Elections 2010 Kikwete: Bila safari za nje tungekufa njaa

kwani lazima uende kuomba..wakati pesa zetu zinaliwa ...! kodi zetu zinafanya kazi gani..? kununua mashangingi tu sio..?

unatumia mabillion ya safari kwenda kuomba million 70 za vyandarua..???
 
Our Preident is depended mind person; kwa yeye ili kuondokana na tatizo lazima aombe misaada, haoni fursa zilizoko nchini mwake ambazo zinawanufaisha hao ambao anawategemea kwa misaada.

Fursa kibao nchini mpaka Balozi wa Ujerumani haelewi kwa nini TZ umaskini kibao (The Guardian, 1/10/2010)
 

Kumbe akiwa hajasafiri au ikulu kazi yake ni kumtazama tu Salma na malavi davi kwa kwenda mbele!
 

JK hivi bila wewe kwenda nje ya nchi hatupati misaada? Mbona misaada imeanza toka awamu ya kwanza lakini walikuwa hawasafiri kama wewe? Balozi wako wa Japan kazi yake nini? Balozi wa Japan nchini kazi yake ni nini? JICA inafanya nini nchini? Au una maanisha kulala nja wewe na familia yako, na ndio maana suala la Urais ni la kifamilia!?
 
Namshauli raisi kikwete ateue washauli wazuri na awasikilize labda itasaidia!

Tatizo lililopo ni kwamba yeye anajua kila kitu, hivyo hata ukimlundikia washauri watakula tu mishahara maana watamshauri na asifanyie kazi
 
,,,,emancipate your self from mental slavery, non but ourselves can free our minds,,,,
 
misaada,misaada,misaada.chandarua kitu gani ndani ya nchi ya maziwa na asali?kikwete kama unataka nikuhrshimu naomba ukae pembeni ili uwapishe wanaojua tz inahitaji nini? na umasikini wa nchi hii umetokana na nini?
hao unaokwenda kuomba msaada wao wana nini na sisi tuna nini? nakuomba sana wapambe wako wote waliokuzunguka ni mwatajiri wanaoweza hata kuingia kwenye jarida la fobes.leo unatuambia umepewa milioni 78 na tajiri wa usa/ naomba ulinganishe huyo aliyekupa hizo hela na rostam aziz ndipo utajua tuna matajiri walioifilisi hii nchi wangapi? na ukome kutudhalilisha miakahii sio ya kuomba msaada. hata sijui kwa nini serikali yako ilimhamisha matonya pale dar naomba arudishwe haraka kabla familia yake haijafa njaa kwa kuwa ndiyo sera yako.kila siku nasema hatuna rais watu wanabisha. mwaka huu ni mwaka wa kutafuta rais na yupo tayari kuwatumikia watu.kura yako tu kwa dr.
 
Huyu jamaa msanii kweli.

(halafu huwa anaangalia na hadhira wanaomsikiliza kwenye mikutano yake. mbona hakuyasema hayo alipokuwa Moshi?).
 
Mie hata unipe nini kamwe siwezi kumpa kura yangu kiongozi wa namna hii. KAMWE NO!
 
"Kuna wakati nilikwenda Marekani nikakutana na rafiki yangu akasema wewe kwako si unatatizo la malaria, nikamweleza ndiyo akasema atanikutanisha na mtu atakayenisaidi na kumaliza tatizo ... kweli akanikutanisha naye na akanunua vyandarua vyenye thamani ya Dola milioni 78," alisema.

" DOLA MILIONI 78 (kama shilingi bilioni 113) KWA AJILI YA KUNUNULIA VYANDARUA?????" hii naona haijakaa sawa, Watanzania wanahitaji hivyo vyandarua kweli?, tatizo la malaria litamalizwa kwa kununua vyandarua ama kuondoa mazalia ya mbu?, napata shida juu ya uwezo wa Rais wetu kutambua matatizo ya wananchi wake na njia sahihi za kuyatatua.
 
Ndo maana balozi wa Ujerumani kasema hajui kwanini Tanzania ni masikini. Sasa Rais anaacha resources zote zimejaa hapa ambazo anaweza kuziexploit effectively kwa maslahi ya nchi anakwenda kukaa mahali na kuomba? Sijui na hao washauri wake ni akina nani?

SOURCE: THE GUARDIAN
 
Mbona hasemi mikataba mibovu aliyoingia huko? Kweli hapa kazi ipo tumpe urais 2010 wallahi tutalia maana atakwangua kila kitu kwa akili hii!!!
 
Hivi ni kwli CCM imetumia miaka 50 kum-groom huyu bwana ili aje awe Rais wetu!!! Pamaoja na kukulia kwenye chama bado anataka kutwambia kuwa hajui CCM ni cha cha UJAMAA na KUJITEGEMEA. Sasa kama leo ansema bila safari zake za nje tungekufa na njaa, hii haiingii akilini kabisa unless anjaribu kujustify safari zake za miaka mitano ijayo. Halafu watu kama akina maggid bado wanakuja na propaganda zao kuwa huyu ndiye.....Labda Maggid kijijini kwao angekufa na njaa bila safari za nje za Mkulu.
 
Haingii akilini kujisifu kwenda kuomba msaada hivi kwa nini tusaidiwe na tusifanye wenyewe mbona hapo nyuma kama ulivyosema mkuu mwalimu alikuwa anakaa hapa hapa na tulifanya makubwa sasa hili la kujisifu kuomba kweli lina walakini.

Mwalimu alisha wahi kusema kuwa kwenda kuomba misaada sio ndio itakuletea maendeleo ni jinsi wewe unavyojipanga na wananchi wako hapa nchi kwa kufanya kazi na kuleta maendeleo kwa wananchi wako nadhani JK anasahau hata husia wa Baba wa Taifa,

Na hao wasaidizi wake walioko IKULU ni Zero kabisa wamepafanya IKULU eneo la walanguzi hawtufai hao hata kidogo kabisa.

Kuna sehemu mwandishi ameandika ati JK amesema akae IKULU amwangalia mama salma teh teh Ivi kama Rais unatamka maneno kama hayo, kwani sie tulikuweka hapo ikulu kumwangalia mama salma? eeebooh sisi tulikupa dhamana ya kutuongoza kwa dhati na kwa dhamira zetu wewe unatujibu upuuzi jamani khaaa au iyo President Immunity ndio inampumbaza jamani? Kama Rais hapo IKULU ni umeenda kututumikia na sio kisingizio cha kwenda Ulaya kuomba misaaada ati ndio sie tuendeleee si shanga JK kushindwa kujibu swali aliloulizwa huko nje kuwa nchi ina utajiri wa kila aina iweje iwe maskini na akakosa jibu hapo sie twahitaji ubunifu wa kujikwamua kutoka katika hii hali ya umaskini na kwenda stage mpya ya maendeleo kutengeneza mikakati ya maendeleo na sio mikakati ya kuwazia kuiba kura CCM ishinde. ndio haya pia huyu balozi wa Germany nae nastahajabishwa
1st October 2010

"There are a lot of opportunities Tanzania could have seized and gone very far ahead economically, but I do not have the answer as to why it is this way, though the situation is better now than it was in the past," he said.Germany`s Ambassador to Tanzania, Guido Hertz

 

Lakini pia Wahariri wa vyombo vya habari wawe makini wanapoandaa habari. Wapime maudhui ya habari yenyewe na itapokelewaje na Watanzania. Ni aibu kubwa habari inayosifia "Umatonya wa Mkuu wa nchi" kufanywa Habari Kuu.
 


Nadhani hafahamu kwanini yuko/alikuwa IKULU! Asirudi tens huyu!
 
Mheshimiwa alisha sema Hajui kwa nini Tanzania ni masikini?
Vipaumbele vyake ni kuendekeza UMATONYA apate VYANDARUA, Kuleta Wajapani wuze SURA Kaliua.
hakuna Kipaumbele cha kuweka uchumi imara na endelevu kwa Watanzania wote
 
"Ninapokwenda nje nakwenda kwa malengo. Siende tu. Siwezi kukaa Ikulu jijini Dar es Salaam, kuangalia uzuri wa mke wangu Salma … hapana lazima nikutane na watu huko huko waliko," alisema JK ."

Hi ni kauli ya kejeli na dharau kwa wananchi waliompa jukumu la kuwatumikia. Kama tungetaka amuangalie mkewe si tungempeleka BBA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…