Elections 2010 Kikwete awateua Meghji na Nahodha ubunge


Matatizo ya EPA yalitokea mwishoni mwa mwaka 2005, aliyekuwa Waziri wa Fedha si Zakhia, ila ukaguzi wa Benki uliogundua upotevu wa EPA ulifanyika yeye akiwa Waziri wa Fedha na ni yeye aliyeajiri kampuni ya kuchunguza sasa anahusikaje? Matatizo ya kodi si uamuzi wa mtu mmoja hivyo huwezi mlaumu waziri wa fedha labda uilaumu serikali yote
 
Hii kwangu si habari wala cha kushangaza!! Ukweli ni kuwa JK anauwezo wa kufanya lolote na ukashangaa!!
 

Sasa huyu kumtoa kwenye taaluma ya ufundishaji na kumleta kwenye SIASA ni matumizi mazuri kweli ya Rasilimali watu?
 
Kama unapinga hayo yote, unaweza kutueleza kwa nini Kikwete aliona hafai baada ya EL kujiuzulu alipotaja baraza jipya la mawaziri alimuacha. Leo hii anaona Meghji anafaa!!!
Acha hizo, haya ni mambo yaleyale ya kuturudisha nyuma. Hatutakuwa na mawazo mapya ya kwenda mbele namna hii.
 
..I hope hatateua Wabunge, kama alivyofanya kwa Jussa,na Janet Mbene, kikiwa kimebakia kikao kimoja kabla Bunge halijavunjwa.
 
Nasikia JK anamtayarisha Zakia kuwa Waziri wa Utalii na Maliasili -- aliyokuwa nayo hapo zamani ambapo alifungulia milango kwa mafisadi kubaka mali asili za msituni.

Lakini JK na Zakia wajue -- hatujasahau kamwe ile Kashfa ya Kagoda ambayo Mama huyo 'alijikwaa' kidogo kwa kutoa tamko la kutaka kuficha ukweli -- baadaye akaja na barua ya kughushi ya kusema 'afanaleik!! kumbe nilipotoshwa na Katibu Mkuu wangu -- Mgonja' -- ambaye sasa ana kesi -- ingawa haihusiani na Kagoda.!!

Akimpa tu uwaziri -- tunaye mama huyu, hatumuachilii hadi ayabwage manyanga.
 

Mbona walioachwa ni wengi tuu - Antonny Diallo, Mramba, Mungai...wote hao walikomba EPA au kupandisha bei ya mafuta?
 
Mbona walioachwa ni wengi tuu - Antonny Diallo, Mramba, Mungai...wote hao walikomba EPA au kupandisha bei ya mafuta?

Unaboa wewe mtoto! Kwanini Zakhia asiende kupambana kwenye majimbo kila wakati anasubiria mbereko ya kuteuliwa? Amekuwa serikalini miaka mingi mno akiteuliwa katika nyadhifa mbali mbali. This is stiffly stinking. Nadhani unaelewa
 
Naombeni mnifahamishe, kwani JK na Zakia wana uhusiano gani?
 
Unaboa wewe mtoto! Kwanini Zakhia asiende kupambana kwenye majimbo kila wakati anasubiria mbereko ya kuteuliwa? this is stiffly stinking. Nadhani unaelewa

Tunalingana tuu kiumri na sura yako usiniite mtoto. Zakhia alijaribu Moshi hakuvuka kura za maoni kwenye Chama Chake na hata aliyemshinda Shemeji yake na Mkapa hakuweza kupeta kwa sababu kule Moshi maswala ya Beijing bado hayajafika na wala hayahitajiki ili kudumisha nidhamu katika jamii
 
Huu ni mwanzo wa kuwafahamu mawaziri wake wateule, ishu hapa ni kujua watapelekwa wizara gani, Mama mkwe wizara ya mali asili na Utalii.

mama mkwe kivipi? tujuze mkuu inawezekana wengine tupo nyuma ya wakati
 
Guys! hivi mnashangaa nini!?? mnakuwa kama hamumjui JK! kweli expect more to come! :bowl:
 
Rais has that prerogative power under the current constitution nan haina ubaya kabisa.

I have a feeling that Nahodha may come to constest for the presidency under CCM ticket come 2015.

Congrats to the wateule.
 

Kungekuwa na thermometer ya kupima kichefuchefu nimsikiapo huyu mama lazima watu wangenilazimisha nilazwe hospitali. Hivi Wa Tz milioni 40 hakuna mama wa kufanya kazi anazotaka Jk mpaka huyu ??? ahhhhkrrrr
 

Nangojea baraza la mawaziri litangazwe. Yawezekana kukawa na staili ile ya THREE MINISTRIES WITHOUT PORTFOLIO KAMA ZENJ.
 
JK na Uozo wake wa siku zote!!
Hoyo mama since 1980s yupo serikalini, amekuwa Waziri miaka mingi...sijui Afya, Maliasili, Fedha n.k, hana jipya na wala hakuwa na utendaji mzuri kama watu wanavyodhani! Ni kwamba jamaa ameishiwa, anaogopa kuteua mawaziri wapya kutoka miongoni mwa wabunge wake....anataka kurejesha walewale waliowahi kushika nyadhifa kadhaa..kwa ku-shake kidogo tu majina na Wizara husika....!! Mwaka huu, na miaka mitano inyokuja TUTAONA MADUDU AMBAYO HAYAJAWAHI KUTOKEA TANGU NCHI IPATE UHURU
 
Jamani sitaki niongelee kuwa walioteuliwa hawa watatu hawafai au laa,ila kitu kimoja wana jf tusaidiane ni how Shamsi Nahodha atatumikia bunge la muungangano na zanzibar, wakati mwingine session zinakuwa kipindi kimoja now kutumikia mabwana hawa wawili itakuwaje? Nawakilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…