii.
Kwa wale wanaomshutumu na waendelee tu,lakini watu wenye akili zao timau tunafahamu kuwa rekodi ya JK inatufikisha katika Taifa lililo tranparent kuliko mataifa mengi katika Afrika.
wakati wa mwalimu kulikuwa hamna internet, tv za kuhesabika sio TZ tu bali world wide...
vitu unavyoviona leo havisababishwi na JK, BM, AM, hii inatokana na teknologia, na kikwete akitoka basi anayekuja itakuwa uhuru mkubwa zaidi...
ukifungia JF, watu wanaamia twitter/facebook
hata zimbambwe kuna uhuru, mugabe amezui kuna mshinda, iran kuna uhuru pamoja na kuzuia lakini wameshindwa
JK akizuia uhuru atakuwa anajipigilia msumari na yeye analijua hilo
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa mtu unaweza kutumia njia mbadala kwa ajili ya kuwasilisha mawazo mbadala na hivyo huwezi kuzuia jambo katika Dunia ya sasa, Hivyo Jk naye inampaswa afanye hivyo
 
JMK kajibu ipasavyo na mbona hamuyasemi mafanikio ya elimu? naye kayasema wazi wazi? ni nini zaidi ya elimu itakayowakomboa wa Tanzania? JMK kwa muda mfupi ameweza kuyafanya katika elimu ambayo hayajafanywa na Rais yeyote kabla yake. Jee, hili hamulioni?

JMK kaweza kuwafunguwa midomo mpaka leo mnaweza kuyasema mnayoyasema, thubutu, mgaliyasema hayo mnayosema wakati wa Nyerere! labda wengi wenu hamkuwepo, tuulizeni sisi tuliyoyaona. Kusingekuwa na waraka wa Mapadiri wala Masheikh. Leo Rais anayewawezesha kusema na kuwafungua midomo na vichwa vyenu mnamponda, ama kweli, mwenye mach haambiwi tazama!

Nyerere hata kura, zilikuwa ni ndio au hapana, yeye au ruhani! ukisema ndio, ndio yeye na ukisema hapana, ni hapana mwengine kuliko yeye! leo mna midomo ya kuchonga, chongeni na ndivyo JMK alivyowataka na kasema kinaga ubaga, kuwa tunataka mseme na mkisema mseme ya kweli yanayowakera naye anayashughulikia. Na kwa hilo ni kweli kabisa. Leo tunaona vigogo wako mahakamani wanajibu tuhuma mbali mbali, yalikuwepo hayo wakati wa Rais yupi?
 
Namuunga mkono Dr. Slaa (100%).

Actually mimi nilikata tamaa wakati ikijibu swali la waraka na kusema "...makamu wa Rais na Waziri Mkuu wapo safarini, nawasubiri wakirudi tutaenda kuongea na viongozi wa dini (eti) tuone tutafikia wapi kuhusu hili,....tupeni muda" Tido Mhando akamuuliza Rais muda unakwenda ....JK akajibu "...mbona uchaguzi wenyewe upo mwaka kesho"

Nimekata tamaa: nilikuwa nasikia tu kuwa huyu mtu ni "weak" - sasa nimeona kwa macho yangu. Rais asiyekuwa na maamuzi katika masuala ya wazi kabisa ni mchovu na hatari. We have a huge leardership vacuum in Tanganyika.

Kwa hiyo hapo anajionyesha objective yake ni election politics na sio ku solve the underlying divisive issues siyo?

Yani huyu jamaa bora akae kimya tu, akiongea ni pumba from A to Z.
 
Akili zingine bwana hata watu kuwaza hawawazi .
JK nakueleza na CCM yake wakiweza kuwaziba watanzania midomo kwa ajili ya CCM kuendelea kuwa madarakani wanaweza kabisa na wanatamani mno ila sema wanabanwa . JK anajikomba kwa wazungu kila siku na ataka kuendelea kujikomba hawezi kuthubutu kujaribu kubana lakini ni ndoto ya CCM kufanya yote kwa ajili ya CCM . Pemba hadi leo ni kitendawili . Elimu imekuwaje ? Yaani shule za kata ndiyo useme Elimu ? JK ana andaa Taifa la wajinga na wasio kuwa na exposure . Ndicho anacho taka lakini hili huwezi kuliona . Unasoma kijijini kwako secondaru kijiji cha jirani na jioni unarudi home na baada ya Form 4 umefeli ubakia kulima less headache kwa CCM wasiotaka kupingwa .

JK hakika sijaona alicho kifanya na nilitegemea asimamie issues nasi kuwapanga wana CCM kuuliza maswali ya Chama chao . Alikuwa pale kama Rais wa Tanzania na si kama mwenyekiti wa CCM .Ndiyo nasema vyama viache kuwapa vyeo vya siasa viongozi wakuu ili tujue kazi zao hasa .

Unampa sifa JK ambaye hata waraka hajui unasemaje na hajui anacho kipinga ? Alianza propaganda za udini nikajua yeye sawa na Kingunge hawajausoma waraka ama wanasoma ila hawaelewi maana neno tuendelee ufisadi kule hakuna kuna kupingana na ufisadi na dhuluma .
 
Kwanza inaonyesha huna data za elimu ilivyopanda za kutosha, wanafunzi wa vyuo vikuu wapenda kwa asili mia mia moja au zaidi kulinganisha na waliokuwepo mwaka 2005. Shule za Sekondari, wanafunzi walioanza form 1 ni zaidi ya wote waliokuwepo mwaka 2005 yaani zaidi ya waliokuwa form 1 mpaka 6, Shule za Sekondari kwa kipindi hicho hicho zimezidi kwa zaidi ya shule elfu 3 ambazo ni zaidi ya shule zote zilizokuwepo kuanzia tulipokabidhiwa nchi hii na Umoja wa Mataifa (tusijidanganye kuwa ulikuwa ukoloni), ukichanganya awamu zote zilizopita hawajajenga hata robo ya shule alizojenga JMK katika muda mfupi aliopo madarakani.

Jee, ni nani alieacha Taifa la wajinga?

Huo ufisadi unaousema, ni awamu gani unaongeleka na unachukuliwa hatua? hakuna jibu ila ni awamu hii ya JMK. Huo ufisadi ulianzia wapi? jibu unalo!

Sema usemayo, ukweli utabaki ukweli na takwimu ndio zenye kuthibitisha ukweli.
 
Huyu mheshimiwa ni wa kumflash out 2010 tu.

Kwanini kuwa na kiongozi wa jinsi hii ? Maneno mengi utendaji mdogo,omba omba wakati mali za nchi hii wanaziuza kinyemela kwa waarabu na kutuibia Rasilimali zetu..

Hakutoa majibu ya msingi zaidi ya kucheka cheka hovyo.
 
Upuuzi huo, mali gani iliyopewa waarabu? Ni swali lipi ambalo hajajibu?

Huna lako, kajibu vizuri na kwa ufasaha kabisa na yeye ndie Rais baada ya 2010, tutamchaguwa mkitaka msitake.
 
Back
Top Bottom