Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

The Romantic,

Mie wala sijakupinga. Nilichokua nasisitiza ni watu kufikiri ELAirLine itaishia Nec ya CCM.

Kama unavyofikiri wewe mie nikasema wrong strategy!

Karibuni ndani jamani humu kila kitu kipo sawa, Lengo la ELAirLine ni kutumikia wananchi tu basi. Maana humu ndani ya ELairline kila mtu amesharidhika.

Mengine tupo pamoja. Tunatofautiana tu kuwa mie nataka ELAirLine itue Ikulu 2015
 

Mkuu kama hii ndio strategic yenu kufikiri kwamba EL akisimamishwa na CCM, chadema itashinda kurahisi think twice???

Kwanza, EL akipitishwa na CCM (God Forbid) hakuna mpinzani ataweka mguu wake kushindana naye atawanunua wote au at least watavurugana wote; nakupa hint: Slaa atatumika mzee sabodo ambaye sasa ndio njia ya mtanado wa lowasa kupata habari zake; na Zitto na Mbowe wana direct contact na Lowassa na bei zao zinajulikana; wengine huko chadema wachumia tumbo au hawana mshiko au hawajui siasa. mfano Prof. Baregu hana ushawishi zaidi ya wasomi wenzake wa st. augustino..mnyika wananulika maana wanahitaji ubunge at most...

Hivyo wote wanaipenda hii nchi na watu wake kiukweli ni kumzuia kina EL asipite ccm; of course akipita tutaondoka wengi kutafuta vyama vingine lakini hata hivyo siyo chama ambacho kitamsimamisha padre kuwa rais wa nchi..
 

La hasha umeninukuu vibaya labda mi wala sifikirii hivyo naona unanichanganya na Pasco na genge lake la waumini wa strategy hiyo,narudia tena naamini katika mapambano ya ndani ili kumdhibiti adui asiwafikie nyie huko badala yake wamchinjie huko huko chumbani kwao then abaki kuwa meneja wa kampeni za chama chake mkoa wa arusha ambako ndio ngome yake pekee tunavyoaminishwa japo wanashare na chadema "ngome" hiyo!LOWASSA IS A DISASTER TENA SIO KWA CCM BALI KWA VYAMA VYOTE,HATA HAO WALIOJIANDAA KUMPOKEA ATAKAPONG'OLEWA CCM NA KUONDOKA NA Kina : Deo Sanga (Jaa People- Iringa), Ernest Mabina (Mwanza) na Khamis Mgeja (Shinyanga), John Guninita (Dar es Salaam), Nawab Mulla (Mbeya), Onesmo Ngole (Arusha), William Kusila (Dodoma),Hypolitus Matete (Sumbawanga),Peter nk watakaribisha matatizo makubwa kwenye vyama vyao
 
...watu walienda mbele kidogo........na unavyofikiri....hebu msome Bob hapo chini.......msifikiri watu hawakuwa wanaliona hilo..........kama alivyokulezea TR.....vita hii ni muhimu kuanza kupigana within....believe me....Mag3!

Mkuu Ogah, wengi mpaka sasa wameshindwa kunielewa. Tofauti na wengi mimi si mnafiki na sifichi chuki niliyo nayo dhidi ya CCM kwa sababu kama nilivyowahi kusema hapo nyuma naamini adui mkubwa wa taifa letu ni CCM kwa kuwalea na kuwakumbatia mafisadi na wezi wanaoifilisi nchi. Nakataa kata kata kuwa ndani hili genge la mafisadi na wezi yupo au anaweza akatokea kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kuikomboa Tanzania huku hadi leo hii, saa hii, dakika hii bado kajaa humo anashirikiana na kula nao, je anafanya nini humo chumbani ? Kama hadi sasa hana ujasiri wa kuachana nao, hana ujasiri wa kukaa mbali nao na hana ujasiri wa kusema hapana, imetosha, huo ujasiri wa kupambana nao ataupata wapi ? Huyo hatufai !

Mkuu Mkandara naona na yeye humo kwenye kundi la ambao hawanielewi ama hawataki kunielewa kwa sababu sijui Chadema inaingiaje katika hoja yake. Mimi si mwana Chadema na kusema kweli hata hao viongozi wa Chadema nawafahamu tu mtandaoni kulingana na ninayoyasoma kuhusu harakati zao za kisiasa lakini niko pamoja nao kama lengo ni kuwaondoa hawa manyang'au madarakani. Historia mpaka sasa imetufundisha sote jambo moja nalo ni kuwa chama cha siasa kikishachafuka na kuwa kimbilio la wahalifu, kitatumia tu uovu kama silaha yao kuu ya kung'ang'ania kubaki madarakani. Hivyo ndivyo serikali zote za kifashisti zinavyozaliwa, zinavyokomaa na zinavyoendeshwa zikiwaonea, kuwagandamiza na ikibidi kuwaua wananchi wake.

Ni kweli kama wanavyodai wengi, yeyote yule CCM ikimsimamisha kugombea hata akiwa chizi wa kutupwa anaweza kuibuka kidedea iwe kimizengwe au kibabe, hilo halina ubishi kwani tumeshuhudia si mara moja hii ikitokea. Lakini kwa Lowassa mambo ni tofauti kidogo na nitaeleza hili kwa kuuliza swali moja kuu, je ni watu wa aina gani hao ambao hawako tayari hata kulisikia hilo jina likitajwa na je, ikatokea hivyo, watafanya nini ? Je wachangiaji kama wewe Ogah au hata Mkandara wenye msimamo wa kutotaka kusikia hata uvumi tu wa hilo, mko tayari kufanya nini kama, God Forbid, hilo jina hilo litapendekezwa ? Kulingana na michango yenu ninayoyaona humu ndani mnaamini kwamba Raisi atakuwa Lowassa na mambo yataendelea kama kawaida.

Sisi wengine on the other hand tumeenda hatua moja mbele kwa kuitambua the weakest link kwenye hiki kitendawili nacho ni aina ya watu ambao hata leo hii hawapati usingizi jina la Lowassa linapoibuka na ndio hawa tunataka ujumbe uwafikie. Bahati nzuri ni kwamba wapenzi wakubwa wa Lowassa wako ndani ya CCM na maadui wakubwa wa Lowassa nao wako ndani ya CCM na hao wote kwa pamoja bahati ilioje kuwa kiongozi wao mkuu ni Kikwete. Hapo ndipo anapoingia mtu kama Mag3, anajua pande zote zinavyofuatilia mjadala na cheche za moto zinavyoanza kuruka ruka, lahaula, anamwaga petroli ! Jamani, adui mkubwa wa CCM ni CCM na kwa wale wenye wasi wasi naomba niwatoe hofu, turufu ya mabadiliko ni Lowassa !
 
Mag3,

Wewe una akili sana! Kupitia mada hii nimewatambua wengi weenu kifikra na kiuwezo wa kuona mbali. Wengi mpo sawa ina kuona visivyoonekana tupo wachache sana.

ELAirLine for 2015!
 

Subiria vibaraka wa ENL wakurudie na PHOTOSHOPed pictures za ENL na Mwalimu, tena akiwa kabebwa mgongoni kama mtoto. Kwani umeshau watu haohao waliweza "kumtengenezea" picha Salim A. Salim na viongozi wakuu wa iliyokua HIZBU?... Just wait, wako kazini saa hizi wanazi doctor.
 

Technlojia imekua ndio lakini Watanzania wa sasa watabaini kama Photoshop au orijino watakupa fact zote.Unajua pamoja na ujio wa technlojia ya kubumba bado ubongo wa Mwanadamu ulioumbwa na Mungu unabaki kuwa ndio controller wa yote hayo.Walete kutuaminisha nasi tutakubali kama tulivyokubali hizi za JK kupata blessing ya Mwalimu.Kisha tukishakubali tunakaa chini kuulizana haya Je na hili la Richmond au Dowans nalo alilikubali?

Akitupatia na evidence ya mengine mengine yanayomzunguka nasi Watanzania kwa ujumla wao watampa go ahead kama walivyompa Kikwete na asilimia 80%.Tena kwa yeye itakuwa zaidi ya hiyo kwa kuwa huku kwenye upinzani wameshaanza mizengwe yao pia mapema.Hivyo siunawajua Watanzania na kipya kinyemi ingawa kidonda, zaidi Watanzania wanaweza kutoa huruma ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.
 
hii nchi ilisha uzwa longtime

na nani? bei gani? risiti zikowapi?
mkuu bado haijauzwa ila ndo ipo sokoni na wanunuzi ni wengi halafu madalali wanapigana vikumbo kuiuza, pambana mkuu tuwatoe hawa madalali wasituhonge kwa hao wanunuzi.
 

Hatuna kazi nyingine zaidi ya siasa. Kweli tumeishiwa akili siku hizi. Miaka ya kusubiri next president si haba na bado tunaonekana kusumbuliwa kwenye akili zetu
 
tafsiri....

 

Attachments

  • 388628_2712905379772_1171039199_33224760_1171462869_n.jpg
    39.5 KB · Views: 456
Jamani,

Nisaidieni, kwa nini anajadiliwa Lowassa tu?

Nini kinaendelea? Ujenzi, ubomoaji?...kwa nini tusijadili ukombozi wa taifa letu kwa ujumla kwa jinsi ambavyo kila mtu anakiri kuwa tumefika mahali pabaya?

Kwa nini? Au vyote vimefungamana?

Kichwa kinachoka kabisa!

Nawapeni mfano mmoja...TANESCO waliingia mkataba na kampuni moja SEMCO Maritime + Rolls Royce kujenga 60 MW heavy oil plant Mwanza. Hiyo kampuni imepigwa dana dana kupewa down payments ili ianze kazi tangu 2010 mpaka leo. Kumbuka wameingia initial costs kibao kuja Tanzania. Na kama wengi wenu mlisoma mwanahalisi la juzi kuna barua wameandika na nadhani baadaye wanaweza kwenda kudai fidia/damages mahakamani, tunarudi pale pale kwa kina Dowans na hapo tena mtawasikia hao mnaowapigia debe wakija kusema SEMCO wasilipwe!

Wote tunabakia na ushabiki wa Lowassa, JK mara sijui nani ilhali hao hao ndio wanatengenezea mashimo ya kuididimiza nchi hii!

Kama Nyani Ngabu anavyosema "Miafrika ndivyo Tulivyo!"

Mpaka JF sasa inatekwa na mjadala kuhusu Lowassa?
 
pipiii piiiiiii pipiiii piii pisheni haraka gari la urais 2015 linapita lilishakata break ukijifanya mbishi utapoteza maisha. hiyo ni horn siyo ya kupuuza
:A S 465:
 

Ngoja nimeze DOCLOPAR kwanza...
 
watatumaliza kumbe Tz bado kuna ukoloni!!!!!!
 

Sidhani kama CDM wamekosa kazi hadi waanze kutafuta mtu wa kumnadi huku tayari wagombea wanafahamika. CCM kushinda wanapigana vikumbo kuhusu Urais ni kukosa uwajibikaji kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…