Elections 2010 Kikwete awateua Meghji na Nahodha ubunge

Jamani, mwashangaa nini? Meghji ni "mama mkwe" wake JK? Au MUMESAHAU?
 

KIPIPILI, kama mtu unauhakika wa kuteuliwa na kupewa uwaziri kwa nini ukachakae na kampeni?
 
Mi wacha ninyamaze tyu manake huyu mkwere anavyonipa hasira nisije nikala ban bureee, yaani Meghji tenaaaa ananuka kashfa za ubadhilifu ila kona?????!!!!!!!!!! Inauma sanaaaaaaaaaaaa mjombaaaa
 
Kwa uhakika Prof. Makame Mnyaa Mbarawa atakua Waziri maana ana uwezo na aliletwa nchini na Dr. Bilali na Bilali sasa ni Makamu wa Rais na alipelekwa jimbo la Mkanyageni la Dr Shein na alisaidiwa sana ashinde akakwama kwa kura chache sana
 
Weraaaaa weraaaaaa mama mkwe! Acha kodi za watanzania zilipe mahali!
 

Kwa mtajii huu ni kweli hakuna maendeleo!
 

"Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni!" Mwl. J. K. Nyerere
 
We are not supposed to keep quite on this!huyu jamaa ni mdini mno,nilikua sikubali nilipokua nikisikia kuhusu hili.Now nimeamini na nahisi atatuletea matatizo baadae
 
Kikwete kumrudisha huyu mama licha ya kuondoka kwa kashfa je anadhani wananchi ni wajinga wenziye? Au ndo tujiandae kwa ujio wa karamagi na akina lowasa kwenye uwaziri?
 
Ni juzi juzi tu, Dr. Slaa alikuwa anawaambia Watanzania kuwa kuchagua ccm ni maafa. Usemi huo unaanza kuwa kweli. Tusubiri mengi tu yajayo!
 
Hapa ni kuwa anamwandaa kuwa waziri na pia Nahodha anaweza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje nyie subirini tu yangu macho
 
Nahodha si mjumbe wa baraza la wawakilishi zanzibar? kama ni hivyo, atawezaje kuhudhuria vikao vyote viwili? Naomba mwenye ukweli wa hili atujuze

Jambo muhimu hapa la kuangalia ni muingiliano wa kazi,huyu Bwana Shamsha Nahodha ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Jimbo la Mwanakwerekwe (Unguja),hichi kitendo cha Rais kumteua Ubunge wa Bunge la Jamhuri si kuwanyima haki yao wananchi wa Jimbo hilo?Ni wazi kuwa Shamsha na Prof.Makame wana nafasi ya Uwaziri ktk Baraza jipya atakalolitangaza Ijumaa,fununu hizi zimekuwa wazi na hata ndio sababu ya Shamsha Vuai kutopewa nafasi ya Uwaziri Zanzibar,kwa sababu ilisemwa kuwa Rais anamuandalia kazi yenye majukumu makubwa kuliko Uwaziri ktk Serikali ya Mapinduzi.Prof.Makame bado ni mwalimu katika Chuo kimoja huko S/A lakini alikuja Tanzania mapema na kugombea Ubunge kwa kupitia Jimbo la Mkanyageni,huko alishindwa na Mtu wa CUF,sasa Rais amemteua ni wazi kuwa anaandaliwa nafasi ya Uwaziri na pengine ni Madini au Mambo yanayohusu rasilimali za bahari.
Linalotisha ni kwamba nafasi hizi zote Tatu ni kutoka Tanzania Visiwani,na bado kuna Mawaziri wazamani wawili wenye asili ya Zanzibar wanatajwa ktk Baraza lake jipya.....Jambo hili linaonekana linafanywa makusudi kuwafurahisha Wazanzibar ambao wanaonekana hawautaki Muungano,kuna nini hapa?Tungoje kutangazwa kwa Baraza la Mawaziri ili tuone kuna agenda gani kati Watawala wetu na suala zima la Zanzibar na Muungano!
 
Utabiri: Watakaofuata ni Mangunga, Masha, Marmo, Buriani. Yaani baadhi ya waliopigwa chini watarudi mjengoni kwa staili hii. Si mnajua wadau; Shem batilda hawezi kuachwa labda kama alilikoroga mahali. That's my prediction! We just have to wait and see! hah.
 
huyu ni rais msanii namba mbili katika historia ya nchi hii, akitanguliwa na mzee ruksa aliyekuwa na waziri asiye na wizara maalum. no positive expectations in his regime!:A S angry:
 
Hii ni Ze Comedy yaani Churaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, chura mwenyewe.



Shemejiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,
 
Nikisikia habari kama hizi napata simanzi moyoni.
Huyu mkwere naona hana uchungu kabisa na hii nchi, kama mwanae tu kwa kipindi hiki alichomaliza na kudakia kingine amesha kuwa fisadi wa kutupwa na bado mama mkwe anavurunda kwenye wizara nyeti kama ya FEDHA hapo tutarajie nini kama atamuweka kwenye wizara tena?


Wenye imani zetu tuna matumaini kuwa Mungu yupo atatusimamia. YANA MWISHO HAYA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…