Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto)
mara baada ya kutua kijiji cha Mawengi Ludewa kufungua mradi wa umeme
RAIS KIKWETE APONGEZA KANISA KWA MRADI WA UMEME ,ATAKA WANANCHI KULIPA BILI KWA WAKATI
RAIS Jakaya Kikwete amelipongeza kanisa la Romani Katoliki jimbo la Njombekwa kusaidia serikali kutatua tatizo la umeme kwa wakazi wa kijiji cha Mawengiwilaya ya Ludewa huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza nyanzo vya maji ilikuwezesha maradi huo wa umeme wa gharana nafuu kwa wananchi kuendeleakusambazwa zaidi katika vijiji vingine vya wilaya ya Ludewa kwa msaada wa kankisa hilo.Akiwahutibia wananchi wa kata ya Mawengi mara baada ya kuzindua mradi wa umeme wa Lumama Electrical Asosoation jana ,Rais Kikwete alisema kuwa hatari ya maradi huu kufa itasababishwa na wananchi wenyewe wa kata hiyo iwapohawatatunza vyanzo vya maji na kusababisha mradi huo ambao unategemea zaidi maji ili kuendeshwa kushindwa kufanya kazi kwa uhakika .
"Waswahili wanasema hivi kitunze kidumu ,kitunze kikutunze ….sasa nawapongeza mmeanzisha chombo chenu cha kusimamia mradi Lumama …..sasa nawaombeni Lumama iendelee kusitawi ili kuhakikisha mazingirahayaharibiwi na maji yanaendelea kuwepo kwani kama vyanzo vya maji vitaharibiwabasi mradi utakufa….pamoja na kuwa maji haya ni neema ya Mungu ila Mungu ametua maarifa ya kuvitawala vyanzo hivyo ili vidumu zaidi kwa kutumia kanunizinazotawala mazingira ili yaendelee kuwepo" Hivyo aliwataka wananchi kupitia umoja wao wa Lumama kuhakikisha wanatunzavyanzo vya maji kwa kutoharibu ovyo mazingira , kuchangamkia fursa hiyo kwakuingiza umeme katika nyumba zao huku akiwakumbusha kulipa bili kwa wakati . Aidha alisema kuwa serikali kupitia shirika lake la huduma ya umeme vijijiniitaendelea kusaidia mradi huo ili uweze kusonga mbele zaidi na kuwanufaishawananchi wengi .
Rais Kikwete pia aliwahakikishia wananchi na wahisani hao kuwa serikaliimeendelea kutoa mchango wake katika mradi huo na itaendelea kuaunga mkonojitihada za kanisa hilo na wahisani wake kwa kusaidia fedha zaidi kwa awamu ya pili ili kuwezesha mradi huo kujitanua zaidi. Alisema kuwa hadi sasa makao makuu ya wilaya ya Ludewa kuna umeme wa Genereta ila bado mkakati wa serikali ni kuiunganisha wilaya hiyo ya Ludewa na umeme wa uhakika wa Gridi ya Taifa ambapo kazi hiyo kubwa mchakato wakeunaandaliwa. Pia alisema kuwa mkakati mwingine wa serikali ni kupeleka umeme wa gridi yaTaifa wenye uwezo wa KW 232 kutoka Makambako wilaya ya Njombe kuelekeaSongea mkoni Ruvuma na kuwa umeme huo utapoonza madaba ili kufikia KW 11na baada ya hapo wananchi wa vijiji vya Ndolela ,Mkongobaki, Shauri moyo ,Mavanga , Mndindi ,Lugarawa ,Mbwila,Mkiu ,Mlangali na Luana . Alisema kuwa wananchi wa kata hiyo ya Mawengi mbali ya kuwa na mradi huo wa umeme wa Lumama bado serikali ipo katika mchakato wa kupitisha umeme wa gridi ya Taifa utakaotokea katika kituo cha Madaba na kupitishwa katika maeneo yao kwenda makao makuu ya wilaya.
Rais Kikwete kabla ya kufika katika kijiji hicho alizuiwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali kata ya Mlangali ambao waliziba barabara na kulazimika kusimama kuwasikiliza na kujibu madai yao mbali mbali likiwemo na kuchelewa kufika kwa gari la wagonjwa ambao alipata kuwaahidi wakati wa kampeni ,tatizo la soko la Mahindi kusimama na kero ya maji ambapo aliwahakikishia kuwa malalamiko hayo yatafanyiwa kazi na majibu ya madai yao atampa mbunge wao Deo Filikunjombe iliawafikishie. "kwanza niwashukuru sana wananchi wa Ludewa kwa kukichagua chama cha mapinduzi (CCM) na kumpitisha mbunge wenu Deo Filikunjombe bila kupingwa ….sasa nawahakikishieni madai yenu yatafanyiwa kazi na kuhusu soko la mahindi wiki ijaya fedha za kununua mahindi zitakuja hapa"
Kuhusu liganga na Mchuchuma Ludewa ,Rais Kikwete alisema kuwa sasa umefikawakati wa kuanza kutekeleza mradi huo kwa kampuni kutoka nchi ya China ambaokuanzia wiki ijayo wawekezaji hao watafika na kuanza kutekeleza mradi huo na ajira 8000 hivyo kuwataka vijana kuacha kuhoji juu ya maisha bora na badala yake kwenda kuomba kazi . Hata hivyo alisema barabara ya lami ya uhakika na Reli kwa ajili ya kupitisha makaa ya mawe na chuma kutoka wilaya ya Ludewa na kwenda kuyauza nchi za nje mkakati wake kuanza kuandaliwa . Alisema kuwa kila jambo lina wakati wake na kuwa sasa ni zamu ya wilaya ya Ludewa kubadilika kimaendeleo .
Awali mbunge wa jimbo hilo la Ludewa alimweleza Rais Kikwete kuwa pamoja naTaifa linasherekea miaka 50 ya Uhuru ila wakazi wa wilaya ya Ludewa wao baada ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika mwaka huu chini ya utawala wa RaisKikweye ndio wanapata uhuru wao baada ya kuwa na uhakika wa barabara ya lami na kuanza kuchimbwa kwa mradi wa Lingana na mchuchuma.
Kwa upande wake meneja wa mradi wa umeme wa Lumama Alice Michelazziakisoma taarifa ya mradi huo mbele ya Rais Kikwete alisema kuwa mradi huo ulianza toka mwaka 1998 kwa kufanyiwa utafiti uliogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 8.900. Hata hivyo alisema kuwa shughuli za mradi kwa sasa ni kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha KW 150 ambao tayari umekamilika mwaka 2010 nakuwa kanisa Katoliki jimbo la Njombe linatekeleza mradi huo kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ACRA.
Aliwataja wahisani wengine kuwa ni wizara ya mambo ya nje ya Italia,mkoa wa Lombaridia-Ilaty,Itervita,Foranzione Cariplo na umoja wa nchi za Ulaya