...watu walienda mbele kidogo........na unavyofikiri....hebu msome Bob hapo chini.......msifikiri watu hawakuwa wanaliona hilo..........kama alivyokulezea TR.....vita hii ni muhimu kuanza kupigana within....believe me....Mag3!
Mkuu Ogah, wengi mpaka sasa wameshindwa kunielewa. Tofauti na wengi mimi si mnafiki na sifichi chuki niliyo nayo dhidi ya CCM kwa sababu kama nilivyowahi kusema hapo nyuma naamini adui mkubwa wa taifa letu ni CCM kwa kuwalea na kuwakumbatia mafisadi na wezi wanaoifilisi nchi. Nakataa kata kata kuwa ndani hili genge la mafisadi na wezi yupo au anaweza akatokea kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kuikomboa Tanzania huku hadi leo hii, saa hii, dakika hii bado kajaa humo anashirikiana na kula nao, je anafanya nini humo chumbani ? Kama hadi sasa hana ujasiri wa kuachana nao, hana ujasiri wa kukaa mbali nao na hana ujasiri wa kusema hapana, imetosha, huo ujasiri wa kupambana nao ataupata wapi ? Huyo hatufai !
Mkuu Mkandara naona na yeye humo kwenye kundi la ambao hawanielewi ama hawataki kunielewa kwa sababu sijui Chadema inaingiaje katika hoja yake. Mimi si mwana Chadema na kusema kweli hata hao viongozi wa Chadema nawafahamu tu mtandaoni kulingana na ninayoyasoma kuhusu harakati zao za kisiasa lakini niko pamoja nao kama lengo ni kuwaondoa hawa manyang'au madarakani. Historia mpaka sasa imetufundisha sote jambo moja nalo ni kuwa chama cha siasa kikishachafuka na kuwa kimbilio la wahalifu, kitatumia tu uovu kama silaha yao kuu ya kung'ang'ania kubaki madarakani. Hivyo ndivyo serikali zote za kifashisti zinavyozaliwa, zinavyokomaa na zinavyoendeshwa zikiwaonea, kuwagandamiza na ikibidi kuwaua wananchi wake.
Ni kweli kama wanavyodai wengi, yeyote yule CCM ikimsimamisha kugombea hata akiwa chizi wa kutupwa anaweza kuibuka kidedea iwe kimizengwe au kibabe, hilo halina ubishi kwani tumeshuhudia si mara moja hii ikitokea. Lakini kwa Lowassa mambo ni tofauti kidogo na nitaeleza hili kwa kuuliza swali moja kuu, je ni watu wa aina gani hao ambao hawako tayari hata kulisikia hilo jina likitajwa na je, ikatokea hivyo, watafanya nini ? Je wachangiaji kama wewe Ogah au hata Mkandara wenye msimamo wa kutotaka kusikia hata uvumi tu wa hilo, mko tayari kufanya nini kama, God Forbid, hilo jina hilo litapendekezwa ? Kulingana na michango yenu ninayoyaona humu ndani mnaamini kwamba Raisi atakuwa Lowassa na mambo yataendelea kama kawaida.
Sisi wengine on the other hand tumeenda hatua moja mbele kwa kuitambua the weakest link kwenye hiki kitendawili nacho ni aina ya watu ambao hata leo hii hawapati usingizi jina la Lowassa linapoibuka na ndio hawa tunataka ujumbe uwafikie. Bahati nzuri ni kwamba wapenzi wakubwa wa Lowassa wako ndani ya CCM na maadui wakubwa wa Lowassa nao wako ndani ya CCM na hao wote kwa pamoja bahati ilioje kuwa kiongozi wao mkuu ni Kikwete. Hapo ndipo anapoingia mtu kama Mag3, anajua pande zote zinavyofuatilia mjadala na cheche za moto zinavyoanza kuruka ruka, lahaula, anamwaga petroli ! Jamani, adui mkubwa wa CCM ni CCM na kwa wale wenye wasi wasi naomba niwatoe hofu, turufu ya mabadiliko ni Lowassa !