Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)


Sasa hivi kinana na lowassa sio marafiki kama wengi wanavyofiria,kinana is a problem kwa kina lowassa,na kama mwenyekiti angekua ni mtu thabiti na mwenye kumaanisha anachokisema kinana angemsaidia sana,yule msomali ana akili nyingi sana miongoni mwa viongozi wa ccm,anajua ccm inaumwa ugonjwa gani na anaijua tiba ya ugonjwa wa ccm sema ndio hivyo mwenyekiti mwenyewe haeleweki leo atakwambia hivi kuhusu lowassa badae unamuona wako pamoja na yote uliyomshauri kuhusu lowassa jana leo lowassa anakupigia simu anakueleza jana mlikua na chairman ukamwambia hivi na hivi na hivi! Ndio mana mtu kama kinana anaamua kujiweka pembeni,lakini kwenye vikao huwa anawachana live kwamba tatizo ni kina lowassa ndio wamekifikisha chama hapo kilipo na ingekua busara wakae pembeni ili mambo yaendelee.Na jk amekuwa akimtaka sana kinana kwenye utawala wake kinana anamchomolea kwa kuwa kisha msoma jamaa hawezi kuachana na kina lowassa na kinana yeye anaamini ili mambo yaende lowassa akae pembeni na rostam adhibitiwe,sasa anasema kutokana na msimamo wa jakaya kwa hao jamaa zake yeye anaona akae mbali kwa sababu hataki kugombana na mtu bora aendeshe biashara zake!

Nafasi za mwisho mwisho alizotaka kupewa na jakaya na kuzikataa ni uspika kumrithi sitta na badae ukatibu wa chama kuchukua nafasi ya mzee makamba.
 

Najua kuna watu watarukia trivial issue ya uandishi, ngoja nisahihishe: SACRIFICED. Lazima tujifunze maslahi ya nchi makubwa kuliko binadamu mmoja. Inatakiwa mtu wa ndani anayefahamu haya madudu kuongoza clean up ya kuondoa nyoka wote bila kujali nafasi aliyepo kwenye usukani (JK,EL+RA) na ndipo hapo atakayechukua usukani ataheshimu hiyo nafasi. Kamwe ukijua ya kwamba Rais hashitakiwi bali anaweza kushughulikiwa kwa kupelekwa kwenye mahakama ya muumba wake kipindi akileta upuuzi ndipo hapo hakutakuwa na mtu anayekimbilia nafasi hiyo. Huo utakuwa mwanzo wa viongozi wanaotakiwa kuguswa bega na kuombwa kuchukua uongozi wa nchi nao watafikiria mara 10 kidogo kama kweli je nichukue hayo madaraka!?

Najiuliza hayo mafunzo huko China, Cuba na kwengineko sijui ni kwa faida gani? Wenzetu WaIsrael walipoona ARIEL SHARON anahatarisha survival ya state yao waliyoipigania ingawa na yeye ni one of their strong fighters...mpaka sasa anakula na kupumulia kupitia kwenye mirija. Walijifunza direct action kama waliyofanya kwa Y. Rabin ingesabisha vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Story hii ni nzito. Ni kama ya mtandao wa freemasons. Kama haya yaliyotamkwa yana chembe ya ukweli, Tanzania inapelekwa wapi? Nanyi wana JF ikiwa tutagundua chembe ya ukweli, as great thinkers, nini litakuwa jukumu letu?
 

Yap hapa tunaenda pamoja!RO hana meno ya kutosha kama wakubwa wa kitengo wa zamani,kama sasa hivi jk ana deal zaidi na Jacky Mugendi Zoka kuliko Rashid.
 
 
@ Mtoa Habari!

Inatisha na kukatisha tamaa. Ila pia nilikuuliza kuhusu kifo cha prof. Mwaikusa na tetesi za yeye kudaiwa kukutana na Daudi Balali (sijui ni kwa bahati mbaya au kwa kupanga) huku USA.

Je kuna ukweli wowote na nani walihusika, an ina uhusiano wowte ule na haya mambo ya kuelekea 2015?
 
Mkuu Mtoahabari, hapo kwenye red umenikumbusha kitu fulani. kuna siku nilikuwa pale Rose Garden na nikamuona L.Masha akiwa na
vijana kama sita hivi wakipata lunch karibu sana na sehemu ambayo na mimi nilikaa kupata lunch yangu....kusema kweli kwa mbali
nilimsikia Lau Masha akimuongelea EL kwa wale vijana aliokuwa amekaanao pale,yaani ilikuwa kama kuna maagizo fulani anawapatia
kuhusiana na EL....yaani walitumia karibu nusu saa hivi kumuongelea EL,lakini Lau Masha alikuwa anaongea kwa sauti ya chini sana kwa hiyo sikuambulia kitu chochote pale zaidi ya jina la EL. Je huyu Masha nae yuko kwenye kundi la EL au yuko against EL?
 
Cabinet ya kwanza ya JMK ilikamatwa na ENL na RA. Kamati Kuu ya CCM na secretariet yake ilikamatwa na ENL na RA akiwa mweka hazina kabisa wa CCM. Zikaanza teuzi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, miji na manispaa kwa utaratibu huohuo. Ungeweza ukadhani JMK alikuwa MZANZIBAR!
Uchaguzi mkuu wa CCM mwaka 2007 ulisimamiwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na secretariet ya CCM makao makuu chini ya Makamba ambaye ni muumini mkubwa wa ENL na RA. Wakapatikana wenyeviti wa wilaya na mikoa ambao ni "watiifu" na waumini wakubwa wa ENL na RA. Nchi ikawa imekamatwa kisawasawa.
Teuzi kubwa za vyombo vya DOLA nazo kwa kiasi kikubwa zina mikono ya hawa jamaa wawili. Bunge letu nalo likapewa Sitta ambaye mwanzoni walimwamini sana kabla yeye mwenyewe hajashtuka baada kugundua kuwa alistahili kuwa WAZIRI MKUU badala ya kuwa SPIKA. Mtaikumbuka ile "wish" ya Lowasa aliyosema atai-"grant" wakati anaachia ngazi.
Hapa ndipo tulipo. Jamaa wanajipanga upya kuichukua CCM baadae mwaka huu kwa ajili ya 2015. Tatizo kwao sasa hivi ni Mukama na secretariet yake. Inasemekana bado hajakubaliana nao mambo mengi tu. Kwa namna alivyo mwoga haioneshi kama atakuwa kikwazo sana kwao. Vinginevyo naye anaweza kuwa kama Dr OA Juma. Nape hata ubalozi wa Burundi utamtosha. January kama baba yake ni mtu wao. Mwigulu yeye ni mkate wake wa kila siku tu.
 

Mwaka 1995 au mwaka 2000?? Nakumbuka kuisoma hii kwenye jamboforums, thanks to Mzee ES siku zile. Si aliikanyaga bendera ya taifa vile?
 
Mkuu ahsante sana kwa uchambuzi wako na nimeuwelewa vilivyo! Ila bado sijaelewa kuhusiana na Lau Masha
Je, huyu mtu yuko kundi gani? la Membe au la EL?
 
Mkuu ahsante sana kwa uchambuzi wako na nimeuwelewa vilivyo! Ila bado sijaelewa kuhusiana na Lau Masha
Je, huyu mtu yuko kundi gani? la Membe au la EL?
Lau aliingia kwenye Cabinet ile kwa msaada na uhusiano mzuri na kijana wa JMK, Riziwani na kampuni yake ya uwakili kusaidia sana ufisadi wa EPA. Ndani ya Cabinet ile akagundua mwenye nguvu mle alikuwa ENL. Unakijua kisa cha paka kuhamia jikoni na mbwa akabaki sebuleni?
 

loooh! mkuu km hii habari ni ya kweli napata mashaka na DR.Slaa jembe nilililoliamini,
hata hivyo siwezi kukuamini sana, maana km batilda arusha ni mtu wa EL na bado wakahenyeshwa na G.Lema wa CDM wakati huo huo unasema miundo mbinu yote ya CDM kaitengeneza EL, ngoja nifikirishe kichwa changu zaidi kabla yakukubali maneno yako yaote.
 
Na JWTZ iko upande gani kwenye sakata hili linaloendelea kuiva?
 
Nimependa mnavyomuuuliza Mtoahabari maswali. Natamani nijibu baadhi lakini mie msimamo wangu upo wazi ni kumtetea na kuomba Lowassa awe rais JK akimaliza muda wake 2015.

Kwahiyo nitaonekana nipo biased.

Mag3 karibu kwenye ELairline.

Mkuu wangu Wildcard uchambuzi mzuri nimeukubali.

Romantic angalau umetoa points za kutosha mkuu.
 
Hamia huku kungine FP. Lowasa alitufaa wakati huo. Sio sasa wala hapo baadae!
 

Nimeamua kuinunua hii kesi ya hawa jamaa aise hata wakatambikie katika makaburi yote na madhabahu wanayayo ya jua kuwa yana nguvu hakuna kati yao wala mtu wao atakaye upata urais wa Tanzania....Mbaya zaidi kuaznia sasa wataingia katika mgogoro mkubwa na wao kwa wao watatoana ngeu na kuvuana nguo hadharani mpaka mambo yao yote yatakapo kuja kwenye uso wa watanzania wawasome vizuri wao ni watu wa aina gani; says the prince the son of th most high Jesus Christ son of David.
 
Reactions: DSN
Hamia huku kungine FP. Lowasa alitufaa wakati huo. Sio sasa wala hapo baadae!

Wapi? Upande upi kaka? Hamna upande wowote zaidi ya Lowassa.

Naomba nishawishi nihamie upande wenu kwa hoja na sio kwa kumkashifu Lowassa! Hapo ndo mnakosea. Mmepoteza ushawishi mmebakia na eti ukimsema EL utafanya vile au hivi a pure BS!

Anza kunishawishi basi......
 

tungekuwa na watanzania kumi tu au watano tu hapo TISS kama wewe...
hii nchi ingeshafika mbaali mno......
na sijui kama wamekuelewa...
 

Utatoka mapovu bure. HuKo kwa Jesus pia tumeshaenda, tume pewa a go ahead pia. Labda uende kwenye mashetani huKo hatujaenda, kwakua tunaamini nguvu ni moja tu ni Mungu.

Lowassa chaguo la Mungu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…