Kikwete frustrated at the UN?

Kikwete frustrated at the UN?

1.
jokaKuu said:
..on paper, Kikwete is supposed to be the most competent and succesful president we have ever had

2.
Kuhani said:
Sasa utasemaje "on paper Kikwete is the most experienced and successful" ?

3.
Kuhani said:
On paper Kikwete ame succeed nini ? Nitajie alicho succeed Kikwete "on paper" ?

Kuhani,

..umenionea. unaniuliza kitu ambacho sijakisema.

..ofisa wa jwtz, mtumishi wa chama wa muda mrefu, waziri wa nishati,waziri wa fedha,waziri wa mambo ya nje for 10yrs.

..10 yrs as the President in waiting.

..ndiyo maana nasema Kikwete alipaswa awe most competent, and most succesful, kuliko hao waliomtangulia.
 
Matatizo ya Speech za Rais hayakuanza leo...Mwaka jana licha ya kuchelewa kwenye kikao cha UN pia alitoa Speech Nyepesi kupindukia..Hii Speech ya Juzi ilizungumzia mambo mengi,kilichotokea ni kubabaika na lafudhi ya kiswahili katika maneno ya kiingereza,Kuzungumza mambo mengi juu juu kwa wakati (muda) mdogo (dk 45).

Hotuba inayotolewa UN inatakiwa iwe nzito na inayofanana na Hadhi ya hapo mahali,[/U]Hiyo sio Hotuba yakuomba kura kule Tarime,au Hotuba ya Ufunguzi wa Daraja huko Songea,Hotuba hizi ndio zina hadhi ya akina Januari,lakini sio Hotuba zinazotolewa kwa watu waliobobea kwenye siasa Nzito.......zinataka watu waliopevuka kwenye Diplomasia na uwezo wa Lugha nyepesi ya kistaarabu na inayoeleweka.

Kwa Mtazamo wangu naona kuwa kuna matatizo makubwa katika Kitengo cha Mwasiliano Ofisi ya Rais.Ama kwa makusudi wanamfanya Mh.Rais Mpuuzi ama watu hawa hawajui vizuri kazi zao.Haiingii akilini kusikia kuwa Januari Makamba ndio yupo kwenye list ya Waandaaji Hotuba za Rais,sina uhakika kama kijana huyu alimaliza shule yake,kwa sabau alikwenda State House kwenye Intern tu,na sio kama ndio ilikuwa ajira.Kuna Magwiji wa uandishi wa Hotuba kama Balozi Daraja,Balozi Sanga,Balozi Sefue,Balozi Chokala na hata Chabaka Kilumanga,kwa nini watu hawa na wengine ambao hatujawataja wasijenge Timu imara ya kunoa Hotuba za Mkuu wa Nchi?.

Huyu Salva alikwishaambiwa matatizo ya Hapo Ikulu,nae aliingia kwa kuibadilisha sura ya Kitengo cha mawasiliano kwa kuwapangua akina Dada waliojazana hapo,lakini leo nae anaonekana kama mwanasiasa zaidi,hakuna lolote linaloendelea hapo,hali imekuwa mbaya kuliko kipindi cha Balozi Kalaghe.Waungwana.....Imefika kipindi cha kuwahoji hawa watendaji.Tanzania ni yetu sote,Aibu inayozungumzwa inatugusa sote...Inatia aibu kuona kwamba jina Tanzania linadidimia kwa sababu ya Uongozi Dhaifu...Mnaokutana na hawa wahusika fikisheni messages zetu,tusichoke kuwaamsha hawa Watendaji!!!


Mkuu Mwawado,

Heshima mbele sana bros, maana yako ni maneno mazito sana, na nina wasi wasi kuwa umewahi kuhudhuria vikao pale, maana sio rahisi kwa mwananchi wa kawaida kusema maneno kama haya yako,

Ukweli ni kwamba haya yamekua ni matatizo ya muda mrefu sana toka mtandao washike power, wengi wao wanaamini kuwa wanajua sana, nasikia pia hawashauriki, mimi nimewahi kuwa-intern ubalozi wa Dominican Republic, ninapafahamu sana pale mahali,

huwezi kwenda na hotuba za kuomba kura Tarime, kuna wakati kiongozi wetu mmoja simtaji jina maana itakua aibu akaenda pale na kuanza kuongelea Chadema, na CUF mkutano unahusu Security Council, wajumbe wakabaki kuulizana what happened to Tanzania?

Ukiwaambia ni wabishi hawataki kusikiliza la mtu, ninafahamu kuwa kiongozi yoyote anapokwenda UN ni lazima anatakiwa awasiliane na maofisa wa ubalozi kule UN ili wampe the inside, na ni wao ndio wanaotakiwa kumtengenezea hotuba, kwa sababu wao ndio wanaojua vizuri nasaba ya ule mkutano, na wanajua vizuri sana nani atakuwepo, na nani msimamo wake ukoje, na nini kina-make a sense,

Lakini mara ya mwisho niliskia kuwa wakuu wetu bongo hawataki kabisa kuambiwa hayo na si wao hasa, bali wasaidizi wao, nasikia ndio hasa hawataki kabiisa kusahihishwa, wakiambiwa hotuba zina makosa kabla ya mkulu kwenda UN, nasikia huwachongea maofisa wa kule kuwa wanajifanya wanajaua sana, haya ndio matokeo, naomba uniambie kabla hajawa rais nani alikuwa msaidizi wake wa kumsaidia hotuba? Aibu tupu hata kuwataja,

Ndio maana wengine tunaona hakuna cha ajabu hapo ni aibu juu ya aibu tu!
o!
 
Mwawado,
Balozi Daraja alibwaga manyanga. Mambo ya Ikulu yalimshinda.
 
Kuna Magwiji wa uandishi wa Hotuba kama Balozi Daraja, Balozi Sanga,Balozi Sefue,Balozi Chokala na hata Chabaka Kilumanga, kwa nini watu hawa na wengine ambao hatujawataja wasijenge Timu imara ya kunoa Hotuba za Mkuu wa Nchi?

Mkuu Mwawado,

Hao uliowataja wanaweza kuunda timu nzuri iwapo watapewa nafasi hiyo. Uzuri mwingine ni kwamba JK na Mzee Luhanjo wamekaa na hao watu kwa miaka 10 na wanawafahamu vizuri sana. Labda tujiulize, kwanini JK hataki kuwatumia hao watu ambao wanauwezo?

Ninachokiona mimi ni kwamba JK ameridhika na hayo madudu na wala haoni kama kuna kasoro kwenye hotuba. Pia inaweza kuwa ni signal kwamba yawezekana JK usanii umemzidi sana na hivyo kufanya kazi na watu makini inakuwa ngumu sana. Maana kufanya kazi na msanii lazima na wewe uwe msanii. Kwa hiyo yawezekana anakwepa kuweka watu makini kwa kuwa wanaweza kumuumbua kwa kujiuzulu ama kupingana nae kwenye baadhi ya mambo.
 
..umenionea. unaniuliza kitu ambacho sijakisema.

..ofisa wa jwtz, mtumishi wa chama wa muda mrefu, waziri wa nishati,waziri wa fedha,waziri wa mambo ya nje for 10yrs.

..10 yrs as the President in waiting.

..ndiyo maana nasema Kikwete alipaswa awe most competent, and most succesful, kuliko hao waliomtangulia.

Unakosea tena.

Paper credentials za Kikwete sio the most robust. Amepitwa mbali.

Mkapa: Dodoma, Tanzania, appointed government administrative officer, 1962, became district officer, 1962, became foreign officer, 1963. Managing editor, The Nationalist and Uhuru (newspapers), 1966, The Daily News and The Sunday News (newspapers), 1972. Office of the president, press secretary, 1974; Tanzania New Agency, founding director, 1976; High Commissioner to Nigeria, 1976; Minister for Foreign Affairs, 1977-90; Minister for Information and Culture, 1980-83; High Commissioner to Canada, 1982-83; ambassador to the United States, 1983-84; Minister for Foreign Affairs, 1984-90; Minister for Information and Broadcasting, 1990-92; Minister for Science, Technology, and Higher Education, 1992-95. Nominated as member of parliament, 1977; elected to National Assembly for the Nanyumbu Constituency, Masasi District, 1985, re-elected, 1990;

Mwinyi: Entered politics in 1963, became permanent secretary to the minister of education in Zanzibar; appointed to the Tanzanian cabinet as minister of state in the president's office,1970; held various government posts in succeeding years, including minister of health and home affairs, 1982-83, and minister of natural resources and tourism, 1982-83; also served as ambassador to Egypt for five years; elected president of Zanzibar and chairman of the Zanzibar Revolutionary Council, 1984; elected vice-chairman of Tanzania's ruling party, CCM, 1984

(Excerpted from Answers.com)

Nyerere: 1961 – 62 Prime Minister ( chini ya Governor General), 1953 Chairman, Tanganyika African Association, 1954 transforming founder, Tanganyika African National Union (TANU). The late 50s, Spearheading leader of Independence movement.

Sawa ?

Kwa hiyo kusema "on paper Kikwete is supposed to be the most competent and successful" zaidi ya Mkapa na Mwinyi ni distorted grasp of presidential history.
 
Mwandishi wa Ikulu

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameyaonya mataifa ya Bara la Ulaya kuacha.... Rais Kikwete alikuwa kiongozi wa 12 kuzungumza katika kikao cha mwaka huu cha UN yenye nchi wanachama 192 na alitoa msimamo wa Afrika baada ya ripoti ya utangulizi ya Katibu Mkuu wa Umoja huo, Ban Ki Moon uliofuatiwa na hotuba za Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, Rais George W Bush wa Marekani, Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa, Rais Gloria Macapagal-Arroyo wa Philippines na Sheikh Hamad bin Khalifa Al-Thani wa Qatar.

Wengine waliozungumza kabla ya Mwenyekiti huyo wa AU ni Rais Daniel Ortega Saavedra wa Nicaragua, Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Rais Abdallah Gul wa Uturuki, Rais Cristina Fernandez de Kirchner wa Argentina, Rais Marc Ravalomanana na Rais Boris Tadic wa Jamhuri ya Serbia.....
.


Ukisikia watu wamekosa la msingi la kuandika na kuanza kujazia listi ya simba au Yanga, ujue kuna shida!

Who cares who was the first speaker or last one or the damn list of those who spoke before Mkwere?

Huyu mwandishi wa Ikulu angekuwa anaandika Paper, hapo kapoteza maksi kwa kujaza kurasa na upupu!
 
Kwa hiyo yawezekana anakwepa kuweka watu makini kwa kuwa wanaweza kumuumbua kwa kujiuzulu ama kupingana nae kwenye baadhi ya mambo.

Ndio mana nikasema kabla hujalaumu wasaidizi wake wa sasa, jaribu kuangalia akiwa waziri, utapata jawabu!
 
Ukisikia watu wamekosa la msingi la kuandika na kuanza kujazia listi ya simba au Yanga, ujue kuna shida!

Who cares who was the first speaker or last one or the damn list of those who spoke before Mkwere?

Huyu mwandishi wa Ikulu angekuwa anaandika Paper, hapo kapoteza maksi kwa kujaza kurasa na upupu!

Mkuu hiyo ni kawaida ya style ya mtandao, na nasikia hutoka kwa mwenyewe kuwa lazima uandike watu wajue kuwa walikuwepo wakubwa na waliongea kwanza ndio na mimi nikaingia, usisahau kuweka hiyo, hizo nasikia ni order za kawaida, kwa hiyo usishangae!
 
Huyu jamaa namsikia sikia tu....who the hell is this guy? Ana uzoefu gani katika mambo ya kuandika spichi? Au uzoefu wake kautoa youngafrican kubishana na kina Critic na Bill Powers.....

Nyani,

Na wewe ulivaa jezi gani kwenye chama hilo? With speechwriters like Makamba no wonder anachemsha.

Unajua rais anaweza kuwa hamnazo lakini akajua kuji-surround na watu wenye uwezo akapeta.

Sasa Kikwete hamnazo anaji surround na watu ambao sifuri kama yeye, the Mkullos, Makambas (father and son, both bogus) watu kama kina Cisco mtiro sijui, ovyoo.

Sasa unategemea nini? hamna kufunga wala nini, kwani Ahmadinajad hajafunga?
 
Matatizo ya Speech za Rais hayakuanza leo...Mwaka jana licha ya kuchelewa kwenye kikao cha UN pia alitoa Speech Nyepesi kupindukia..Hii Speech ya Juzi ilizungumzia mambo mengi,kilichotokea ni kubabaika na lafudhi ya kiswahili katika maneno ya kiingereza,Kuzungumza mambo mengi juu juu kwa wakati (muda) mdogo (dk 45).

Hotuba inayotolewa UN inatakiwa iwe nzito na inayofanana na Hadhi ya hapo mahali,Hiyo sio Hotuba yakuomba kura kule Tarime,au Hotuba ya Ufunguzi wa Daraja huko Songea,Hotuba hizi ndio zina hadhi ya akina Januari,lakini sio Hotuba zinazotolewa kwa watu waliobobea kwenye siasa Nzito.......zinataka watu waliopevuka kwenye Diplomasia na uwezo wa Lugha nyepesi ya kistaarabu na inayoeleweka.

Kwa Mtazamo wangu naona kuwa kuna matatizo makubwa katika Kitengo cha Mwasiliano Ofisi ya Rais.Ama kwa makusudi wanamfanya Mh.Rais Mpuuzi ama watu hawa hawajui vizuri kazi zao.Haiingii akilini kusikia kuwa Januari Makamba ndio yupo kwenye list ya Waandaaji Hotuba za Rais,sina uhakika kama kijana huyu alimaliza shule yake,kwa sabau alikwenda State House kwenye Intern tu,na sio kama ndio ilikuwa ajira.Kuna Magwiji wa uandishi wa Hotuba kama Balozi Daraja,Balozi Sanga,Balozi Sefue,Balozi Chokala na hata Chabaka Kilumanga,kwa nini watu hawa na wengine ambao hatujawataja wasijenge Timu imara ya kunoa Hotuba za Mkuu wa Nchi?.

Huyu Salva alikwishaambiwa matatizo ya Hapo Ikulu,nae aliingia kwa kuibadilisha sura ya Kitengo cha mawasiliano kwa kuwapangua akina Dada waliojazana hapo,lakini leo nae anaonekana kama mwanasiasa zaidi,hakuna lolote linaloendelea hapo,hali imekuwa mbaya kuliko kipindi cha Balozi Kalaghe.Waungwana.....Imefika kipindi cha kuwahoji hawa watendaji.Tanzania ni yetu sote,Aibu inayozungumzwa inatugusa sote...Inatia aibu kuona kwamba jina Tanzania linadidimia kwa sababu ya Uongozi Dhaifu...Mnaokutana na hawa wahusika fikisheni messages zetu,tusichoke kuwaamsha hawa Watendaji!!!

Balozi Mwawado,

maneno mazito hayo mkuu......i hope wahusika wamekusikia.........matatizo ya ushikaji ni mabaya sana............
 
jamani nimeona Jk akisema kujiuzulu kwa Mbeki is a great loss to Africa, je amewaonaq wa South ni wajinga? Ki-protocol inaruhusiwa au? na Je ianzishiwe thread yake au ijadiliwe hapa hapa.

....if that is true is really undiplomatic comment ..amounting to enterfearance of internal matters of RSA gorvernment......statement like that could be timely placed on mwanawasa"s funeral....you can not regard mbekis move as A LOSS[TRAGGIC]..it is rather a DEMOCRATIC move......amekosea sana ..ndio maana itabidi kikwete awe anatembea na mtu wa kumnongoneza maneno ya kusema sikiomni kila anapoenda ..kwani akili yake na mdomo havina ushirikiano.......nadhani mnakumbuka last days za YASSER ARAFAT hasa baada ya kupata mild stroke or parkingsons signs....kila anapoenda nyuma yake alikuwa anakuwa na msaidizi wa kumsaidia cha kuongea pale anapoona anakwama.;....i think our president need that.....nakumbuka kusoma kuhusu marais wa zamani wa marekani ...kuna mmoja wao zamani alikuwa ameweka msaidizi nyuma yake wa kumkumbusha majina ya watu anaokutana nao..alikuwa na tatizo la kukumbuka majina ya watu.....ie mtu akija mbele yake msaidizi atamnongoneza "..........mr pressident..infront of you is former governor jefferson you played golf at his ranch last summer..."""...nayeye hapo hapo atasema ..."...halllo mr jefferson welcome to whitehouse....i enyoyed last time we played golf...bla..bla.."..unajuwa kwa wazungu ..au kistaarabu kumtaja mtu kwa jina ni muhimu sana!!!............
 
Kama ningekuwa ni Kikwete au Mwenyekiti wa AU, ningeongelea umuhimu wa kulinoa bara la Afrika katika kupambana na mazingira hasa katika matumizi ya Nishati za Jua, Upepo. Kutoa msukumo wa Sayansi na teknolojia mpya kwa Afrika ili kutoa uwiano bora wa maendeleo.

Ningekemea tabia ya nchi zenye viwanda kupuuza bara la Afrika kwa kutuuzia bidhaa mbovu na majaribio na kutufanya jalala la uchafu wao.

Ningelia na nchi tajiri kuhusu bei za mazao na ushirikiano wa Biashara kwa kuruhusu Ruzuku kwa wazalishaji wao huku wakikemea Serikali zetu kwa kutoa ruzuku. Ningepigania kurekebishwa kwa soko la dunia na hivyo kumfanya mkulima, mvuvi na mfanayakazi wa Afrika apate pato la kuhimili maisha na kuondokana na umasikini.

Ningekoromea double standards za baraza kuu la usalama hasa zile nchi kuu 5, kwa kushindwa kuwa kinara wa kuingoza Dunia katika amani, maendeleo n autunzaji mazingira.

Ningekemea tabia ya nchi tajiri kudhulumu nchi changa na masikini kupitia miradi au miuondo mbinu ya uwekezaji. Kwenye hili ningejigeuzia kidole na kutaka nchi zote za dunia ya tatu kuacha kuwa wanyenyekevu na kutegemea misaada.

Ningerejea kwenye nia ya kujenga jamii zenye kujitegemea kwa kuoanisha mifumo ya uchumi ambayo ingelenga katika kutoa haki sawa kwa mwanadamu kama imani kuu za UN zinavyosema ambazo ni kufuta ujinga, umasikini na maradhi.

ningeongelea umuhimu wa nchi tajiri na makampuni yao kuruhusu nchi changa na maskini kupata teknolojia na utaalamu wa kuwezesha nchi hizi ziwe na uwezo wa kujitegemea na kujitosheleza. Suala la haki miliki za magunduzi ya sayansi na tiba (afya) ningelikoromea sana na kuhoji ni vipi tutaijenga dunia mpya ya kuingia karne mpya ikiwa tunadhoofika kwa magonjwa na umasikini huku tuna uwezo wa kushinda vita hivi?

Lakini kwa kuwa Mkwere anafahamika kwa kutembea na bakuli na vikengele vile vinavyovaliwa miguuni wakati wa kucheza ngoma, hotuba yake kamwe haiwezi kuwa ya substance!

He is victim of his own demerits and inferiority, he can never be a champion of change and success under the circumstance that he is prevailing and especially on self sufficiency and good governance.

Lets give him his Hi Five; He did his best!
 
Halafu kitu kimoja tunakimiss; hivi hotuba ya JK jana alikuwa anazungumza kama Mwenyekiti wa AU au kama Rais wa URT? au aliamua kuchanganya yote mawili? Alipozungumza kuhusu suala la Palestina alisema kuwa suluhisho la nchi mbili sambamba za Israeli na Palestina lazima lifikiwe hitimisho.

Tukijiunga na OIC msimambo wa OIC ni kuwa Yerusalemu (Al Quds Al Shariff) uwe makao makuu ya Palestine. Je sera yetu kuhusu mgogoro wa Palestina kweli inaeleweka? Alizungumzia suala la Darfur na kusisitiza kuwa kwa wao (viongozi wa Afrika) kutaka mashtaka dhidi ya Al Bashir yawe deferred isionekane kama wana endorse injustice in Darfur. Wanasema wanataka serikali ya Bashir isitengwe na ihusishwe ili mambo yasichafuke zaidi.

Hivi ni lini Tanzania tumekuwa waoga kupinga serikali inayowatesa watu wake. Wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Madola in 1960s Nyerere alimwambia Malkia na wajumbe kuwa kama Afrika ya Kusini itapigiwa kura kuingizwa tena humo, basi kura hiyo itakuwa imeipigia Tanzania kujitoa. Hakuwa na compromise kwenye hilo. Juzi tumeona kati ya nchi zote za Afrika ni Botswana ambayo pekee ilikataa kumtambua Mugabe na nadhani waliondoa hata balozi wao or some sort of a diplomatic step kuonesha kuwa hawakufurahishwa.

Yeye jana amewaambia kuwa msimamo wa AU ni kuwa mahali popote katika Afrika ambapo demokrasia inachezewa basi kiongozi huyo hatatambuliwa na uongozi huo na akatolea mfano wa Mauritania. Lakini wakati huo huo alishindwa kusema mbona walimuacha Mugabe aingie kwenye kikao chao kule Misri kabla ya mazungumzo haya ya muafaka na hawakumkatalia?
 
Ukisikia watu wamekosa la msingi la kuandika na kuanza kujazia listi ya simba au Yanga, ujue kuna shida!

Who cares who was the first speaker or last one or the damn list of those who spoke before Mkwere?

Huyu mwandishi wa Ikulu angekuwa anaandika Paper, hapo kapoteza maksi kwa kujaza kurasa na upupu!

Rev,

Muandishi anachukua somo kutoka kwa bosi wake Kikwete. Ulimuona Kikwete katika ile interview ya MSNBC a few years ago? Watu wanamuuliza maswali Prime Time TV kuhusu mambo ya uchumi yeye anaanza kutaja majirani wa Tanzania, akaanza Kenyaaaa, Ugandaaaaa, Rwandaaaa, Burundiiiii, Congooo, Zambiaaaaa, Malawiiiiiii, Mozambiqueeee

Watu wenye 8 second attention span wakawa wamekwisha flip channel.

Kikwete bonge la mtupu.
 
Hapa inabidi ajifunze namna ya ku-prioritize vitu sio ishu ya kusimama bungeni masaa matatu unapiga porojo
 
Is it possible to talk about the content of the speech?
 
Rev,

Muandishi anachukua somo kutoka kwa bosi wake Kikwete. Ulimuona Kikwete katika ile interview ya MSNBC a few years ago? Watu wanamuuliza maswali Prime Time TV kuhusu mambo ya uchumi yeye anaanza kutaja majirani wa Tanzania, akaanza Kenyaaaa, Ugandaaaaa, Rwandaaaa, Burundiiiii, Congooo, Zambiaaaaa, Malawiiiiiii, Mozambiqueeee

Watu wenye 8 second attention span wakawa wamekwisha flip channel.

Kikwete bonge la mtupu.

Pundit,

Umenifanya nicheke nikikumbuka jinsi alivyokuwa kajikaza kifua mithili ana ushuzi!
 
Back
Top Bottom