KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,147
Kinana yupo sahihi, kwani mkataba uliopo ni baina na JK na EL/RA, kinana yeye hayupo humo, huwa wanamuomba tu awe mwenyekiti wa kampeni kwa sababu yupo very sharp, na ana mvuto na ushawishi mkubwa ndani ya CCM. Vinginevyo mkataka uliopo kati ya JK na EL ulianzia mwaka 1995, kwamba wewe ukiwa rais, mimi waziri mkuu, mimi nikiwa rais, wewe waziri mkuu, na yeyote atakayekuwa waziri mkuu atakuwa ni Rais in waiting. Na ndani ya mkataba huo, JK, EL, RA wakafanya madudu mengi pamoja katika kipindi cha 1995 - 2005, ambayo yalizidi kuwa bind pamoja. Vinginevyo EL angeamua kuwa kama Kinana - kuachana na Siasa na kujikita katika biashara zake, nchi isingekuwa katika hali tete kama hii leo. Ikumbukwe pia kwamba Kinana na EL ni marafiki wa miaka mingi sana, na ukaribu wa Kinana na JK ulijengwa na EL.
Ipo siku jina na EL litapotea katika anga za siasa na kurudisha nchi katika hali ya utulivu na ujenzi wa taifa. Vinginevyo mpaka tufike huko, tukubali kupoteza muda na nguvu zetu nyingi kuhoji, huyu EL ni nani, ana malengo gani na nchi hii, na kwanini anataka Urais kwa nguvu kubwa kiasi hicho wakati kiongozi wa kweli ni yule anaeogopa madaraka.
Sasa hivi kinana na lowassa sio marafiki kama wengi wanavyofiria,kinana is a problem kwa kina lowassa,na kama mwenyekiti angekua ni mtu thabiti na mwenye kumaanisha anachokisema kinana angemsaidia sana,yule msomali ana akili nyingi sana miongoni mwa viongozi wa ccm,anajua ccm inaumwa ugonjwa gani na anaijua tiba ya ugonjwa wa ccm sema ndio hivyo mwenyekiti mwenyewe haeleweki leo atakwambia hivi kuhusu lowassa badae unamuona wako pamoja na yote uliyomshauri kuhusu lowassa jana leo lowassa anakupigia simu anakueleza jana mlikua na chairman ukamwambia hivi na hivi na hivi! Ndio mana mtu kama kinana anaamua kujiweka pembeni,lakini kwenye vikao huwa anawachana live kwamba tatizo ni kina lowassa ndio wamekifikisha chama hapo kilipo na ingekua busara wakae pembeni ili mambo yaendelee.Na jk amekuwa akimtaka sana kinana kwenye utawala wake kinana anamchomolea kwa kuwa kisha msoma jamaa hawezi kuachana na kina lowassa na kinana yeye anaamini ili mambo yaende lowassa akae pembeni na rostam adhibitiwe,sasa anasema kutokana na msimamo wa jakaya kwa hao jamaa zake yeye anaona akae mbali kwa sababu hataki kugombana na mtu bora aendeshe biashara zake!
Nafasi za mwisho mwisho alizotaka kupewa na jakaya na kuzikataa ni uspika kumrithi sitta na badae ukatibu wa chama kuchukua nafasi ya mzee makamba.