Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

The Romantic,

Mie wala sijakupinga. Nilichokua nasisitiza ni watu kufikiri ELAirLine itaishia Nec ya CCM.

Kama unavyofikiri wewe mie nikasema wrong strategy!

Karibuni ndani jamani humu kila kitu kipo sawa, Lengo la ELAirLine ni kutumikia wananchi tu basi. Maana humu ndani ya ELairline kila mtu amesharidhika.

Mengine tupo pamoja. Tunatofautiana tu kuwa mie nataka ELAirLine itue Ikulu 2015
 
Romantic, ngoja na mimi niingilie kidogo hii mada maanake naona wakati Pasco anaongelea Lowassa kusimamishwa kuwa mgombea wa CCM, wewe unaongelea jamaa kuwa Raisi wetu 2015 ! Hakuna hata sehemu moja Pasco anaunga mkono Lowassa kuwa Raisi bali anaunga mkono Lowassa kuwa mgomea Uraisi kwa tiketi ya CCM - what's so hard to understand ?

Wengine wetu tunachosisitiza ni kuwa ili mabadiliko ya kweli yatokee hakuna kama Lowassa ndani ya CCM kuteuliwa kugombea Uraisi mwaka 2015 - siri ni kugombea ! Hilo la kuwa Raisi ni kitu tofauti kabisaaa na hapa ndipo wengi tumeshindwa kuona kwamba ili mabadiliko ya kweli yafanikiwe, ndani ya CCM hakuna mtu muhimu kama Lowassa - what's so hard to see ?

Tumekwenda dukani, tukanunua kitoweo, tukatayarisha chakula na sasa tumeweka mezani , kwa nini mnatutegemea kuwatafunia na kuwamezea ? Jamani hii ni JF na wachangiaji wanategemewa angalau wawe na uelewa usio chini ya ule wa wastani hivyo Romantic, mbona hueleweki ? Labda hilo umbo la Lowassa linawatisha hata msione - but what's so hard to comprehend ?

Mkuu kama hii ndio strategic yenu kufikiri kwamba EL akisimamishwa na CCM, chadema itashinda kurahisi think twice???

Kwanza, EL akipitishwa na CCM (God Forbid) hakuna mpinzani ataweka mguu wake kushindana naye atawanunua wote au at least watavurugana wote; nakupa hint: Slaa atatumika mzee sabodo ambaye sasa ndio njia ya mtanado wa lowasa kupata habari zake; na Zitto na Mbowe wana direct contact na Lowassa na bei zao zinajulikana; wengine huko chadema wachumia tumbo au hawana mshiko au hawajui siasa. mfano Prof. Baregu hana ushawishi zaidi ya wasomi wenzake wa st. augustino..mnyika wananulika maana wanahitaji ubunge at most...

Hivyo wote wanaipenda hii nchi na watu wake kiukweli ni kumzuia kina EL asipite ccm; of course akipita tutaondoka wengi kutafuta vyama vingine lakini hata hivyo siyo chama ambacho kitamsimamisha padre kuwa rais wa nchi..
 
The Romantic,

Mie wala sijakupinga. Nilichokua nasisitiza ni watu kufikiri ELAirLine itaishia Nec ya CCM.

Kama unavyofikiri wewe mie nikasema wrong strategy!

Karibuni ndani jamani humu kila kitu kipo sawa, Lengo la ELAirLine ni kutumikia wananchi tu basi. Maana humu ndani ya ELairline kila mtu amesharidhika.

Mengine tupo pamoja. Tunatofautiana tu kuwa mie nataka ELAirLine itue Ikulu 2015

La hasha umeninukuu vibaya labda mi wala sifikirii hivyo naona unanichanganya na Pasco na genge lake la waumini wa strategy hiyo,narudia tena naamini katika mapambano ya ndani ili kumdhibiti adui asiwafikie nyie huko badala yake wamchinjie huko huko chumbani kwao then abaki kuwa meneja wa kampeni za chama chake mkoa wa arusha ambako ndio ngome yake pekee tunavyoaminishwa japo wanashare na chadema "ngome" hiyo!LOWASSA IS A DISASTER TENA SIO KWA CCM BALI KWA VYAMA VYOTE,HATA HAO WALIOJIANDAA KUMPOKEA ATAKAPONG'OLEWA CCM NA KUONDOKA NA Kina : Deo Sanga (Jaa People- Iringa), Ernest Mabina (Mwanza) na Khamis Mgeja (Shinyanga), John Guninita (Dar es Salaam), Nawab Mulla (Mbeya), Onesmo Ngole (Arusha), William Kusila (Dodoma),Hypolitus Matete (Sumbawanga),Peter nk watakaribisha matatizo makubwa kwenye vyama vyao
 
...watu walienda mbele kidogo........na unavyofikiri....hebu msome Bob hapo chini.......msifikiri watu hawakuwa wanaliona hilo..........kama alivyokulezea TR.....vita hii ni muhimu kuanza kupigana within....believe me....Mag3!

Mkuu Ogah, wengi mpaka sasa wameshindwa kunielewa. Tofauti na wengi mimi si mnafiki na sifichi chuki niliyo nayo dhidi ya CCM kwa sababu kama nilivyowahi kusema hapo nyuma naamini adui mkubwa wa taifa letu ni CCM kwa kuwalea na kuwakumbatia mafisadi na wezi wanaoifilisi nchi. Nakataa kata kata kuwa ndani hili genge la mafisadi na wezi yupo au anaweza akatokea kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kuikomboa Tanzania huku hadi leo hii, saa hii, dakika hii bado kajaa humo anashirikiana na kula nao, je anafanya nini humo chumbani ? Kama hadi sasa hana ujasiri wa kuachana nao, hana ujasiri wa kukaa mbali nao na hana ujasiri wa kusema hapana, imetosha, huo ujasiri wa kupambana nao ataupata wapi ? Huyo hatufai !

Mkuu Mkandara naona na yeye humo kwenye kundi la ambao hawanielewi ama hawataki kunielewa kwa sababu sijui Chadema inaingiaje katika hoja yake. Mimi si mwana Chadema na kusema kweli hata hao viongozi wa Chadema nawafahamu tu mtandaoni kulingana na ninayoyasoma kuhusu harakati zao za kisiasa lakini niko pamoja nao kama lengo ni kuwaondoa hawa manyang'au madarakani. Historia mpaka sasa imetufundisha sote jambo moja nalo ni kuwa chama cha siasa kikishachafuka na kuwa kimbilio la wahalifu, kitatumia tu uovu kama silaha yao kuu ya kung'ang'ania kubaki madarakani. Hivyo ndivyo serikali zote za kifashisti zinavyozaliwa, zinavyokomaa na zinavyoendeshwa zikiwaonea, kuwagandamiza na ikibidi kuwaua wananchi wake.

Ni kweli kama wanavyodai wengi, yeyote yule CCM ikimsimamisha kugombea hata akiwa chizi wa kutupwa anaweza kuibuka kidedea iwe kimizengwe au kibabe, hilo halina ubishi kwani tumeshuhudia si mara moja hii ikitokea. Lakini kwa Lowassa mambo ni tofauti kidogo na nitaeleza hili kwa kuuliza swali moja kuu, je ni watu wa aina gani hao ambao hawako tayari hata kulisikia hilo jina likitajwa na je, ikatokea hivyo, watafanya nini ? Je wachangiaji kama wewe Ogah au hata Mkandara wenye msimamo wa kutotaka kusikia hata uvumi tu wa hilo, mko tayari kufanya nini kama, God Forbid, hilo jina hilo litapendekezwa ? Kulingana na michango yenu ninayoyaona humu ndani mnaamini kwamba Raisi atakuwa Lowassa na mambo yataendelea kama kawaida.

Sisi wengine on the other hand tumeenda hatua moja mbele kwa kuitambua the weakest link kwenye hiki kitendawili nacho ni aina ya watu ambao hata leo hii hawapati usingizi jina la Lowassa linapoibuka na ndio hawa tunataka ujumbe uwafikie. Bahati nzuri ni kwamba wapenzi wakubwa wa Lowassa wako ndani ya CCM na maadui wakubwa wa Lowassa nao wako ndani ya CCM na hao wote kwa pamoja bahati ilioje kuwa kiongozi wao mkuu ni Kikwete. Hapo ndipo anapoingia mtu kama Mag3, anajua pande zote zinavyofuatilia mjadala na cheche za moto zinavyoanza kuruka ruka, lahaula, anamwaga petroli ! Jamani, adui mkubwa wa CCM ni CCM na kwa wale wenye wasi wasi naomba niwatoe hofu, turufu ya mabadiliko ni Lowassa !
 
Mag3,

Wewe una akili sana! Kupitia mada hii nimewatambua wengi weenu kifikra na kiuwezo wa kuona mbali. Wengi mpo sawa ina kuona visivyoonekana tupo wachache sana.

ELAirLine for 2015!
 
Mashamushamu ya JK na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya Dodoma Uchaguzi wa mgombea kwa tiketi ya CCM Mwaka 1995.Jamani wachina wanasema Picha uongea mara 1000.Wanaompigia debe EL watutafutie evidence kama hizi japo zitupe ushahidi wa kimazingira kumbe hata yeye kuna uwezekano kuwa kumbe Watu wanamsingizia Mwalimu hakusema Bad Things [Negative] kumuhusu hivyo nasi wengine tuingie kumnadi Mzee huyo ambae kwa hakika tunasubilia ushawishi mkubwa kutuaminisha sisi tusio wakina Tomaso.

Subiria vibaraka wa ENL wakurudie na PHOTOSHOPed pictures za ENL na Mwalimu, tena akiwa kabebwa mgongoni kama mtoto. Kwani umeshau watu haohao waliweza "kumtengenezea" picha Salim A. Salim na viongozi wakuu wa iliyokua HIZBU?... Just wait, wako kazini saa hizi wanazi doctor.
 
Subiria vibaraka wa ENL wakurudie na PHOTOSHOPed pictures za ENL na Mwalimu, tena akiwa kabebwa mgongoni kama mtoto. Kwani umeshau watu haohao waliweza "kumtengenezea" picha Salim A. Salim na viongozi wakuu wa iliyokua HIZBU?... Just wait, wako kazini saa hizi wanazi doctor.

Technlojia imekua ndio lakini Watanzania wa sasa watabaini kama Photoshop au orijino watakupa fact zote.Unajua pamoja na ujio wa technlojia ya kubumba bado ubongo wa Mwanadamu ulioumbwa na Mungu unabaki kuwa ndio controller wa yote hayo.Walete kutuaminisha nasi tutakubali kama tulivyokubali hizi za JK kupata blessing ya Mwalimu.Kisha tukishakubali tunakaa chini kuulizana haya Je na hili la Richmond au Dowans nalo alilikubali?

Akitupatia na evidence ya mengine mengine yanayomzunguka nasi Watanzania kwa ujumla wao watampa go ahead kama walivyompa Kikwete na asilimia 80%.Tena kwa yeye itakuwa zaidi ya hiyo kwa kuwa huku kwenye upinzani wameshaanza mizengwe yao pia mapema.Hivyo siunawajua Watanzania na kipya kinyemi ingawa kidonda, zaidi Watanzania wanaweza kutoa huruma ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.
 
hii nchi ilisha uzwa longtime

na nani? bei gani? risiti zikowapi?
mkuu bado haijauzwa ila ndo ipo sokoni na wanunuzi ni wengi halafu madalali wanapigana vikumbo kuiuza, pambana mkuu tuwatoe hawa madalali wasituhonge kwa hao wanunuzi.
 
It is pity that in 2011, just a year after the 2010's election, we're already discussing presidential candidates for 2015. Five years in politics is a long time. More than enough for peril to be averted and political capital to be accumulated in the process. So, let's escape from that hypothetical and face the facts of brutal reality.

In 2015, the public will assess the present government in terms of the decisions made and the choices taken. They will also be delivering their verdict on the state of Tanzania in those five years. At the moment, what the public want to hear is not presidential candidates for 2015, but whether their problems are being heard and addressed.

Hatuna kazi nyingine zaidi ya siasa. Kweli tumeishiwa akili siku hizi. Miaka ya kusubiri next president si haba na bado tunaonekana kusumbuliwa kwenye akili zetu
 
tafsiri....

attachment.php
 

Attachments

  • 388628_2712905379772_1171039199_33224760_1171462869_n.jpg
    388628_2712905379772_1171039199_33224760_1171462869_n.jpg
    39.5 KB · Views: 456
Jamani,

Nisaidieni, kwa nini anajadiliwa Lowassa tu?

Nini kinaendelea? Ujenzi, ubomoaji?...kwa nini tusijadili ukombozi wa taifa letu kwa ujumla kwa jinsi ambavyo kila mtu anakiri kuwa tumefika mahali pabaya?

Kwa nini? Au vyote vimefungamana?

Kichwa kinachoka kabisa!

Nawapeni mfano mmoja...TANESCO waliingia mkataba na kampuni moja SEMCO Maritime + Rolls Royce kujenga 60 MW heavy oil plant Mwanza. Hiyo kampuni imepigwa dana dana kupewa down payments ili ianze kazi tangu 2010 mpaka leo. Kumbuka wameingia initial costs kibao kuja Tanzania. Na kama wengi wenu mlisoma mwanahalisi la juzi kuna barua wameandika na nadhani baadaye wanaweza kwenda kudai fidia/damages mahakamani, tunarudi pale pale kwa kina Dowans na hapo tena mtawasikia hao mnaowapigia debe wakija kusema SEMCO wasilipwe!

Wote tunabakia na ushabiki wa Lowassa, JK mara sijui nani ilhali hao hao ndio wanatengenezea mashimo ya kuididimiza nchi hii!

Kama Nyani Ngabu anavyosema "Miafrika ndivyo Tulivyo!"

Mpaka JF sasa inatekwa na mjadala kuhusu Lowassa?
 
pipiii piiiiiii pipiiii piii pisheni haraka gari la urais 2015 linapita lilishakata break ukijifanya mbishi utapoteza maisha. hiyo ni horn siyo ya kupuuza
:A S 465:
 
7. JK hakumtaka Bilal, lakini umoja ukalazimisha ndiye awe makamu wa rais. Mkapa alitumwa bila kuelewa.
8. Hawa watatu kwa pamoja walimteua Mkama. Wewe hujui hilo ingawa mwenzako chiligati alishastukia!
9. Membe unafahamu ya kwamba kujivua gamba ni hoja iliyoletwa na rostam kwa mara ya kwanza kwenye kikao cha watatu hao ili game iishie bungeni kwenye kujadili Richmond upya? Symbion iko nchini Membe. Unajua kaileta nani?. Je, nani kamleta Mama Clinton nchini?
10. Membe muulize Mwandosya akwambie jinsi watatu hawa wanavyomtesa. Umesahau tulipokuwa Marekani jinsi Balali alivyosema kuhusiana na chanzo cha afya yake kuzorota?.
etc, etc, etc, etc

Ushauri wangu kwa Membe
:
Be careful sana katika game hili Membe. Kama kweli unautaka urais lazima kwanza uufahamu mchezo unavyokwenda. Wenzako wanacheza game nzito na kisayansi zaidi. Know your enemy first.Na kwa kukusaidia, adui yako namba moja ni huo utatu and not an individual person

Ngoja nimeze DOCLOPAR kwanza...
 
kiukweli upinzani si watu wa kuwategemea kuleta changamoto yeyote,tazama sasa wakati hapa kila kukicha tunawasikia kuwachambua wanaotajwa tajwa kumrithi jakaya magogoni sio (lumbumba wala chimwaga)lakini upinzani hatuwasikii hata mmoja,hivi nani wanaotajwa tajwa kugombea kwa tiketi ya chadema ambacho ndicho cha tunachokitegemea sana?au wanasubiri dakika za mwisho wakati ccm wameshampata mgombea ambae wakati huo atakuwa mashuhuri tayari kupitia hili debe tunalopiga hapa magazetini,kwenye barza za kahawa na kila mahalai kuhusu mgombea wa ccm?mbona wa cdm mpaka sasa hatumsikii,amejificha wapi?maana hata mashabiki wa kutupwa wa chadema sasa wanacheza ngoma hii ya ccm,vipi kuhusu kumuandaa mgombea wao?wamemuachia nani kazi hiyo?au mwisho wa siku tunataka matokeo bila maandalizi na kuandaa mabegi ya sababu za kushindwa ikiwemo hii ambayo imeshaanza kutajwa tajwa hapa ya tume ya uchaguzi kuipendelea ccm,manazi wa chadema amkeni tokeni kwenye usingizi mzito,achanaeni na na hii ngoma ya ccm,wenzenu ndio wameshaanza kampeni ya kumuandaa mgombea wao ambayo na nyie mnaishiriki bila kujua!

Sidhani kama CDM wamekosa kazi hadi waanze kutafuta mtu wa kumnadi huku tayari wagombea wanafahamika. CCM kushinda wanapigana vikumbo kuhusu Urais ni kukosa uwajibikaji kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom